Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
shusha vitu mkuu arostoooSTORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 8
SONGA NAYO............
Lile swali kidogo lilimshtua sana mheshimiwa IGP alionekana hakujiandaa kushtukizwa swali kama hilo kwa huo muda, aliguna kidogo kuliweka koo lake safi.
“Wakati lile tukio la kutumiwa sms pale mahakamani likitokea na yeye kuondoka akiwa anakimbia kama vile kachanganyikiwa hakuna sehemu yoyote ile ambayo mtu huyo alionekana japo wakati anatoka ndani ya mahakama walikuwa wote ila hatukujua alipotelea wapi na tangu hapo hajaonekana tena mpaka hivi ninavyo ongea nawewe hatujui kama amekufa au kama yupo hai?
“Mmefanya kitu gani baada ya kulitambua hilo?”
“Hakuna tulicho kifanya kwa sababu kwa sasa mambo ni mengi sana, huko tuna majukumu ya kuchunguza kuhusu mheshimiwa raisi na hili la jaji mkuu limeibukia njiani hivyo tumeamua kuanza na haya kwanza halafu kuhusu huyo mlinzi wake kama zitatoka taarifa kwamba anahusika kwa lolote basi tutahakikisha tunaanza naye ili aje atoe maelezo”
“Mbona mnafanya kazi kienyeji sana, hivi labda nikuulize swali rahisi tu una watoto wangapi?”
“Wawili”
“una ndugu yeyote kwako?”
“Ndiyo nipo na wadogo zangu wawili”
“Vipi siku ukija kusikia kwamba wameuawa halafu hujui kilicho waua ni nini kwenye mazingira kama haya utachukua uamuzi gani?”
“Lazima wahusika watatafutwa na ikiwezekana wachukuliwe hatua kali sana”
“Nadhani umeelewa kwamba mpaka sasa hakuna jibu sahihi ambalo umenijibu kwenye maswali yangu, kwa sasa naomba nipe nafasi huku chumbani naingia mwenyewe wewe utasubiri nje hapa halafu nitakuwa na mazungumzo nawewe baada ya hapa” IGP alikuwa mpole tu kwa mwanaume huyo wala hakuwa na makuu yoyote ikambidi arudi mpaka kwenye ngazi ya chini akakaa hapo na kujishika tama wakati huo mwanaume alikuwa anaingia kwenye hicho chumba ambacho kaka yake pamoja na shemeji yake aliyekuwa na mtoto tumboni waliuawa.
Aliusukuma mlango huo na kusimama akiwa anakadiria namna ndani palivyokuwa, kulikuwa na damu kiasi ambayo ilikuwa imeganda kwenye sakafu alisogelea hilo eneo na kuigusa damu hiyo akiwa anaangaza kila sehemu, macho yake yalikuwa mekundu sana alikaa chini na kutoa kitambaa alijifuta machozi yake, kuna kitu Kizito sana kilikuwa kinamkaba shingoni alisimama na kujifuta vizuri hakuhitaji mtu yeyote yule ajue kama alikuwa kwenye hiyo hali. Aliangalia kwa umakini sana hicho chumba alikumbuka namna alivyopigiwa simu na kaka yake na matukio machache ambayo aliweza kuyashuhudia siku ile, alisogea kwenye ukuta ambapo palikuwa pamejiziba vyema alibonyeza hiyo sehemu na dole gumba mara mbili pakafunguka ndani yake kulikuwa na kichuma kilicho mhitaji kuingiza namba za siri alifanya hivyo kwa kuingiza tarehe yake ya kuzaliwa na mwaka wake pakafunguka na kukutana na makablasha mengi sana hakuyajali kwa wakati huo alivuta droo ndogo ndani ya hicho chuma humo ndani kulikuwa na funguo nyingi sana, baada ya kuipata ile ambayo alikuwa anaitafuta yeye alifunga hapo ndani kisha akatoka mpaka kwenye kordo moja ndogo huko huko juu alijongea kwa mita sita tu akawa ameufikia mlango mwingine, aliingia mpaka ndani, hiki ndicho kilikuwa chumba cha maktaba ya kaka yake, kulikuwa na vitabu vya kila aina hususani vya sheria ndivyo vilivyokiwa vimejaa huko ndani.
Aliisogelea hilo kabati kubwa sana la vitabu, aligeuka nyuma kama hakuna mtu ambaye alikuwa anamuona alilizungusha likasogea pembeni hapo palikuwa na mlango wa shaba alitoka kifaa muundo wa simu ila haikuwa simu alipitisha kwenye kitasa cha huo mlango, alijiridhisha baada ya kuona kwamba hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa ameugusa mlango huo, akaparudishia kama palivyokuwa mwanzo kisha akafunga hicho chumba na kushuka mpaka pale ambapo alikuwa amekaa IGP alionekana kuwa kwenye mawazo mazito sana.
“Naomba hiyo simu ya brother, baada ya hapo nipeleke huko hospitali iliko hifadhiwa miili yao na hakikisha nakutana na daktari aliye ipokea miili hiyo na kuishughulikia pamoja na huyo askari ambaye alikuwa hapa nyumbani wakati tukio limetokea, hayo yakikamilika sasa nitaomba nikae tena mimi na wewe unieleze kwa kirefu kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa mheshimiwa raisi” Jason aliongea kwa sauti kavu sana ambayo alikuwa na uhakika na anaye ongea naye kwamba alikuwa anamsikia vizuri tu wala hilo halikumpa sana shaka, IGP alinyanyuka na kuuingiza mkono wake kwenye mfuko alitoka na simu hiyo ambayo kiasi fulani ilikuwa imepasuka na kuonyesha kwamba ilikanyagwa tena kwa makusudi kabisa, mwanaume aliipokea halafu wakaongoza nje wote ili waweze kuelekea huko huspitalini kama walivyokuwa wameelekezwa.
