Innocent Killer (The Revenge)

Innocent Killer (The Revenge)

Stori: Innocent Killer (The Revenge)
Msimuliaji: Bux the story teller
Umri: 18+
Sehemu ya Tano:

Songa nayo.............

Akiwa amepigwa na butwaa mbele ya mwili wa mwanae wa kwanza ndipo alipo shtuka kutoka kwenye huo mfadhaiko baada ya kumkumbuka mkewe ambaye alikuwa ni mjamzito na siku sio nyingi angefanikiwa kumletea mtoto wa kiume hapo ndani kwake na ni kitu ambacho alikuwa anakisubiria kwa hamu kubwa sana, alikurupuka kama hana akili timamu na kuanza kukimbia kuelekea sehemu ambayo ilikuwa na ngazi za kupandishia juu na huko ndiko ambako alihisi mkewe atakuwepo kwenye chumba chao cha kulala.

Alisita sana baada ya kufika kwenye mlango huo wa kuingilia chumbani lakini hakuwa na namna ilibidi ajikaze kiume huku akiwa anafuta machozi na jasho jingi ambalo lilikuwa likimtoka kwenye mwili wake na kufanya kuwa kama maji hususani kwenye eneo lake la uso, mlango uliegeshwa tu hivyo akausukuma kidogo huku akiwa anahema kwa nguvu sana, alitulia kama dakika nzima akiwa hajafanya mjongeo wowote wala kutamka neno lolote zaidi ya kutetemeka tu baada ya kumuona mkewe, mkewe alikuwa akihema kwa nguvu sana akiwa amemnyooshea mkono mmewe kumhitaji pale alipokuwepo yeye, alianza kuogopa sana mheshimiwa jaji mkuu baada ya kuona kuna binadamu ambaye hakuwa na uhakika sana kama naye aliwahi kuzaliwa na mwanamke kwa kitendo ambacho alikuwa amemfanyia mkewe.

Kisu chenye ncha kali mno kilizamishwa kwenye tumbo la mwanamke huyo na binadamu ambaye yeye hakumuona mpaka wakati huo, na huyo mkewe alikuwa amembebea mtoto wa kiume humo tumboni ambaye walikuwa wakimsubiria kwa hamu kubwa sana, machozi yalikuwa yanamshuka mwanaume taratibu huku akianza kutembea kwa kujivuta kuelekea pale alipokuwepo mkewe, wakati anazidi kusogea kuna ishara mkewe alikuwa akimpatia kwa sababu hakuwa na uwezo wa kutoa sauti kutokana na damu iliyokuwa imemtoka kwa wingi na nyingine ilikuwa ikiendelea kutoka mdomoni, mwanaume hakuelewa chochote alienda pale chini ya kitanda na kumuweka mkewe kwenye mapaja yake.

“Nisamehe nisamehe mama, nisamehe sana mimi nimekuulia wanao wote wawili lakini nimekuletea matatizo hata wewe pia nisamehe sana” aliongea kwa uchungu sana aakiwa amemkumbatia mwanamke huyo, mkewe alitabasamu kwa mbali sana kwa sababu tabasamu lake lilikuwa na maumivu makali sana ndani yake, alijitahidi sana kutaka kumpa ishara mumewe huyo kipenzi ambaye alijijua wazi kwamba yeye ndiye alikuwa dawa pekee ya mwanaume huyo, lengo lake alikuwa anahitaji kumpatia taarifa kwamba nyuma ya huo mlango kulikuwa na mtu lakini jaji mkuu hata hakushtuka kuhusu hilo.

Aliitoa simu yake na kuingia upande wa live video, aliipiga simu Kwenda nje ya nchi akiwa anatokwa na machozi kwenye macho yake, simu ilipokelewa na kwa upande wa pili ilionekna sura ya kijana mmoja ambaye alikuwa na sura kama shombe shombe ila ilikomaa kiasi chake na kumfanya kuwa mwanaume kweli, huyo alikuwa ni mdogo wake wa damu kabisa walizaliwa tumbo moja na walikuwa wawilitu. Mdogo wake alishangaa sana kumuona kaka yake akiwa kwenye hiyo hali ya majonzi ni kitu ambacho hata yeye mwenyewe kilimtia shaka.

“They have killed us, they have killed us” aliongea kwa uchungu akiwa anapangusa machozi akiigeuza simu kuelekea upande ambao alikuwa amemkumbatia mkewe, mwanaume upande wa pili hakuongea kitu baada ya kumuona kaka yake kwenye hiyo hali alimuangalia shemeji yake kwa uchungu sana baada ya kuona kitu ambacho alikuwa amefanyiwa, alitabasamu kama kumpa tumaini la maisha shemeji yake kwa sababu kupigiwa simu ina maana yeye ni mtu aliyekuwa amekusudiwa kuwafariji kwa huo wakati na haikutakiwa aonyeshe udhaifu. Alikuwa na mengi sana ya kuuliza kwa sababu kwanza hakujua kipi kinaendelea na nini kilikuwa kimetokea mpaka wakati huo aliamua kuupa muda nafasi huenda kaka yake angemwambia ukweli, akiwa anaendelea kumuangalia kwa uchungu shemeji yake ambaye macho yake yalikuwa yameanza kufifia sana alitamka neno moja tu.

“Mama nakupenda sana” Huyo mwanamke wote walikuwa wakimuita hivyo mama kwa sababu jinsi alivyokuwa akiishi nao alichukua moja kwa moja nafasi ya mama yao mzazi ndiyo maana walimheshimu na kumpenda kiuliko kitu chochote kile kwenye maisha yao, mwanamke huyo alitaka kama kutabasamu lakini alishindwa taratibu akawa anayefumba macho yake, hilo tukio halikukamilika moja kwa moja kwa sababu mwanaume alianza kuona chenga chenga ghafla sana baada ya kusikia kishindo kikubwa na sauti kali ya maumivu ikilia upande wa pili

“Hey brother, brother talk to me please” alibaki anaita bila mafanikio yoyote yale, baada ya sekunde kama thelathini alisikia kwa mbali sauti yenye maumivu na isiyokuwa na matumaini kabisa ikisema

“They have killed your brother, they have killed your brother” ilififia baada ya kusikia mlio wa risasi na simu hiyo ikakatwa, alijaribu sana kuipiga tena simu hiyo lakini haikupatikana tena, aliishiwa nguvu mwanaume hakujua nyumbani ni tatizo gani la ghafla lilikuwa limetokea mpaka wakati huo kwa sababu kwa mara ya mwisho aliona kuhusu ile kesi iliyokuwa inaendeshwa na aliona kama kaka yake kama jaji mkuu alikuwa amefanya maamuzi ya maana sana kuweza kumuua mtu ambaye alikuwa moja kwa moja amehusika na mauaji ya mheshimiwa raisi na haikujulikana ni kwa sababu zipi yeye hakuweza kabisa kupiga simu nyumbani mapema sana kiasi hicho.