Walitoka mpka nje wakiwa pamoja jambo ambalo liliendelea kuleta taharuki kwa maaskari ambao walikuwa nje
“Mheshimiwa huyo mtu ni nani? tumepewa jukumu la kukulinda kama likikukuta tatizo lolote lile sisi tunaingia matatizoni, huyo ni mtu ambaye amekuja hapa kwa namna ambayo haieleweki na mpaka sasa hatuelewi kwamba anafanya nini hapa na yupo hapa kwa ajili ya nani na hata wewe hautupi majibu sahihi” mheshimiwa Lusubilo Mtindiga hakujibu kitu baada ya kuisikia kauli hiyo kutoka kwa kijana wake zaidi zaidi alimsogelea mpaka pale alipokuwa amesimama, alimwangalia sana kisha alimtandika makofi kama Matano ya haraka haraka ambayo yalimfanya kijana yule ahisi amebeba kilo kadhaa za mchanga kwenye mashavu yake kwa namna yalivyokuwa yanawasha, mheshimiwa hakuongea neno lolote aliondoka na kuingia kwenye gari ambayo tayari Jason alikuwa ameingia na IGP alikaa kwenye usukani akiwa anaendesha yeye mwenyewe hiyo gari, walinzi wake walibaki wameduwaa tu.
“Huenda wako sahihi kuhitaji kumjua mtu ambaye muda wote yupo na kiongozi wao na hawana uhakika wa usalama wa kiongozi wao, natamani sana kama wangekuwa makini sana kwenye kila jambo la nchi namna hiyo ila inasikitisha sana linapokuja suala la kuijenga nchi wanakuwa wanazingatia zaidi kuyajenga matumbo yao na si vinginevyo na hapo usikute kijana anatafuta ni cheo” Jason aliongea huku akiwa anaiangalia kwa umakini sana picha ambayo ilikuwa kwenye mkono wake, alikuwepo yeye, kaka yake, mke wa kaka yake pamoja na mtoto wa kwanza wa kaka yake ambapo picha hiyo ilipigwa mtoto huyo akiwa bado mchanga, aliiingiza kwenye mfuko wake wa suruali na kutulia kuendelea kuangalia mazingira ya nje jinsi yalivyokuwa.
“Kama tu uliweza kumficha kaka yako wa damu ambaye ni nusu ya maisha yako, mheshimiwa raisi hakutaka mtu yeyote ajue kuhusu wewe, ni marafiki wachache sana ambao tulibahatika kulijua hili sasa itakuwa hao watoto ambao wanakuja kufanya kazi kwa sababu ya njaa na sio weledi wa kazi? Nadhani wewe mwenyewe utakapo amua wakujue wewe ni nani itakuwa ni vyema zaidi na ukizingatia ni watu wachache sana ambao wanajua wewe ni mdogo wake toka ni toke na jaji mkuu ndiyo maana wanakushangaa, hili tukio ndilo linalo Kwenda kukutambulisha kwamba wewe ndi ndugu yake na jaji kwa sababu serikali imetangaza kukusaidia kama ndugu yake lakini watu wengi hawakujui hivyo kwenye utambulisho lazima utatangazwa na kama unavyojua yule alikuwa ni mtu mkubwa sana hivyo vyombo vya habari vitakuwa vingi sana” IGP aliongea akiwa yupo makini sana kuangalia mbele mikono yake ikiwa ipo kwenye usukani wake.
“Ndiyo maana kaka yangu alikataa sana nisisome sheria kwa sababu aliyajua madhara yake kama haya, najiona kama ni mtu wa hovyo sana kuweza kushindwa kuilinda familia yangu mimi mwenyewe ambayo ndiyo pekee niliyokuwa nayo, wananchi hawatakiwi kabisa kujua uhalisia wangu zaidi watajua tu kama mimi ni ndugu yake na jaji mkuu basi. Mpaka sasa nimechanganyikiwa sijui naamua kipi nakiacha kipi, hakuna kitu kinauma kama kuipoteza familia ambayo ndiyo pekee ulikuwa ukiitegemea kwa kipande kidogo cha furaha cha maisha yako kilicho bakia kukiishi inauma sana tena sana, moyo hauwezi kuongea ila huwa unatoa ishara kwa kupitia macho na baadhi ya sehemu za mwili, najiona mkiwa sana kwenye haya maisha ila niseme tu nikushukuru sana wewe na wengine ambao mlikuwa marafiki wema sana kwa kaka yangu. Nimepatwa na Mikasa mizito sana nimempoteza mheshimiwa raisi ambaye amehusika kuyatengeneza maisha yangu kwa asilimia 40 na zilizo salia zote alizitengeneza kaka yangu lakini kabla hata sijajua nafanyaje kuhusu hilo wameamua kunichukulia pacha wangu, yule kwangu hakuwa kaka tu alikuwa kama pacha, alikuwa kama baba, sikuwahi kuijua shida kwa miaka mingi sana japo tumeishi kwenye maisha ya shida sana”
“Alikuwa tayari kulalia kikombe cha maji yule mwanaume ila hakuwahi kuruhusu mdogo wake nilie kisa njaa, kwangu alikuwa role model wangu na ndiyo mfano bora zaidi ambao nitaufuata siku zote kwenye maisha yangu lakini pamoja na yote ambayo ameyafanya haya bado mpumbavu mimi nimeshindwa kumlinda kabisa. Nitakuwa na dhambi kubwa sana ya Kwenda kujibu kwa MUNGU kama sitageuka na kuwa mtu katili sana kwa sasa MUNGU anisamehe sana kwa sababu naenda kuyaanza maisha yangu mapya kwa kuugeuzia mgongo wema wangu ambao nimeutenda kwa binadamu wasiokuwa na shukrani kwenye haya maisha” Aliongea kwa uchungu sana IGP alikuwa anamtazama kijana huyo na kumuonea sana huruma, walikuwa wamefika tayari ndani ya hospitali ya taifa ya Mhimbili, walishuka na kuanza kuelekea ndani ambapo walikumbana na waandishi wa habari waliokuwa wengi sana baada ya kumuona IGP walimtaka aseme chochote kile kwa kila kilichokuwa kimetokea kwa sababu juzi tu kwenye hospitali hiyo uliletwa mwili wa mheshimiwa raisi ambao jana yake ulipelekwa ndani ya makao makuu ya jeshi la wananchi na jana hiyo hiyo kwenye hospitali hiyo hiyo ulikuwa umeletwa mwili wa mheshimiwa jaji mkuu hivyo taharuki ilikuwa ni kubwa sana hata hivyo hakuna alicho wajibu mzee huyo zaidi zaidi askari walimsaidia kumtengenezea njia yeye na Jason mpaka wakafanikiwa kupita hapo na kuingia ndani, walipanda lifti na kuelekea kwenye vyumba vya VIP huko ndiko ilikuwepo hiyo miili ya ndugu zake .