Nyumbani kwa jaji mkuu wakati anaongea na ile simu mwanaume aliyekuwa nyuma ya mlango alikuwa akimwangalia kwa umakini sana na hakutaka kukurupuka ili kama mtu huyo alikuja na watu au ulinzi basi iwe ni rahisi kukabiliana nao ndio maana hakuhitaji kukurupuka kumfuata hapo chini, baada ya kujihakikishia kwamba hilo eneo lilikuwa salama kwa upande wake yeye basi alimsogelea mwanaume huyo wakati akiendelea kuongea na simu alipigwa buti moja kali sana la kichwa na ndio ule muda ambao simu ilimponyoka na kuanza kuonyesha chenga chenga.

“Uliambiwa ukajifanya mjanja kuendelea kuyafanya yale ambayo wewe hukupaswa kuyafanya sasa utawapa somo na wenzako ambao utawakuta mbele huko” ni sauti moja kavu sana kutoka kwa mwanaume ambaye yeye mwenyewe baada ya kumuangalia alikuwa akimfahamu mtu huyo ila hakupewa nafasi ya kuendelea kuishi alitamka tu kwa nguvu

“They have killed your brother” akiamini kwamba mtu wa upande wa pili wa hiyo simu alikuwa akimsikia vizuri wakati akiwa anaongea na ndio huo muda ambao ulisikika mlio wa risasi na simu hiyo ikakanywangwa na mwanaume huyo ukimya ukawa umepita.

Hiyo ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Jason pamoja na watanzania wote ambao walishtushwa sana na taarifa za kifo cha ghafla sana cha mheshimiwa jaji mkuu wa nchi ya Tanzania Markvelous Japhary ikiwa ni muda mchache tu tangu aweze kutoka kumsomea hukumu mwanaume ambaye alisadikika kuwa alikuwa amemuua mheshimiwa raisi wa nchi ya Tanzania. Hata mwili wa mheshimiwa raisi ulikuwa bado haujapumzishwa lakini naye jaji mkuu alikuwa tayari amekufa na kibaya yeye alikufa na familia yake yote mtoto wake wa kike pamoja na mkewe mjamzito, zilitolewa taarifa chache sana kwamba kwenye hiyo familia alikuwa amebakia mtu mmoja tu ambaye ni mdogo wake na mheshimiwa jaji mkuu ambapo serikali iliahidi sana kumpatia ushirikiano mkubwa kijana huyo ikiwa ni pamoja na kumsaidia pale ambapo angehitaji msaada wowote ule kutokana na heshima kubwa pamoja na mambo makubwa ambayo kaka yake alikuwa ameifanyia nchi hii kwa kipindi chake ambacho yeye alikuwa yupo hai.

Polisi wa kutosha walikuwa ndani ya eneo la tukio wakiwa wanaendelea na uchunguzi wao ili kujua ni nani ambaye alikuwa amehusika na hilo tukio la mauaji ya mheshimiwa jaji mkuu,walichukua kila kiambatanisho cha ushahidi wote ambao ulipatikana kwenye hilo eneo ikiwepo simu na risasi ambazo zilitumika kuwaua watu hao kisha wakaibeba miili na kuelekea nayo mochwari ambako walikusudia kwenye kuifanyia uchunguzi zaidi.

“Haya matukio naona moja kwa moja yana uhusiano mkubwa sana kwa sababu mheshimiwa raisi amekufa ndani ya muda mfupi tu halafu baada ya mheshimiwa jaji mkuu kutoa hukumu kwa yule mtu naye amekufa leo leo tena kwa muda mfupi sana baada tu ya kumaliza ile kesi, nina uhakika haya matukio yalipangwa kwa muda mrefu na hayatokei kwa bahati mbaya na huenda wahusika ni wale wale hivyo hili jambo kwa mtu ambaye nimeapa kulitumikia vyema vazi langu la jeshi la polisi nitahakikisha nakula sahani moja na hawa wote walio husika na watakamatwa tu hii kesi naenda kuisimamia mwenyewe” Aliongea kwa msisitizo sana Afisa wa polisi (Asp) Bakari Zalimo akiwa anatoa maelezo kwa wenzake baada ya muda mchache aliokuwa amekaa hapo kuweza kung’amua baadhi ya mambo.

“Ndugu yangu huo uhodari wako ambao huwa unautafuta kuna siku utakuja kukuponza sana, huwa unafanya vitu bila hata kujiwazia kwamba kuna maisha baada ya hivyo vitu, hivi wewe unadhani mtu mkubwa kama huyu anaweza kuuawa kiwepesi tu kama unavyo hisi wewe? ni mtu gani wa kawaida ambaye anaweza kumuua mheshimiwa kama huyu huenda hao wanao tutuma hizi kazi ndiyo wahusika wenyewe kwa sababu sioni wakuu wakitilia mkazo sana katika hilo kwahiyo nadhani sisi tujiweke kando tu” Afisa mwenzake ambaye alijulikana kama UTAPEWA aliongea kumtahadharisha mwenzake huyo ambaye alionekana kuhitaji kulivalia njuga hilo suala ambalo lilikuwa na uzito kwa upande wake yeye.

“Haina maana yoyote ya kuvaa hilo vazi lako ambalo lipo kwenye mwili wako na hauna hata uwezo wa kulilinda, unajua tafsiri sahihi ya hilo vazi? Unakumbuka siku unaapa mbele ya bendera ya nchi yako na kauli uliyo itoa kuhusiana na hilo vazi? Basi kama unakumbuka unatakiwa kuliweka hilo kichwani mwako hiyo kofia ina maana kubwa sana kwenye maisha ya jeshi la polisi, hiyo ni alama ya mtu ambaye anapaswa kuipigania hiyo kofia mpaka pumzi yake ya mwisho, wananchi wanapo iona hiyo kofia na hilo vazi basi huwa wanajaa matumaini na kujihakikishia kwamba wapo kwenye eneo salama kabisa na hiyo ndiyo sababu hata leo hii ukimuona mwananchi amepata tatizo ambalo litahatarisha usalama wa maisha yake yeye, kitu cha kwanza lazima atapiga simu polisi ambako ana uhakika kwamba kuna usalama wa maisha yake”

“Sasa kama wewe hapo unavaa vazi ili kujifurahisha na kulitumia kama kivuli cha kujilinda na kuyaficha mambo yako ya hovyo pamoja na kujichumia mali ambazo zinatokana na kodi za wananchi kwa jasho lao wenyewe una utofauti gani na mtoto wa kike ambaye anaikataa mimba huku akiwa anatamani kuitwa mama? Kama unahisi hauiwezi hii kazi ungesomea hata ualimu ili ukawadanganye watoto kuhusu uzalendo ambao hata wewe mwenyewe hauna. Unatakiwa kujionea aibu mwanaume kama wewe kutanguliza uoga wa namna hiyo mbele ya haki ya mtu mwingine, sina uhakika kama ungekuta mama yako, baba yako, kaka yako, dada yako au ndugu yako wa karibu kafanyiwa hivi halafu ukawa na nguvu za kutamka huo utumbo wako, kumbuka ana mdogo wake ambaye inadaiwa muda wowote ule anaingia nchini lazima atahitaji ripoti juu ya kifo cha familia yake utamjibu nini wewe hapo zaidi ya kuishia kuingiza mikono mfukoni kama mgane ambaye amekataliwa na kila mwanmke kutokana na majivuno yake, siku nyingine usije ukaongea utumbo kama huo mbele yangu maana nitakupiga risasi, kawaambie na hao wenzio kesho asubuhi sana naingia kuanza uchunguzi wangu na ole wake nikukute hata wewe umo kwenye hilo kundi” Afisa wa polisi alichukizwa sana na kauli ya mwenzake UTAPEWA alitegemea mtu huyo na wenzake wangejadili namna sahihi ya kuweza kulifanyia kazi hilo jambo cha ajabu yeye alikuwa anamshauri jinsi ya kujiweka mbali na hilo jambo alimuona kabisa hafai kuwa kwenye hilo vazi ambalo yeye alikuwa analiona kama lina thamani kubwa sana.