“Dokta samahani sana huyu hapa ndiye ndugu wa pekee wa marehemu ambaye ulipewa taarifa zake kwamba alikuwa nje ya nchi na ndo amefika saivi hivyo yupo hapa kwa ajili ya kuiona miili ya ndugu zake kabla ya Kwenda kuzikwa hapo kesho hivyo naombeni sana mpeni ushirikiano kwa kila anacho kitaka” Daktari alimpa mkono IGP na kuonyesha kwamba alikuwa amemuelewa vizuri sana na hilo jambo angelifanyia kazi kwa muda mfupi ujao, alimchukua Jason akatoka naye nje ya chumba chake na kuelelea naye mkono wake wa kulia, walitembea kwa sekunde thelathini tu kisha wakakunja mkono wa kushoto huko walianza kukumbana na hali ya ubaridi sana ila mwanaume huyo alikuwa siriasi sana hakuwa ametamka neno lolote lile tangu aingie ndani ya hospitali hiyo.
Daktari huyo alifungua moja ya mlango ambao ndani yake kulikuwa na baridi kali sana
“Sasa wewe waweza Kwenda nahitaji kuwa pekeyangu humu ndani” Dakatari alishtuka mtu huyo alovyosema kwamba anahitaji kubaki yeye mwenyewe, alitaka kuongea kitu ila aliyakumbuka maneno ya IGP kwamba mtu huyo asikilizwe kwa kila ambacho alikuwa anakitaka yeye hivyo ilimlazimu kuondoka na mwanaume akausukuma mlango na kuufunga na komeo kwa ndani, mbele yake yalikuwa ni majokofu ambayo yaliandikwa majina ya familia yake, moja lilikuwa la kaka yake, shemeji yake na mtoto wa kaka yake, alihesabu hatua tatu mpaka lilipokuwa jokofu ambalo lilikuwa na jina la kaka yake, alilifungua lakini alicho kiona kilimshtua sana.
Jason kaona nini? yeye ana nini hasa mpaka hataki kujulikana? Siri gani hizo ambazo anazo alimficha hata kaka yake? Atamjua mhusiKa? Na vipi kuhusu raisi alikuwa na mahusiano naye gani mpaka aseme kwamba amechangia kumtengeneza kwa asilimia 40?.INNOCENT KILLER sehemu ya 8 natia nukta.
Bux the storyteller.
Chuma kabisa hiki, umetisha sana mkuuSTORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 9
SONGA NAYO............
Jason kitu alicho kiona baada ya kuuona mwili wa kaka yake kilimfanya aume meno kwa hasira sana, aliuangalia kwa dakika kumi bila kukwepesha macho yake. Mwili huo ulikuwa na tobo la risasi kwenye paji la uso wa kaka yake, alisogelea sehemu ambapo lilikuwa limeandikwa jina la shemeji yake napo aliangalia kwa umakini sana na kuona kitu kile kile risasi ilipita kwenye paji la uso.
Alikumbuka vizuri kwamba shemeji yake alichomwa na kisu maeneo ya tumboni aliyafumba macho yake akijaribu kuvuta hisia kwa mtu kukosa huruma mpaka kufikia hatu ya kuweza kumchoma kisu mwanamke mjamzito namna hiyo, inahitajika mtu kuwa na roho ngumu sana.
Alienda kumalizia kwenye jokofu lililokuwa na jina la mtoto ambaye alikuwa anapenda sana alivyokuwa anamuita baba mdogo, huyo ndiye pekee aliwahi kumfanya naye ajihisi ni baba kwenye hii dunia, alivuta taratibu sana kuonyesha kwamba hakuwa tayari kuona kilichokuwa mbele yake ila hakukuwa na namna alihitaji kujihakikishia mwenyewe kile ambacho kilikuwa kimetokea, mtoto alikuwa ameyafumba macho kama vile alilala na angeamka ila ni kitu ambacho kilikuwa ni ndoto tu na isingewezekana kuwa kweli hata kama ungekuwaje.
Kama alivyokuwa ametegemea hata huo mwili pia ulikuwa una risasi kwenye paji la uso, aliinama na kumbusu mtoto huyu kwa dakika nzima akiwa ameinamisha uso wake hapo alinyanyuka na kuanza kuzunguka humo ndani kama mtu aliye changanyikiwa mpaka akaenda kukaa kwenye kona ya hicho chumba cha kuhifadhia maiti licha ya kuwepo kwa baridi kali sana humo ndani ila kwake haikuwa sababu ya msingi sana ya kumfanya kutoka haraka.
Yaliisha masaa mawili mazima ndipo mlango huo ulipo funguliwa na mwanaume huyo akatoka na kuurudishia mlango kama ulivyokuwa, alitembea taratibu mpaka kwenye ile ofisi ambayo kwa mara ya kwanza alipelekwa na IGP, aliingia bila hata kugonga na kumfanya IGP na daktari huyo kushtuka sana hawakujiandaa na ujio wake humo ndani.
“Nina maongezi nawewe nifuate” aliongea na IGP kisha akatoka nje kumsubiria mtu wake huyo, IGP alibaki anaangaliana na daktari tu mle ndani
“Hivi huyu ndiye mfiwa kweli? Mbona hana hata wasiwasi wala dalili za kuonyesha kwamba ni mtu mwenye majuto kupotelewa na familia yake? Halafu mbona kama anakuchukulia kawaida sana kwamba hajui kama wewe ni kiongozi mkubwa kwenye nchi hii” daktari alimuuliza IGP akiwa anajiandaa kutoka Kwenda kuongea na mtu wake huyo, IGP aligeuka na kulazimisha tabasamu
“Jambo usilo lijua ni sawa na usiku wa giza hivyo kuna mambo usilazimishe kuyajua yatakuja kuhatarisha maisha yako, kuhusu familia hakuna binadamu ambaye anafiwa na familia anayo ipenda sana halafu akafurahia au kuwa kawaida sema kuna watu wamefunzwa kuwa wanaume unaweza ukamuona anacheka sana ila moyo wake unalia kuliko unavyo fikiria wewe shida yako umezoea sana hizo kazi za kubembelezana na wagonjwa hivyo hata kulia kwako ni rahisi sana yule hayupo vile mpaka unamuona yupo siriasi sana jua ni mtu ambaye anatokwa machozi kila dakika ila hayo machozi wewe hapo huwezi kuyaona kwa sababu umechagua kuyaamini sana macho yako kuliko hisia” IGP alijibu kwa mafumbo na kumuacha daktari huyo kwenye njia panda wakati huo aliubamiza mlango huo na kutoka nje ambapo alikohoa kidogo baada ya kumkaribia Jason ili kumpa taarifa kwamba alikuwa amefika.
“Kwanini unanipa taarifa nusu nusu?” swali la Jason lilimshtua kidogo mheshimiwa
“Una maanisha nini kusema hivyo?”
“Unajua wale waliokufa ni akina nani kwangu?
“Ni familia yako”
“Sasa mbona unanipa taarifa kama vile nimefiwa na jirani yangu au mtumishi mwenzengu?”
“Taarifa ipi hiyo ambayo wewe unaihitaji na haujaipata kama ulivyokuwa umetarajia?”
“Umenipa maelezo mengi sana lakini hakuna sehemu ambayo umenielezea kwamba familia yangu imekufaje na hicho ndicho nilichokuwa nakihitaji”
“Bado sijakuelewa”
“Una kichwa Kizito sana sijui ulipewaje hiyo nafasi”
“Sasa nafasi yangu inahusiana vipi na swali lako?”
“Nimekuuliza walikufaje? Mbona hujanambia kama miili yote ilimuwa na risasi kwenye kichwa”
“Daaah nilikuwa mbali sana haya majukumu naona kabisa kwamba yananizidi sasa ndiyo maana hata sikuwaza huko kwa sababu nilijua utayapata kwenye ripoti ya madaktari wanavyokupatia taarifa ya vifo vyao”
“Mhhhhhhh kiwepesi tu namna hiyo”
“Yes, imegundulika kwamba wote mpaka walinzi walipigwa risasi za kwenye paji la uso ndiyo maana nilisema kwamba muuaji ni mmoja tu na sio wengi kwa sababu aina ya mauaji iliyotumika ilikuwa ni moja tu basi”
“Sijajua kwamba ni kwanini kiwepesi tu namna hiyo ulininyima hizo taarifa ila kwa sasa nahitaji niandaliwe hiyo ripoti na daktari nitakuja kuichukua na huyo daktari mwenyewe nitahitaji kukutana naye, pia utanipa namba ya nyumba ya huyo askari ambaye alifika pale mapema sana kuja kufanya uchunguzi baada ya tukio, hivyo sivihitaji saivi labda tu namba ya nyumba ya huyo askari nitumiwe ndani ya muda mfupi ila ripoti ya daktari naihitaji siku moja baada ya msiba”
“Kwa muda huu hapa nina vitu viwili, kitu cha kwanza naihitaji hiyo video ambayo inaonyesha mheshimiwa raisi akishambuliwa na huyo mtu mpaka kufa na kingine nataka kujua kwanini ulinambia uongo” ishu ya video IGP hakushtuka sana japo alisita ni kama alitarajia mtu huyo angeiomba tu kwa namna yoyote ile ila kilicho mshtua sana ile ya kusema kwanini alimwambia uongo, alibaki anawaza uongo upi wakati asilimia zote alikuwa anatoa maelezo ya kitu ambacho anakijua? Ilimbidi alijibu ili asije akashtukiwa.
“Uongo upi huo ambao unausema?” Jason alimwangalia sana mzee huyo
“Najua kwenye ile simu hakukuwa tu na zile sms tatu kama ulivyosema wewe, kuna sms uliamua kuzimezea na sijajua kwanini na kwa sababu zipi, hilo utaenda kujitafakari mwenyewe kisha tutaongea vizuri siku nyingine kwa sasa nionyesha hiyo video ya kuuawa kwa raisi” Aliongea bila kitetemeshi chochote kile, IGP hakuongea kitu chochote zaidi alinyoosha kwenye njia ambayo ilikuwa inawapeleka kwenye lifti, walishuka mpka chini na kuelekea kwenye gari yake ambapo waliingia na kufunga milango yote, alitoa simu kwenye droo yake na kumpatia Jason ambaye aliifungua na kuangalia kwa dakika tano video hiyo fupi ambayo ilikuwa inajirudia rudia.
“Pumbavuu, inawezekana vipi raisi wa nchi auawe kirahisi sana namna hii?” aliongea kwa hasira sana akiwa amemkazia macho IGP ambaye alibaki ameinama tu
“Si nakuuliza wewe hapo au haunisikii? Nitajibu vipi hili suala kwa watu ambao mliaminika mtamlinda huyu mtu ndo mkaacha afe kizembe sana namna hii, shiiiiiiit this is lunatic” alifoka kwa hasira sana Jason na mzee huyo ambaye kwa umri alikuwa mkubwa sana alikuwa ametulia tu akimsikiliza kijana huyo hakutaka kabisa kumuingilia kwenye hizo hasira zake.
“Ok kama huwezi kunijibu hilo kwanini mmeruhusu ahukumiwe mtu ambaye siyo muuaji? Ina maana huu ulikuwa ni mpango endelevu wa kumuua na kaka yangu sio?” hayo maswali ya Jason yalimshtua mzee huyo baada ya kusikia kwamba walikuwa wamemhukumu mtu ambaye alikuwa hahusiki na chochote kabisa
“Mbona sijakuelewa”
“Mzee ujue nakuheshimu sana na nadhani unajua miongoni mwa vijana ambao huwa wanakupenda sana namimi nipo na unalijua hilo ila usitake tuende kuwa maadui hapo mbeleni nitakusahau kama sijawahi kukuona kwenye maisha yangu. Ni nani ambaye alimkamata huyo mtu ambaye amenyongwa kama muuaji? Nani alifanya huo uchunguzi?”
“Tulipewa taarifa kwamba huyo muuaji alikamatwa na jeshi la wananchi hivyo sisi hatukuwa na namna zaidi ya kufuata mamlaka zilizokuwa zimemshikilia kwa sababu walituambia itabaki kuwa hivyo na hapo ndipo tulipo ingilia kati kuanza kufanya uchunguzi lakini tulizuiliwa na kuambiwa kwamba watu wa ikulu watahusika na hilo na sisi tutashughulika na mengine ambayo yataendelea mbele” IGP alijibu jibu ambalo ni kama mtu huyo lilimuacha njiapanda sana kwa namna alivyo jibiwa kiwepesi sana
“Huyo aliyewapa hiyo amri ni nani?”