Aliondoka kwa hasira sana baada ya kumwambia mwenzake ukweli wa kila ambacho alikona kilikuwa sahihi kwa upande wake, aliahidi kwamba kutakapokucha tu angeamkia Kwenda kuianza hiyo kazi ambayo kwake ilikuwa ni ya lazima kuifanya na haukuwa msaada bali alikuwa ana uhakika kwamba huo ulikuwa ni wajibu wake ndio maana alikuwa akilipwa.

Bado ni mapema sana, ndio kwanza tunaanza, leo tuishie hapa.

Wasalaam

Bux the storyteller.
FB_IMG_1680324048558.jpg
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 6

SONGA NAYO............

HAVARD UNIVERSITY,

Ndicho chuo namba moja kwa ubora zaidi duniani kikiwa kinapatikana ndani ya nchi ya Marekani ama waweza kuiita United States of America kama wale ambao lugha za wenzetu zinapanda vizuri ndivyo huwa wanakiita hivyo wakiwa na maana ya muunganiko wa majimbo mbali mbali ambayo yapo takribani 52 ndiyo kwa pamoja yanaiunda nchi hiyo.

Ndani ya hicho chuo ndiko ambako simu iliyokuwa imepigwa na jaji mkuu wa nchi ya Tanzania kuelekea kwa mdogo wake ilimkutia mtu huyo, yalikuwa majira ya jioni au waweza kusema usiku wa mapema wakati kwa huku Tanzania ilikuwa inaelekea mchana wa saa 7 ndio muda ambao Jason alipipigiwa simu na kaka yake.

Wakati simu inapigwa yeye alikuwa kwenye bustani moja nzuri sana ndani ya viunga vya chuo hicho ambacho ndicho alikuwa anasoma, alipokuwa hapo bustanini alikuwa karibu na ua moja zuri sana wakiwa kwenye furaha kubwa mno.

“Hivi Jason ni kitu gani huwa unakikumbuka sana mimi ninapokuwa karibu nawewe?” sauti moja maridhawa ambayo ilipewa kibali cha kupenya kwenye kila sikio la mwanaume rijali ilikuwa ikisikika kwenye masikio ya mwanaume huku mwanamke huyo akiwa amejilaza kwenye ,mapaja ya mwanaume ambaye kwake alikuwa ni nusu ya maisha yake, mwanaume huyo alikuwa amekishika kitabu kimoja kinaitwaa BLACK AMERICAN REFUGEE akiwa anamsimulia mwanamke huyo harakati za mmarekani mweusi kuweza kuukimbia ubaguzi wa rangi ulio kithiri kutoka kwa mabeberu na kuweza kujitafutia sehemu ambayo angekuwa salama kama sio kuweza kuipigania haki yake mwenyewe dhidi ya huo unyonyaji na mateso yaliyokuwa yamekithiri.

Monalisa ndilo lilikuwa jina lake mwanamke huyu, huyu ndiye ambaye alikuwa ni ubavu wa Jason akiwa huko Marekani, walipendana sana ilifikia hatua watu karibia wote ambao walikuwa wakiwazunguka walijua kwamba watu hao ni kama pipa na mfuniko, kama pwagu na pwaguzi lakini walitoa tafsiri sahihi ya mapenzi ya kweli kama kwa Romeo na Juliet au yale ya Bonnie na Clyde.

Swali hilo lilimfanya mwanaume huyo akifunike kitabu kwanza akanyanyuka huku akiwa anatabasamu sana usoni kwake,penzi lilimtembelea alikuwa na nuru ya kutosha mbele ya nyusi zake na kumfanya kuzichezesha atakavyo yeye wa kumfuta jasho alikuwa karibu yake, aliguna kidogo kisha akamwangalia mrembo huyo kwa mujibu, aligeuza macho na kuziangalia bustani hizo ambazo zilikuwa zinavutia sana kwa kupambwa na taa safi ambazo zilikuwa zimezungushiwa hayo maeneo, baada ya kuzungusha macho yake aliyarudisha tena kwa mwanamke huyo, alicheka baada ya kuona mwanamke huyo amemkazia sana macho ni wazi alikuwa anatamani sana kuweza kusikia majibu ambayo alikuwa amemuuliza mtu huyo kwa namna alivyokuwa amemkazia macho.

“Mapenzi ni nadharia ya kufikirika japo sio kama TEHAMA maana tehama unaweza kuifanyia tafiti na ukaja na gunduzi mbali mbali ambazo zitauthibitisha ukweli ila mapenzi ni kama zile nomino za kuzifikiria huwezi ukazigusa, kuziona, kuzishika, kuziuliza wala kuzisikia ila tu utazihisi kwenye moyo wako. Mapenzi nimekuja kukataa kwamba sio kama zile nomino dhahania baada ya kukutana na wewe”

“Siwezi kuisahau ile siku ambayo mimi nilikuwa mgeni ndani ya hiki chuo siku ile ya kwanza kabisa ukiwa umetoka kwenye matembezi yako ya kimasomo kama ulivyoweza kusema ndipo nilipokutana na moja ya sura nzuri zaidi kuwahi kuziona kwenye maisha yangu na nikaamua kuichagua sura hiyo kuwa moja ya sehemu ya maisha yangu milele mpaka pale ambapo nitaikata pumzi yangu ya mwisho ya kuitwa mwanadamu ambaye yupo hai” mwanaume alipumzika kidogo na kumwangalia tena mwanamke huyo kisha akaendelea

“Ile ilikuwa ni zaidi ya stori nzuri ya kwenye ajali ya TITANIC kwenye ule mfano bora wa mapenzi ambao unaishi kwenye mioyo ya watu wa Jack na Rose lakini kwetu imekuwa tofauti sana ndio maana hata mimi leo ukiniuliza kipi ningependa kukiona kwenye maisha yangu kabla sijatoweka hapa duniani ni kipi? Basi nitakwambia mimi natamani nife mapema sana kabla yako wewe, hii haimaanishi kwamba mimi sikupendi wala nataka nikuache pekeyako ukiwa unateseka duniani hapana mimi nakupenda sana na nadhani unaelewa kwamba moyo wangu umegeuka kuwa uwaridi unukiao kwa sababu ya huba lako lakini ningetamani kufa mapema kabla yako kwa sababu nahisi kwamba siwezi kukushuhudia wewe ukifa kabla yangu maana nina uhakika maumivu yake siwezi kabisa kuyabeba kwenye moyo wa……….” Mwanaume akiwa anampatia Samaki wake chambo ambayo ilikuwa inamfanya azidi kunasa kwenye ndoano zake, moja ya maneno matamu sana ambayo wanawake wengi huwa wanatamani sana kuyapata kutoka kwa wale watu ambao wamewakabidhi maisha yao ya mapenzi na kuwaruhusu wawamiliki watakavyo wao, maneno ambayo yalimfanya Monalisa waweza kumuita Lisa abaki anacheka cheka huku akiwa anatabasamu sana wakati mwanaume akiwa anajaribu kumuelezea mwanamke huyo anacho kikumbuka kwenye mapenzi yao pale wanapokuwa karibu, ndio muda ambao Jason alishtushwa na mlio wa simu yake.

Simu yake muda wote ilikuwa inakuwa on kwa sababu alizoea hivyo ili hata pale ndugu yake au shemeji yake anapokuwa anampigia aweze kumpata kiwepesi zaidi, aliitoa simu yake alitabasamu baada ya kuona jina la kaka yake basi aliipokea kwa bashasha akiwa anamuangalia kaka yake lakini alishtuka baada ya kumuona kaka yake akiwa kwenye hali ya majonzi kama hiyo ndipo aliposikia kila kilichokuwa kinaendelea mpaka wakati ule anasikia milio ya risasi na simu kukatika kisha kuacha kabisa kupatikana, sana sana aliyazingatia sana maneno ya mwisho ya kaka yake “ They have killed us, they have killed your brother” haya maneno yalimchanganya na kumfanya achanganyikiwe, ile hali ambayo alimuona nayo shemeji yake pale moyo wake ulikuwa unamuenda mbio na kasi kubwa sana, alikuwa anatabasamu mbele ya shemeji yake ila moyoni mwake alikuwa anatoa machozi ambayo asingeweza kabisa kuyafuta kwa mkono au kitambaa cha kawaida.

Baada ya simu kukatika alibaki akiongea mwenyewe “Brother talk to me please” ilikuwa kimya hakupata mrejesho wowote ule mpaka pale ambapo alikuja kugundua kwamba simu hiyo ilikuwa imekatika hewani kwa muda mrefu sana.

“Noooooooooooooo” alipiga kelele akiwa anarudia mara mbili mbili kuipiga simu hiyo lakini hakuna kitu angeweza kufanya hapo, hiyo kelele, mshtuko wake, namna alivyokuwa anahema na jasho kali ambalo lilikuwa linamtoka licha ya baridi ambayo ilikuwepo ndivyo vilimfanya mwanamke wake Monalisa kumsogelea na kumuuliza.

“Babe are you alright” mwanaume huyo hakumjibu kitu zaidi ya kumuangalia mwanamke huyo huku macho yake yakiwa mekundu sana, Monalisa aligundua kwamba moja kwa moja hapakuwa na usalama huko alimfuata na kumkumbatia mwanaume akiwa anampiga piga mgongoni. Zilipita dakika kumi ndipo mwanaume alipokaa na mrembo huyo kumwelezea kile ambacho alikuwa amekishuhudia kwenye simu yake.

“Usijali nyumbani hakuna kitu kibaya ambacho kimetokea kila kitu kitakuwa vizuri tuwaombee tu huko waliko wawe salama nina imani ndugu zako watakuwa salama” mwanamke huyo hakuwa na taarifa nyingi sana za Jason ndiyo maana mpaka muda huo hakuwa akijua kama Jason ni mdogo wa jaji mkuu wa nchi ya Tanzania hivyo alimpa moyo mwanaume wake ili angalau awe sawa ila mwanaume alisikitika tu kwa sababu mwanamke huyo alikuwa anampa moyo kwenye kitu ambacho yeye alijua hakipo kama Monalisa alivyokuwa akifikiria yeye.

“Nadhani tutaonana kwa wakati mwingine tena?” Jason aliongea kama masiara akiwa anasimama

“Whaaaaaaat?”

“Im leaving”

“Where are you going?”
“Home”
“You mean Tanzania?”
“Yes”
“No Jason naomba usubiri kwanza mpenzi wangu ili tuweze kufanya mawasiliano tujue kama kuna tatizo kubwa ambalo linaweza kukufanya mpaka urudi kwa sababu mi mwenyewe nitarudi huko likizo baba ameniambia niende” Jason alimwangalia sana binti huyo

“Hakuna unacho kijua kuhusu hili it’s me and my family hauwezi ukanielewa kwa sasa ila nikwambie tu naomba niende kama MUNGU atapenda tunaweza kuja kuonana tena kama sio kwenye maisha haya basi kwenye maisha ya wakati mwingine” bibie alitoa kicheko sio kwamba alipenda Hapana ila alikuwa haamini kwa namna mambo yalivyokuwa yanaenda kwa kasi, alihisi alikuwa kwenye ukumbi wa tamthiliya akiwa anaangalia filamu moja ya kusisimua na ikiisha angejikuta yupo pale pale na kutoka kwenye hisia, kwa hapo alichokuwa anakiona kilikuwa ndicho kinacho tokea hakukuwa na cha movie wala nini

“Jason, are you serious? Unarudi nyumbani muda huu unapata ndege gani ambayo ina nafasi, unaniachaje mimi? Na masomo inakuwaje? Unatakiwa ukumbuka nafasi za hiki chuo huwa zinapatikana kwa nadra sana unataka kuipoteza kirahisi sana namna hiyo na vipi kuhusu mapenzi yangu mimi unahisi nitaishije bila wewe? nitaishi maisha gani mimi? Aaaaah” aliongea kwa uchungu sana Monalisa kwa sababu ilikuwa ni ghafla sana na ndivyo huwa inakuwa hivyo kwenye mapenzi mara nyingi mwanamke huwa anaangalia upande wake tu bila kujali unayo yapitia au matatizo uliyo nayo kwake furaha yake huwa ndiyo kila kitu hata kama wewe unavuja damu kwenye moyo wako, mwanaume hakuongea chochote kwa sababu alijua hapo watabishana mpaka asubuhi.

Hakujibu kitu akaondoka akiwa anakimbia kwa spidi sana, mwanamke huyo alianza kumfuata kwa nyuma, spidi za Jason zilienda kuishia kwenye ofisi moja kubwa sana ndani ya chuo hicho, alipandisha mpaka ghorofa ya tatu kisha akatoa kadi yake mfukoni na kuipitisha kwenye moja ya milango mizito sana ambao kwa juu ulikuwa na jina la Professor Michael, hiyo ilikuwa ni ofisi ya moja kati ya maprofessor wakubwa sana ndani ya chuo hicho haikueleweka aliingia kutafuta nini na kwanini alikuwa na uwezo wa kuingia hiyo sehemu, Monalisa alikuwa anakuja kwa mbali alimuona mwanaume wake huyo akiingia kwenye ofisi hiyo alishangaa sana ila bahati mbaya sana baada ya kufika hapo mlango ulijifunga akawa amekaa nje kusubiri. Alisubiri nusu saa, saa liliisha, la pili, likaisha saa la tatu kulikuwa kimya hakukuonyesha hata dalili kwamba ndani humo kulikuwa na mtu basi ilimlazimu kutoa simu yake mfukoni na kuanza kupiga namba ya Jason ila aliambiwa kwamba haikuwa ikipatikana namba hiyo, hicho kitu kilimshangaza mno.