“CDF alitupatia hiyo taarifa kwamba imeamuliwa iwe hivyo”
“Huyo CDF anahusika nini na mheshimiwa raisi mpaka yeye ndiye atoe amri ya taarifa ya uchunguzi? Na yeye anahusika nini na ikulu? Sasa naomba umpe taarifa kwamba leo usiku nataka nikutane naye tukiwa wawili tu, akiukuuliza nani mwambie mdogo wake jaji anakuhitaji sana kuliko hata maisha yake nadhani yeye ndiye aje anipe hayo majibu sahihi”
“Sawa hilo nalifanyia kazi lakini sijakuelewa ulivyosema kwamba amehukumiwa mtu ambaye hahusiki” IGP alihitaji sana kuzijua hizo taarifa
“Kaka amekufa baada ya hukumu na yule mtu kunyongwa sio?”
“Ndiyo”
“Umeona namna raisi alivyokufa”
“Ndiyo alipigwa risasi”
“Ya wapi?”
“kwenye paji la uso”
“Na familia yangu imeuliwa vipi?”
“Kwa risasi za paji la uso” hapo sasa hata IGP akili yake ilifunguka, alijiona kuwa ni mzembe sana kushindwa kung’amua hicho kitu mapema ni mchezo mdogo sana ambao hata mtoto mdogo anaweza kuutegua bila hata kutumia nguvu.
“Muuaji hapa ni mmoja, maana yake mtu aliyeweza kumuua mheshimiwa raisi ni yule yule ambaye aliiua familia yangu, sasa kama alikamatwa na kunyongwa kivipi aue familia yangu baada ya kufa? ni kitu ambacho hakiwezekani inamaanisha huyo mtu yupo hai ila kuna mchezo tu wa akili ndogo wameamua kuucheza sasa naingia mimi mwenyewe kwenye huu mchezo nikacheze nao hilo draft ambalo wamelichora wao wenyewe na sheria wamezitunga wao wenyewe” aliongea kwa msisitizo sana Jason akiwa anaufungua mlango ili atoke humo ndani.
“CDF nimwambie mkutane saa ngapi?”
“Mwambie saa 6 kamili usiku nitakuwa nje ya nyumba yake na unitumie namba ya nyumba ya huyo askari wako muda huu” mwanaume aliongea hivyo na kuondoka IGP alibaki anashangaa jasho likiwa linamtoka, kwa muda mfupi sana aliona mambo yanaenda kuwa mabaya kuliko hata ilivyokuwa imekadiriwa, alichukua simu yake na kuitafuta namba ambayo alikuwa ameisevu Jaiwelo Mkupi Makubilo huyu ndiye ambaye alikuwa CDF mwenyewe mkuu wa majeshi, aliruhusu simu hiyo iweze kupiga, iliita kidogo na kupokelewa.
“Nakuja kwako ndani ya dakika thelathini zijazo” hakusubiri hata kujibiwa alikata simu na kuwasha gari yake kisha akaondoka kwa kasi sana hilo eneo.
Jason Japhary ni nani huyu kijana mpaka anajiamini sana namna hii mbele ya watu wakubwa sana serikalini kama hawa wakati kuna watu wanamjua kama ni kijana laini sana asiye na makuu na mtu waweza kumuita mtoto wa mama? ……. bado tupo taratibu twende pamoja michezo ya akili imeanza tukaitafutie majibu halisia.
Bux the storyteller.
Ahsante sanaaaaaa
Hatari sanaSTORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 10
SONGA NAYO............
Ndani ya dakika thelathini na tano mheshimiwa IGP alikuwa anaingia getini kwa CDF gari yake ilikuwa inajulikana sana hivyo alifufuliwa geti bila wasiwasi, baada ya kushuka alinyoosha moja kwa moja mpaka sehemu ya nyuma ya nyumba hiyo, alikuja mwanamke mmoja mzuri sana ambaye alimletea kahawa ambayo ndiyo ilikuwa kitu pendwa saa kwa mzee huyo kisha akampa maelekezo kwamba mtu huyo alikuwa hayupo wakati anampigia simu hivyo atarudi ndani ya dakika 15 zijazo, haikuwa shida sana kwake kuweza kusubiri hapo huku akiendelea kupata kahawa yake.
Dakika ishirini zilitosha kusikia hatua za buti kubwa ambazo hakuwa na shaka na mtu ambaye alikuwa amezivaa, alijua ni mkuu wa majeshi ndiye ambaye alikuwa amefika hiyo sehemu, akiwa anaangalia mbele sehemu ambayo ilipandwa miti mizuri kwa mpangilio iliyokuwa karibu na bwana la kuogelea ambayo iliifanya sehemu hiyo kuwa ya kuvutia sana alitamka kwa sauti moja ya utulivu sana.
“Kila nikisikia kuhusu hizo hatua za hivyo viatu basi huwa nakumbuka mbali sana, mwaka ule tupo kwenye mafunzo ya jeshi kule Msangi Tabora tulikuwa watu watano ambao tulishibana kwa kila kitu, siku ile rafiki yetu mmoja alipo kufa kwa sababu ya kukuokoa siwezi kuisahau kabisa ile ni moja ya stori mbaya sana kwetu lakini ni kumbukumbu moja nzuri sana kwenye maisha yetu sisi kama marafiki” alivuta pumzi kidogo kuacha hayo maneno yamuingie vyema mtu ambaye alikuwa akimpa hiyo taarifa.
“Tuliingia kwenye orodha ya marafiki bora zaidi kuwahi kutokea hapa duniani, tulibaki wanne ambao tuliapa kubebana na kusaidiana kwenye kila hatua ambayo tungeipiga kwenye maisha yetu na ilibaki kuwa hivyo hata pale mwenzetu alipo fanikiwa kuwa raisi wa nchi basi hakuweza kabisa kutuacha alimpa kila mtu kitengo ambacho alikuwa anakihitaji na kukielewa kwa upana lakini kati yetu wote tulikuwa tunamtegemea sana jaji mkuu kwa sababu ametusaidia sana na ndiye mtu ambaye tulikuwa tunamtegemea kwenye kila mpango wetu, alikuwa ni mtu mwenye akili zaidi kati yetu sisi wanne lakini hata hivyo imekuwa pigo kubwa sana kuwapoteza marafiki wote wawili tena kwenye mazingira ya kutatanisha sana na kwa muda mfupi mno” aliongea na kushushia kahawa yake, mkuu wa majeshi alikuwa akisikiliza huku amesimama akiwa ndani ya kombati ya jeshi ambayo ilimpendeza sana pamoja na buti kubwa sana nyeusi ambayo ilikuwa imesafishwa vizuri mno begani kwake kukiwa kumejaa nyota za vyeo mbali mbali, aliisogea pembeni na kuketi kwenye hicho kiti ambacho kilikuwa kinawatosha watu wawili akaingiza mfukoni na kutoa pombe ndogo lakini kali sana ambayo ilikuwa kwenye kibati akamkabidhi rafiki yake huyo kama alivyo dai na kuendelea kuinywa ya kwake huku akiwa anakunja uso wake kwa ukali wa pombe hiyo.