Alisubiri saa lingine mpaka yakawa yameisha masaa manne kukiwa bado kimya basi aliondoka hapo kinyonge sana akaelekea sehemu ambapo alikuwa amepaki gari yake, aliingia ndani ya gari hiyo akawa ametulia hapo ikionekana kuna kitu anasubiri. Baada ya masaa mawili kupita alimuona mwanaume mmoja mwenye upara akiwa anakuja ile sehemu akiwa ana begi lake mkononi, sura moja ya kiafrika ambayo uso ulitakata kwa pesa ambayo haikuonekana kuwa shida kwake ilikuwa ndani ya miwani, huyo ndiye alikuwa professor Michael mwenyewe, Monalisa wakati anaondoka aliiona gari ya professor huyo ndiyo maana aliamua kusubiri hapo ili amhoji mtu huyo kama alikuwa anajuana na Jason na kwa muda huo alikuwa wapi?

Alishuka kwenye gari na kumkimbilia mheshimiwa huyo ambaye kwa wakati huo alikuwa amefungua mlango wa gari yake akitaka kuingia.

“Professor” mheshimiwa huyo aligeuka
“Nikusaidie nini?”
“Samahani mimi ni moja ya wanafunzi wako”
“Sawa nina wanafunzi wengi sana hivyo siwezi kuwakariri sura wote waweza kunieleza shida yako?”
“Nataka kujua mpenzi wangu yuko wapi?”

“Yupi huyo?”
“Kuna mwanaume mmoja ambaye ameingia kwenye ofisi yako mle japo sijui ameingiaje na hajatoka tena kwahiyo nahitaji kujua ameelekea wapi?"

"Wewe ni nani?”
“Mpenzi wake” Professor huyo aliitoa simu yake na kuingia kwenye picha, aliangalia picha ambayo alikuwa anaonekana Jason na mwanamke mmoja ambaye baada ya kumwangalia vizuri alijiridhisha kwamba kweli alikuwa ni huyo, aliirudisha tena mfukoni.

“Nadhani kwa sasa yupo angani anaelekea kwao?”
“How?” Monalisha alishangaa sana
“Umeniuliza swali nimekujibu hata hivi nina haraka sana sihitaji maswali mengi nimechoka” baada ya kuongea maneno hayo mzee huyo aliingia kwenye gari kisha akatoweka, Monalisa alichoka mpaka akakaa chini, hakuelewa kimefanyika nini mtu ameingia kwenye ofisi ya professor halafu anaaambiwa kwamba yupo angani maana yake kwenye ndege sasa kafikaje?

Hilo swali hata mimi sina jibu lake kwa leo, sijui huyu professor ni nani hasa na Jason ni kweli yupo kwenye mchuma akiwa anaelekea bongo land? Twende sawa huenda tukapata majibu sahihi.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 7

SONGA NAYO............

Mida ya Asubuhi na mapema Jason alionekana ndani ya uwanja mkubwa sana wa ndege ndani ya nchi ya Kenya KENYATTA AIRPORT, hakukaa sana aliingia kwenye ndege ambayo ilikuwa inaelekea ndani ya taifa pendwa zaidi Afrika Tanzania amani imetawala sana ndani ya nchi hiyo, mwanaume alipanda kwenye ndege hiyo maana hakukaa sana hapo ilionyesha wazi kwamba kila kitu kilikuwa kimeandaliwa tayari kwa ajili yake na ilionekana kama kulikuwa na taarifa za ujio wake tayari. Haikuchukua muda sana ndege ikawa inatua mabawa yake ndani ya KIA (Kilimanjaro International Airport). Napo hakukaa sana kuna mwanaume mmoja alikuja kumpokea hapo hakuongea naye chochote zaidi kumpa heshima kisha aliongozana naye mpaka kwenye gari ambapo walitembea kwa nusu saa tu kisha wakashuka, mbele yao ilikuwa inaonekana Helikopita ya kampuni la Decan miongoni mwa helikopta ghali zaidi duniani.

Safari ya kuingia kwenye ardhi ya wazaramo ilianzia hapo, ambapo kwa takribani nusu saa tu walikuwa wameshafika tayari, mwanaume alishuka na kuna mwanaume mmoja ambaye alikuwa amevaa suti nzuri sana alienda kumpokea na kumpa heshima yake mtu huyo na kwa namna alivyokuwa akimpa hiyo heshima alionekana ni mtu ambaye alikuwa anamheshimu sana, walikuwa wamekaa kimya sana kwenye hiyo gari hata mtu huyo ambaye ndiye alikuwa anaiendesha gari hiyo hakuhitaji kumsumbua mwanaume huyo ambaye alionekana kuwa kwenye tafakuri nzito sana.

“Bosi tunaenda hospitali au nyumbani?” lilikuwa ni swali la mwanaume huyo kuelekea kwa Jason
“Nipeleke nyumbani” alijibu kifupi tu na kufumba macho alionekana hakuhitaji usumbufu na utulivu ulitakiwa kuchukua nafasi yake. Gari ilikuwa kwenye mwendo mkali muda mfupi tu walikuwa wamefika ndani ya nyumba hiyo ambayo aliona kwa mbali imezungushiwa vizuizi mbali mbali na kuwaona baadhi ya askari wakiwa wanazunguka pale wengine wakiendelea kupima pima, gari ilisimamishwa na mwanaume rasmi akawa anashuka ndani ya hiyo gari akiwa katika ardhi ya nyumbani. Aliiangalia sana nyumba hiyo ambayo ilikuwa mbele yake ilikuwa inamkumbusha mbali sana kipindi hicho wanaishi kwa furaha,kaka yake na shemeji yake walikuwa wakimdekeza sana na kumfanya ajihisi kama ilikuwa ni jana yake, alianza kujongea taratibu kuelekea kwenye mlango wa hilo jumba la kifahari, geti lilikuwa wazi hivyo alipitiliza ndani moja kwa moja lakini alizuiwa na askari.

“Hey wewe mpumbavu hivi huoni kama kuna vizuizi hapa unakuja kutafuta nini? usije ukafanya nikakupa kesi ya mauaji ambayo yameweza kutokea hapa siku ya leo” askari huyo alikuwa akipiga makelele huku akiwa anamsogelea Jason na kifua chake kakitunisha vilivyo, hatua moja ilibaki afike alipo huyo mwanaume alishtukia anapigwa kofi moja zito sana kwenye shavu lake mpaka yeye mwenyewe alishangaa raia wa kawaida anampigaje kofi la namna hiyo tena askari kabisa kama yeye, wenzake walitoa silaha zao na kumuweka Jason chini ya ulinzi, aligeuka kuwatazama zamu kwa zamu kisha akayarudisha tena macho yake kwa yule askari wa kwanza ambaye alikuwa anamfokea.

“Ikija kutokea ukaja kunitolea maneno kama hayo tena kwenye maisha yako sitakupa nafasi nyingine tena ya kuendelea kuishi, lizingatie sana hilo” alitamka kitu ambacho kila mtu alibaki anamshangaa mtu ambaye hawakujua ametokea wapi na alikuwa akiongea maneno ya kijasiri sana mbele ya askari wa jeshi la polisi.

Wakiwa hawajafanya chochote nje ulisikika msafara wa magari ukiwa unaingia mahali hapo, askari wote walipiga saluti baada ya kumuona kiongozi wao akiwa anaingia hapo ndani na baadhi ya askari, alikuwa ni IGP Lusubilo Mtindiga, hakuitikia salamu zao zaidi alienda kumpa mkono Jason

“Pole sana kwa yote yaliyo kukuta, najua sio rahisi sana kuweza kuyavumilia ila MUNGU akusaidie sana kwa nyakati hizi ngumu kwako” alitamka mzee huyo huku wakianza kutembea taratibu na Jason kuelekea upande wa pili mwa nyumba hiyo eneo ambalo lilikuwa na bustani nzuri sana pamoja na eneo kubwa la kuweza kupumzikia, maaskari wote walibaki kwenye mshangao kivipi mtu huyo aonekane kujuana na kiongozi wao na wao hawamjui?

“Kipi ambacho kimetokea wakati nipo huko? Ni ghafla sana kaka yangu jana wakati naongea naye simu ilikatika na nilisikia mlio wa risasi unaweza ukanieleza kwa undani ni kitu gani ambacho kinaendelea mpaka saivi na kuniambia mmefikia wapi?” aliongea akiwa ana uhakika na anacho kisema Jason hakuwa na wasiwasi sana kuuliza hali ya hao ndugu zake alikuwa anajua kitu ambacho kilitokea kwa sababu ni habari ambazo zilitapakaa kila sehemu.

“Ilikuwa ni ghafla sana tukio kama hilo kuweza kufanyika na hakuna ambaye alitegemea kwa sababu alikuwa mahakamani kuweza kuhukumu kesi ya yule mtu na ndipo hapo inadaiwa matatizo yalipo anzia, baada ya kumhukumu yule mtu inadaiwa kwamba aliondoka pale mahakamani akiwa mtu mwenye wasiwasi sana na haikuwa kawaida yake kwa sababu ni mtu ambaye huwa anayafanya mambo yake kwa weledi sana hivyo kuondoka na hali ya sintofahamu kama nilivyo ona kwenye kamera za pale mahakamani basi ilinipa jibu kwamba hakukuwa na usalama wakati anaondoka. Baadae nakuja kupigiwa simu kwamba kwa mheshimiwa jaji mkuu kumevamiwa na watu wameuawa ambapo ni yeye na mkewe mjamzito pamoja na mwanae wa kike, ni kitu ambacho kilikuwa kigumu kwangu mimi kuweza kuamini kwa sababu najua yule ni miongoni mwa watu ambao wanalindwa vizuri sana hivyo nilituma vijana wangu ambao wapo kituo cha karibu na hapa wakati huo mimi nilikuwa njiani ninakuja huku.”

“Baada ya kufika ndipo nilishangazwa sana na namna tukio lilivyotendeka, moja kwa moja kabla ya kufanya kitu chochote kile niliamua Kwenda kuangalia cctv kamera za humu ndani ila bahati mbaya sana sikuweza kukuta huo mkanda ambao una video za takribani mwezi mzima, zilikuwepo tu za kuanzia mwezi ulio pita kurudi nyuma inaonekana kwamba mtu ambaye alikuwa amehusika na hili tukio ni muda mrefu sana alikuwa akilipanga hilo shambuzlizi lake japo hakuna uhakika juu ya hilo na kama ni la kweli basi mtu huyo alikuwa anajua kitu ambacho anahitaji kukifanya na yale ambayo yangetokea baadae ndiyo maana alikuwa anaipanga mipango yake tangu mapema sana( Jason alimkazi sana macho IGP kwenye suala la video hapo)” mzee huyo alimeza mate kisha akaendelea.

“Niliumia sana baada ya kuuona mwili wa rafiki yangu kipenzi ukiwa kwenye hali kama ile, sitaki sana kusimulia kilicho tokea pale ila iliniuma sana kwa sababu mtoto aliuawa kikatili sana pamoja na mama yake ambaye alikuwa mjamzito lakini hata jaji mkuu mwenyewe lile tukio lilikuwa la kusikitisha sana. kitu ambacho nilikifanya moja kwa moja ilikuwa ni Kwenda kuikagua simu yake kwa watu wa mawasiliano kwenye kitengo chetu kule kuna meseji ambazo tulizikuta mle ndani kama tatu, ya kwanza alitumiwa usiku na namba ambayo ni private number hivyo haikuonekana na tumejaribu kuifuatilia sana ila inaonekana kwa mara ya mwisho ilitumika kutoka London Uingereza hivyo tumeshindwa kujua kwamba alikuwa ni nani ambaye alikuwa anaitumia hiyo namba lakini meseji ya pili, ilitumwa wakati anaelekea kwenye kesi ikimsihi kama akimuachia huru yule muuaji basi ataingiziwa bilioni kumi za kitanzania na familia yake itakuwa salama ila mbali na hapo basi ataikosa familia yake, sina uhakika kama aliisoma au alikuwa amesha ondoka ila tumekuja kuiona meseji nyingine ya tatu ambayo alitumiwa baada ya yeye kumaliza kutoa hukumu na hapo alipewa dakika kumi na tano tu za kuwahi kuiokoa familia yake na ndio muda ambao alitoka kule mahakamani na kuwahi nyumbani kwake kwa sababu ya familia yake na ndipo mauti yalipo mkuta” mzee huyo alielezea kwa kirefu kifogo ila kwenye maelezo yake wakati anataja idadi ya meseji ambazo zilikutwa mle ndani ni kama alisita kiasi fulani na Jason alikuwa amelisoma hilo ila aliamua kukaa kimya na kumsikiliza kwanza IGP.

“Sawa naomba nipeleke kwenye eneo la tukio na unionyeshe kila hatua kwa kile kitu ambacho kilitokea mpaka hao watu wanatekeleza hilo tukio lao, naomba usiruke hatua hata moja, sihitaji maelezo ya walinzi wa getini nahitaji kilichokuwa kimeendelea ndani halafu baada ya hapa naomba nikutane na kiongozi wa hao askari ambao uliwaagiza siku ya jana waweze kuja hapa kufanya uchunguzi wa awali kisha baada ya hapo naomba nipelekwe hospitali na miili hiyo isifanyiwe kitu chochote kile bila mimi kuiona na nikienda hospitali nahitaji niingie pekeyangu kwenye chumba ambacho miili imehifadhiwa” Jason alitoa maelezo ambayo hakusubiri hata majibu kutoka kwa IGP alinyanyuka na kumpisha kiongozi wa jeshi la polisi huyo aweze kutangulia ili aweze kumpa kinaga ubaga wa hilo tukio, ila swali ambalo hata wale maaskari walikuwa wakishangaa kivipi mtu huyo hakuonekana kumuogopa hata IGP kabisa na alikuwa anaongea nae kawaida sana hakuna ambaye alijua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea hiyo ilikuwa ni siri baina ya watu hao wawili ambao wenyewe walionekana kujuana vyema kabisa na wala hilo halikuwa na shaka sana kwa upande wao hao wawili.