“Maisha hayana tafsiri halisi ila namna tunavyokuwa tunayaishi ndivyo yanavyotupa tafsiri sahihi ni namna gani tunapaswa kuyachukulia, hiki ndicho kitu pekee ambacho ninaweza kukifanya kwa ajili ya rafiki ambaye aliamua kuyatoa maisha yake siku ile kwa ajili yangu, ile kamba ambayo alinirushia na yeye kuamua kudondoka ili mimi niidake na kupona yeye akaishia kudondokea kwenye yale mawe yaliyokuwa yamechongoka sana basi huwa inanifanya niumie sana ila kwa baadae nilikuja kugundua kwamba kwenye maisha kila kinacho toke abasi huwa kina sababu nzito sana nyuma yake huenda mimi kubaki hai kulikuwa na sababu nzito sana na hiki ndicho ambacho mimi huwa nabaki namuenzi”
“Alikuwa anaipenda sana hii pombe na tangu siku ile amekufa basi mimi niliapa kwamba ningeinywa hii pombe mpaka siku naingia kaburini na ndicho ambacho huwa nakifanya kila siku mpaka sasa. Kuwa na marafiki ambao kwako ni kama familia huwa ni kitu bora zaidi kwenye maisha ya mwanadamu hususani unapokuwa unapata nafasi ya kufurahi pamoja na hao marafiki zako, kama ulivyosema tuliishi zaidi hata ya ndugu kwa sisi wanne ambao tulikuwa tumebaki na ndiyo maana mpaka leo wote tumeishi maisha mazuri sana kwa sababu tuliamua kumpigania mmoja kutimiza ndoto yake kisha na yeye akatutimizia ndoto zetu sisi ila kama tungeamua kila mtu aanze kuwa na wivu na mwenzie basi saivi usikute tungeishia kuwa wapiga debe kama sio kuwa vibaka huko mtaani ila kwa sasa tunachagua tule nini na nchi gani tuende kwa sababu tuna kila kitu kwenye maisha, ni wakati mgumu sana tutapitia kuwapoteza hawa watu wawili mhimu sana kwenye maisha yetu nitawaombea siku zote huko waliko waweze kupumzika kwa amani kwa maana wamefanya mambo makubwa sana kwetu na kwa nchi yetu pia” mheshimiwa CDF aliongea akiwa anaongeza kinywaji kingine kwenye mdomo wake na kumfanya IGP atabasamu kwa maumivu kwa sababu sio kwamba walikuwa wanafanya mazungumzo ya kuweza kufurahishana ila bali mazungumzo yao waliamua kujikumbushia zaidi nyakati za furaha ambazo wao waliziishi wakati wapo na wenzao.
“Nilikuwa najua kama kuna kufa ila sikuwahi kuwaza kama tutakuja kuanza kupotea mmoja mmoja kimaajabu na kwa vifo vya kutisha sana namna hii inanifanya naanza kuogopa sana kwa sababu sijui kama kesho utafuata wewe au nitakuwa ni mimi, kuna muda natamani niendelee kuaiamini dunia lakini nashindwa najikuta hata nafsi yangu siiamini bado na sina jibu la kujipa. Hivi unafanya nini pale yule mtu ambaye ni wa mhimu sana kwenye maisha yako halafu unakuta ana ukakasi mkubwa kwenye kuyapunguza maisha ya watu wengine ambao nao ni wa mhimu kama yeye kwenye maisha yako pia?” IGP aliuliza kitu ambacho kilimshtua sana CDF lilikuwa ni kama swali la mtego hata hivi hakuhitaji kuonekana kwamba yeye ndiye kashtuka sana, aliangalia juu angani kisha akayarudisha macho yake chini.
“Kama huyo mtu anaweza kuleta madhara makubwa kwa wenzie basi ni wazi hatatakiwa kuwepo kati yao au kati ya watu wa aina yoyote ile kwa sababu hatakuwa sehemu ya furaha ya binadamu wenzie zaidi atasababisha hata ile furaha ndogo iliyopo kwa wenzake kutoweka hivyo hatakiwi kuwepo kwenye kundi la hao watu kwa namna yoyote iwe kwa nguvu au kwa kupenda inabidi atolewe” IGP alikuwa anasikiliza kwa umakini sana hayo maelezo, alikunywa tena hiyo pombe mpaka alitokwa na machozi kwa namna pombe hiyo ilivyokuwa kali.
“Hii pombe inatakiwa kuinywa kwenye baridi ina joto kali sana, sasa vipi kama huyo mtu yupo miongoni mwetu mimi na wewe inakuwaje?” aliuliza wakati huu akiwa anamkazia macho CDF, CDF alimshangaa mtu huyo kwanini anampa hayo maelekezo
“Una maanisha nini?”
“Unajua wewe ni rafiki yangu tena zaidi hata ya rafiki tumeshakuwa ndugu tayari naomba uniambie ni kitu gani ambacho unanificha kwenye hii kesi ya jaji mkuu kuweza kuuawa?”
“Mhhhhhhhh kwahiyo una amini mimi naweza kukuficha nini kuhusu rafiki yangu mwenyewe, inamaanisha kwamba siku hizi hauniamini kiasi hicho ndugu yangu?”