“Kwa inavyoonekana ni kwamba wakati mhusika anaua walinzi wote nje mawasiliano ndani ya hii nyumba yalikuwa yamekatwa kwa sababu kwa aina ya mauaji inaonekana kabisa kwamba yalifanywa na mtu mmoja tu basi, muuaji aligonga geti kama mtu wa kawaida tu na geti dogo likafunguliwa na hapo ndipo aliingia na yule mlinzi ambaye aliingia naye kwa kumfyatulia risasi kwenye paji la uso wake baada ya kufika ndani aliwamiminia risasi walinzi wote wa pale getini ambapo inaonekana wengine walikuwa wakicheza karata pembeni maana zimekutwa na ndiyo maana ilikuwa rahisi sana kuweza kuwashambulia. Hapa panapo fuata panaleta ukakasi mkubwa sana kwa sababu hatua za kutoka getini mpaka kuja kufika hapa ulipo mlango wa kuingilia ndani haikua rahisi kufika bila walinzi wa lango la kuingilia ndani kumshambulia mvamizi maana yake hapa kuna vitu viwili, cha kwanza ni kwamba huyo mtu ambaye aliivamia hii nyumba alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana kwa sababu sio rahisi mtu wa kawaida kuweza kumudu spidi ya kutoka pale mpaka hapa bila kushambuliwa, lakini kitu cha pili ni kwamba inawezekana ni mtu wa karibu sana ndiye ambaye aliweza kufanya hili tukio kwa sababu huenda alikuwa anajua vizuri kwamba watu hao huwa wanakaaje na kwa muda gani huwa wanakaa hivi ndiyo maana ilimpa urahisi kutekeleza tukio lake”

“Nimesema kwamba mawasiliano yalikatwa kwa sababu kuna vifaa maalumu hawa viongozi na wake zao huwa wanawekewa kwenye miili yao na nadhani hiyo kazi wewe mwenyewe ndiye uliisisitiza sana ifanyike haraka, sasa kama ni hivyo mpaka walinzi wote wanauawa maana yake wakati wanashambuliana lazima wangetoa taarifa kwa jaji pamoja na mkewe ambaye alikuwa ndani huenda angechukua hatua ambayo ingemsaidia kuyaokoa maisha yake pamoja na ya wanae lakini cha ajabu yeye hakuwa na taarifa yoyote juu ya hilo na hili tumelithibitisha kwa sababu hii (mheshimiwa alimeza mate kisha akausukuma mlango wakaingia sebleni)”

“Wakati tunafika hapa ni kwamba tumeukuta mwili wa mtoto ukiwa upo kwenye kochi na tv iko on maana yeke mtoto aliuawa akiwa anaendelea kuangalia runinga kama mama yake angekuwa na taarifa kwamba kuna hatari lazima angekuwa amemtoa mtoto wake eneo kama hilo lakini pia mke wa jaji alionekana hakuwa na taarifa yoyote ndiyo maana alikuwa kwenye chumba chake akiwa amepumzika hilo linatosha kuthibitisha kwamba hakukuwa na mawasiliano yoyote ambayo yalifanyika” mheshimiwa alishusha pumzi ndefu sana huku akiwa anamuonyesha Jason sehemu ambayo mtoto huyo alifia, mwanaume macho yake yalikuwa makavu sana usinge amini ukiambiwa kwamba alikuwa ameipoteza familia yake siku ya jana yake tu na hata miili yao hakuwa ameiona bado.

Walianza kupandisha huko ghorofani ambako ndiko kilikuwa chumba cha kaka yake, wakiwa wanaendelea kupandisha ngazi na IGP akiwa mbele alisikia sauti nzito nyuma yake

“Bado kuna taarifa hujamalizia kunipatia wakati unanipa habari za tukio zima kwa namna lilivyo tokea”
“Taarifa zipi hizo?”
“Bodyguard binafsi wa brother yuko wapi?” lilikuwa swali ambalo lilimfanya IGP amgeukie mwanaume huyo.

Huyo bodyguard yuko wapi? sehemu ya 7 tutie nanga hapa.

Bux the storyteller.
FB_IMG_1680324048558.jpg
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 8

SONGA NAYO............
Lile swali kidogo lilimshtua sana mheshimiwa IGP alionekana hakujiandaa kushtukizwa swali kama hilo kwa huo muda, aliguna kidogo kuliweka koo lake safi.

“Wakati lile tukio la kutumiwa sms pale mahakamani likitokea na yeye kuondoka akiwa anakimbia kama vile kachanganyikiwa hakuna sehemu yoyote ile ambayo mtu huyo alionekana japo wakati anatoka ndani ya mahakama walikuwa wote ila hatukujua alipotelea wapi na tangu hapo hajaonekana tena mpaka hivi ninavyo ongea nawewe hatujui kama amekufa au kama yupo hai?

“Mmefanya kitu gani baada ya kulitambua hilo?”
“Hakuna tulicho kifanya kwa sababu kwa sasa mambo ni mengi sana, huko tuna majukumu ya kuchunguza kuhusu mheshimiwa raisi na hili la jaji mkuu limeibukia njiani hivyo tumeamua kuanza na haya kwanza halafu kuhusu huyo mlinzi wake kama zitatoka taarifa kwamba anahusika kwa lolote basi tutahakikisha tunaanza naye ili aje atoe maelezo”

“Mbona mnafanya kazi kienyeji sana, hivi labda nikuulize swali rahisi tu una watoto wangapi?”
“Wawili”
“una ndugu yeyote kwako?”
“Ndiyo nipo na wadogo zangu wawili”

“Vipi siku ukija kusikia kwamba wameuawa halafu hujui kilicho waua ni nini kwenye mazingira kama haya utachukua uamuzi gani?”

“Lazima wahusika watatafutwa na ikiwezekana wachukuliwe hatua kali sana”

“Nadhani umeelewa kwamba mpaka sasa hakuna jibu sahihi ambalo umenijibu kwenye maswali yangu, kwa sasa naomba nipe nafasi huku chumbani naingia mwenyewe wewe utasubiri nje hapa halafu nitakuwa na mazungumzo nawewe baada ya hapa” IGP alikuwa mpole tu kwa mwanaume huyo wala hakuwa na makuu yoyote ikambidi arudi mpaka kwenye ngazi ya chini akakaa hapo na kujishika tama wakati huo mwanaume alikuwa anaingia kwenye hicho chumba ambacho kaka yake pamoja na shemeji yake aliyekuwa na mtoto tumboni waliuawa.