“Wala sio hivyo hakuna sehemu hata moja ambayo nimesema sikuamini, unajua kwa kilicho tokea Mark kuweza kuuawa nyuma yake kuna mambo ya siri ambayo yanaendelea, baada ya lile tukio tuliipata simu yake ile simu niliipeleka kwa vijana wangu ili tuweze kujua kama labda kuna watu alikuwa ana matatizo nao kabla ya kupatwa na umauti, ni kweli ilikuwa hivyo kuna namba ilimtishia usiku mmoja kabla ya kesi kwamba kama akifanya kitu cha hovyo na kumhukumu yule mfungwa basi anauawa yeye na familia yake jambo ambalo liliendelea mpaka asubuhi kabla hajaingia kwenye chumba cha kusikilizia kesi na hata baada ya kutoka huko kuna sms ambayo ilimtaka aweze kufika kwake ndani ya dakika 15 ili aiokoe familia yake” alikohoa kidogo kisha akaendelea
“Lakini kwenye zile sms ambazo zilipatikana pale kuna sms ambayo kabla ya kuingia kwenye kesi ilitumwa muda mmoja na ile nyingine ya kumtisha na kumuahidi bilioni kumi lakini hata baada ya kutoka mle ndani kuna sms nyingine ambayo ilitumwa sambamba na ile sms tena, baada ya uchunguzi namba ambayo ilitumika ni ya kwako mwenyewe, baada ya kulijua hilo nikaamua kuchukua ushahidi wote huo na kuwapa vijana majukumu mengine, sasa nahitaji uniambie ukweli vipi unahusika kwenye hili jambo la kumuua Mark na kama ni kweli kwanini? Kuna nini mpaka ufikie hatua ya kumpunguza ndugu yetu?” maelezo na maswali mfululizo ambayo aliulizwa yalimfanya kwanza ainame kwa muda wa dakika tano kisha akanyanyua uso wake na kumwangalia IGP
“Siwezi kumuua mtu wa karibu kwangu kama yule, namuua kwa sababu ipi? Namuuaje rafiki yangu ambaye tumetoka kwenye sifuri naye pamoja? Mimi sipo kwa ajili ya kuua watu mimi nipo kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wa nchi hii wapo salama, mipaka ya nchi ipo salama na hata mheshimiwa raisi yupo salama sasa naanzaje kumuua Mark? Mimi nilifanya vile kwa sababu nilijua ile video italeta matatizo makubwa sana ndiyo maana nikamwambia asifanye yale maamuzi” alitulia baada ya kujibu, IGP alimwangalia sana rafiki yake kwa sababu alimpa majibu mepesi sana.
“Mimi sijajia hapa kwa sababu ya hilo jambo kama kutakuwa kuna umuhimu wa kuliongelea basi tutakutana mimi nawewe ila kama utanificha basi linaweza kuja kukuletea matatizo makubwa sana kwa sababu sasa halipo kwenye mikono yangu lipo kwenye mikono ya mtu mwingine ambaye naye kaahidi kulifuatilia mwenyewe”
“Mhhhhhh nani huyo?” swali lake lilimfanya IGP amwangalie sana mwenzake
“Jason”
“Ndo nani?”
“Wanadamu huwa tunabadilika sana hivyo sikushangai kusema humjui huyo kijana, nakukumbusha tu Mark udhaifu wake mkubwa ulikuwa unaujua?”
“Daaah nilikuwa mbali sana yule bwana mdogo si alikuwa kusoma?”
“Sasa ataendelea na masomo na **** msiba wa kaka yake?”
“Enhe sasa yeye anahusikaje na hili? Kwa sababu yeye kaahidiwa kusaidiwa kila kitu na serikali na hata sisi hatuwezi kumtupa tutampatia kila kitu ambacho yeye atakuwa anakihitaji”
“Sasa huyo ndiye ambaye amesema hili suala anaenda kulifuatilia kwa mkono wake mwenyewe”
“Inawezekanaje na vyombo vya usalama vipo? Anaanzia wapi yule ambaye haijui sheria hata kusema A inasemaje anaenda kumfuatilia nani zaidi atajiingiza kwenye matatizo tu hivyo hatutakiwi kabisa kuruhusu hilo jambo liweze kutokea, haiwezekani tusije kumpoteza kama kaka yake”
“Mhhhhhhh wewe ni mkuu wa majeshi ndiyo lakini una uhakika gani kwamba hiyo sheria haijui?”
“Yule mtoto nilikuwa nakutana naye mara chache sana muda mwingi huwa ni mtu wa kuzunguka nchi za watu kusoma huko sasa hiyo sheria anaijulia wapi na sijawahi kumsikia wakisema anasomea sheria, si anasomea uhandisi yule mtoto”
“Sasa huyo ndiye ambaye amenifanya nije hapa siku ya leo kukufuata na kama siyo yeye tusingekutana kwa wakati huu hapa” CDF alizidisha umakini ili aweze kuzipata habari hizo
“Anataka nini?”
“Kwenye maelezo yangu baada ya yeye kuhitaji taarifa za vifo vya wana familia wake kuna sehemu ambayo niliruka kuhusu sms zako na wala sikuhitaji kabisa kumhusisha kwa chochote kile alinikalia kimya tu mpaka nilipo mpeleka hospitali ya mhimbili Kwenda kuiona hiyo miili ya ndugu zake ndipo alipoweza kuniuliza hicho kitu nimeshtuka sana”
“Ameniuliza kwanini namdanganya kuhusu sms ambazo nilizikuta mle ndani, sijui amejuaje kama kuna sms mule nimezifuta ambazo ni zako lakini pia ameniuliza kwanini tumeruhusu mtu ambaye hahusiki kabisa na mauaji akauawa mbele ya mahakama maana yake ni kwamba tulitengeneza mtego ndugu yake afe”
“Umeniacha kidogo hapo ebu fafanua kiundani kidogo” CDF aliuliza kwa wasiwasi baada ya kuona kuna sehemu kama hajaelewa vizuri
“Ndugu zake wote wamekufa huku wakiwa wamepigwa risasi za kichwa kwenye paji la uso na hata raisi ilikuwa ni hivyo hivyo, kama raisi aliuawa na mtu ambaye wewe ulisema mlimkamata na akanyongwa mbele ya mahakama maana yake kama angekuwepo muuaji mwingine basi aina ya mauaji ingekuwa ni tofauti lakini cha ajabu hata ndugu zake wameuliwa vile vile tu kama raisi hapo inaonekana kabisa kwamba muuaji alikuwa ni mtu mmoja. Swali lake kwamba kama ni mtu mmoja ndiye anahusika maana yake ni kwamba aliye nyongwa mahakamani siyo mhusika ila mhusika yupo sasa kwanini tulimhukumu mtu ambaye siye mhusika? Ndugu yangu niwe muwazi tu hilo swali na uzee wangu huu limenishinda kabisa kulijibu hivyo alilazimika kuniuliza mtu aliye toa amri ya mtu huyo kukamatwa ikabidi nikutaje wewe kama ulivyokuwa umeamuru”
“Enhe kama ni hivyo kwahiyo yeye anataka iweje?”
“Anahitaji sana akutane nawewe ili wewe uje umjibu hayo maswali mwenyewe maana kuna vitu ambavyo kwa mimi vilikuwa nje ya uwezo wangu kwa sababu sivijui nadhani wewe una maelezo mengi zaidi, kuna makosa mengi sana ya wazi ambayo yamefanyika kwenye hii kesi naona kabisa huko mbeleni yanaenda kuleta matatizo makubwa sana”
“Huyo mtoto anajiona nani kwani mpaka aanze kutupelekesha namna hii kama ametuajiri yeye, inatakiwa asubiri mpaka pale nitakapo pata nafasi yangu ndipo naweza kumtafuta tukae naye”
“Amesema anataka leo na anakuja saa sita kamili usiku utamkuta nje ya geti lako na amesisitiza sana mkutane kwa sababu kama ukizidisha hata dakika moja humkuti huwa ni mtu wa kwenda na muda sana”
“Hivi ndiye huyu mtoto mdogo wake na Mark ambaye ndiye anatoa hizo amri au ni nani?”
“Ndiye huyo huyo”
“Kivipi yaani mpaka mtu na utu uzima wako unatii kila kitu kwa huyo mtoto”
“Ni mtoto sio?”
“Yes, wewe huoni kama ni mtoto mdogo yule hata kama kafiwa hata sisi yule ni rafiki yetu inatakiwa awe mpole asitupelekeshe”
“Sawa ni kwa sababu tu humjui ndiyo maana una hiyo jeuri ya kuongea hivyo ila nakusihi sana jitahidi sana msije kuingia kwenye mgogoro wowote ni vyema ukamsikiliza”
“Kamwambie nitamsikiliza pale nitakapo muita mimi”
“Hayo maneno utamwambia mwenyewe akija hapa kwako kwa mdomo wako”
“Huyo kijana kuna nini kwani upande wake mpaka unahaha hivyo IGP mzima kabisa”
“Ipo siku utakuja kumjua na ndipo utakuja kuyakumbuka maneno yangu, mimi naenda itakapo hitajika tutakutana tena”
Huyu Jason ni nani hasa mpaka IGP anaonekana anamuogopa sana mtoto laini kama yule?
Marafiki wawili hawa mazungumzo yao yaliishia sehemu mbaya kidogo ya kutokuwa na maelewano mazuri hata kidogo japo walianza vizuri hiyo ni kawaida kwenye maisha ya mwanadamu yeyote hakuna mtu ambaye atakuwa upande wake milele ukitoa wazazi wake hata ndugu wanaweza kutokomea na kuzipambania familia zao, ila wazazi usije ukawasahau kamwe hata kama walikukosea vipi as the saying goes Go EAST, GO WEST, HOME IS ALWAYS THE BEST.
Wasalaaam
Bux the storyteller.
Brother nina uhakika 100% bado haunifahamu ama umesoma hadithi moja tu pekee kutoka kwangu.Tahadhali Kwa ambao hampendi alosto huyu hua hamaliza ko tusome ikifika mda akasema inaisha hapo msimtukane
Mkuu Hawa hawakujui mzigo lazima uishe sisi ni mashahidiBrother nina uhakika 100% bado haunifahamu ama umesoma hadithi moja tu pekee kutoka kwangu.
Kusema huwa simalizi nadhani umenikosea pakubwa sana unless kama unafanya jokes.
Nimeleta simulizi 4 hapa jf na hii ni ya 5.
1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA (Niliileta hapa mpaka mwisho)
2. NATAKA KUFA HAKIMU (niliileta mpaka mwisho)
3. HATIMA YA UJINGA WAKE (niliileta mpaka mwisho)
4. GEREZA LA HAZWA (Hii ndo haikuisha nadhani iliishia 96. Nikaja kuomba execuse hapa kwamba kuna watu wanahitaji niwatolee kitabu (nakala ngumu). So nikaomba tusiendelee kuisoma humu maana itakuwa haina maana mtu kaimaliza huku halafu tena anunue kitabu. Nakumbuka watu walikuja kudhihaki sana, sikumbuki kama ulikuwa mmoja wao
Wengine wakadai kama nataka kufanya biashara niende kwenye threads za biashara (sikumjibu mtu), wengine wakadai kwamba kama vipi modes waitoe tu na kweli ikatolewa) japo kuna watu walinielewa pia na baadae nilikuja kuamua kutaka kuiendeleza ila ikawa imetolewa.
5. INNOCENT KILLER (ndo hii tunaisoma hapa)
Hivi mkuu nikikwambia uthibitishe kauli yako kwa hayo maelezo ya hapo juu unaweza?
Nadhani ni wakati sahihi watu kujifunza COMMUNICATION SKILLS na kuachana na kutu kinaitwa MANIPULATION mkuu. Hapo mtu ambaye atakuwa anaanza kusoma kwa mara ya kwanza anaweza kuhisi kwamba ni kweli nipo hivyo kitu ambacho siyo sahihi.
NB
Hii nilisema nitakuwa naipost mara mbili kwa wiki kwa sababu mpaka sasa bado naiandika japo imefika mbali kidogo (sehemu ya 90). Nilifanya hivyo sikutaka tusome halafu tuje kustop njiani lakini huwa naileta zaidi ya mara mbili kwa wiki mpaka mara 4 na itakuwa zaidi muda unavyo zidi kwenda.
TUJIFUNZE KUZUIA HISIA MKUU JAPO NAKUELEWA maana hata mimi nimewahi kuwa msomaji kabla ya kuwa mwandishi.
Amani itawale japo nina imani huenda haukuongea kwa nia mbaya ila watu wengine wanaweza kuichukulia kwa namna tofauti, nadhani kikubwa ni kueleweshana tu, bado najifunza.
Baadae kidogo naweka mwendelezo hapa [emoji120]
Unatakiwa Umsaport mwamba sio unasoma tu, jiongeze siku moja mojaTahadhali Kwa ambao hampendi alosto huyu hua hamaliza ko tusome ikifika mda akasema inaisha hapo msimtukane
Please PM me if you won't mind.