Aliusukuma mlango huo na kusimama akiwa anakadiria namna ndani palivyokuwa, kulikuwa na damu kiasi ambayo ilikuwa imeganda kwenye sakafu alisogelea hilo eneo na kuigusa damu hiyo akiwa anaangaza kila sehemu, macho yake yalikuwa mekundu sana alikaa chini na kutoa kitambaa alijifuta machozi yake, kuna kitu Kizito sana kilikuwa kinamkaba shingoni alisimama na kujifuta vizuri hakuhitaji mtu yeyote yule ajue kama alikuwa kwenye hiyo hali. Aliangalia kwa umakini sana hicho chumba alikumbuka namna alivyopigiwa simu na kaka yake na matukio machache ambayo aliweza kuyashuhudia siku ile, alisogea kwenye ukuta ambapo palikuwa pamejiziba vyema alibonyeza hiyo sehemu na dole gumba mara mbili pakafunguka ndani yake kulikuwa na kichuma kilicho mhitaji kuingiza namba za siri alifanya hivyo kwa kuingiza tarehe yake ya kuzaliwa na mwaka wake pakafunguka na kukutana na makablasha mengi sana hakuyajali kwa wakati huo alivuta droo ndogo ndani ya hicho chuma humo ndani kulikuwa na funguo nyingi sana, baada ya kuipata ile ambayo alikuwa anaitafuta yeye alifunga hapo ndani kisha akatoka mpaka kwenye kordo moja ndogo huko huko juu alijongea kwa mita sita tu akawa ameufikia mlango mwingine, aliingia mpaka ndani, hiki ndicho kilikuwa chumba cha maktaba ya kaka yake, kulikuwa na vitabu vya kila aina hususani vya sheria ndivyo vilivyokiwa vimejaa huko ndani.

Aliisogelea hilo kabati kubwa sana la vitabu, aligeuka nyuma kama hakuna mtu ambaye alikuwa anamuona alilizungusha likasogea pembeni hapo palikuwa na mlango wa shaba alitoka kifaa muundo wa simu ila haikuwa simu alipitisha kwenye kitasa cha huo mlango, alijiridhisha baada ya kuona kwamba hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa ameugusa mlango huo, akaparudishia kama palivyokuwa mwanzo kisha akafunga hicho chumba na kushuka mpaka pale ambapo alikuwa amekaa IGP alionekana kuwa kwenye mawazo mazito sana.

“Naomba hiyo simu ya brother, baada ya hapo nipeleke huko hospitali iliko hifadhiwa miili yao na hakikisha nakutana na daktari aliye ipokea miili hiyo na kuishughulikia pamoja na huyo askari ambaye alikuwa hapa nyumbani wakati tukio limetokea, hayo yakikamilika sasa nitaomba nikae tena mimi na wewe unieleze kwa kirefu kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa mheshimiwa raisi” Jason aliongea kwa sauti kavu sana ambayo alikuwa na uhakika na anaye ongea naye kwamba alikuwa anamsikia vizuri tu wala hilo halikumpa sana shaka, IGP alinyanyuka na kuuingiza mkono wake kwenye mfuko alitoka na simu hiyo ambayo kiasi fulani ilikuwa imepasuka na kuonyesha kwamba ilikanyagwa tena kwa makusudi kabisa, mwanaume aliipokea halafu wakaongoza nje wote ili waweze kuelekea huko huspitalini kama walivyokuwa wameelekezwa.

Walitoka mpka nje wakiwa pamoja jambo ambalo liliendelea kuleta taharuki kwa maaskari ambao walikuwa nje

“Mheshimiwa huyo mtu ni nani? tumepewa jukumu la kukulinda kama likikukuta tatizo lolote lile sisi tunaingia matatizoni, huyo ni mtu ambaye amekuja hapa kwa namna ambayo haieleweki na mpaka sasa hatuelewi kwamba anafanya nini hapa na yupo hapa kwa ajili ya nani na hata wewe hautupi majibu sahihi” mheshimiwa Lusubilo Mtindiga hakujibu kitu baada ya kuisikia kauli hiyo kutoka kwa kijana wake zaidi zaidi alimsogelea mpaka pale alipokuwa amesimama, alimwangalia sana kisha alimtandika makofi kama Matano ya haraka haraka ambayo yalimfanya kijana yule ahisi amebeba kilo kadhaa za mchanga kwenye mashavu yake kwa namna yalivyokuwa yanawasha, mheshimiwa hakuongea neno lolote aliondoka na kuingia kwenye gari ambayo tayari Jason alikuwa ameingia na IGP alikaa kwenye usukani akiwa anaendesha yeye mwenyewe hiyo gari, walinzi wake walibaki wameduwaa tu.

“Huenda wako sahihi kuhitaji kumjua mtu ambaye muda wote yupo na kiongozi wao na hawana uhakika wa usalama wa kiongozi wao, natamani sana kama wangekuwa makini sana kwenye kila jambo la nchi namna hiyo ila inasikitisha sana linapokuja suala la kuijenga nchi wanakuwa wanazingatia zaidi kuyajenga matumbo yao na si vinginevyo na hapo usikute kijana anatafuta ni cheo” Jason aliongea huku akiwa anaiangalia kwa umakini sana picha ambayo ilikuwa kwenye mkono wake, alikuwepo yeye, kaka yake, mke wa kaka yake pamoja na mtoto wa kwanza wa kaka yake ambapo picha hiyo ilipigwa mtoto huyo akiwa bado mchanga, aliiingiza kwenye mfuko wake wa suruali na kutulia kuendelea kuangalia mazingira ya nje jinsi yalivyokuwa.

“Kama tu uliweza kumficha kaka yako wa damu ambaye ni nusu ya maisha yako, mheshimiwa raisi hakutaka mtu yeyote ajue kuhusu wewe, ni marafiki wachache sana ambao tulibahatika kulijua hili sasa itakuwa hao watoto ambao wanakuja kufanya kazi kwa sababu ya njaa na sio weledi wa kazi? Nadhani wewe mwenyewe utakapo amua wakujue wewe ni nani itakuwa ni vyema zaidi na ukizingatia ni watu wachache sana ambao wanajua wewe ni mdogo wake toka ni toke na jaji mkuu ndiyo maana wanakushangaa, hili tukio ndilo linalo Kwenda kukutambulisha kwamba wewe ndi ndugu yake na jaji kwa sababu serikali imetangaza kukusaidia kama ndugu yake lakini watu wengi hawakujui hivyo kwenye utambulisho lazima utatangazwa na kama unavyojua yule alikuwa ni mtu mkubwa sana hivyo vyombo vya habari vitakuwa vingi sana” IGP aliongea akiwa yupo makini sana kuangalia mbele mikono yake ikiwa ipo kwenye usukani wake.

“Ndiyo maana kaka yangu alikataa sana nisisome sheria kwa sababu aliyajua madhara yake kama haya, najiona kama ni mtu wa hovyo sana kuweza kushindwa kuilinda familia yangu mimi mwenyewe ambayo ndiyo pekee niliyokuwa nayo, wananchi hawatakiwi kabisa kujua uhalisia wangu zaidi watajua tu kama mimi ni ndugu yake na jaji mkuu basi. Mpaka sasa nimechanganyikiwa sijui naamua kipi nakiacha kipi, hakuna kitu kinauma kama kuipoteza familia ambayo ndiyo pekee ulikuwa ukiitegemea kwa kipande kidogo cha furaha cha maisha yako kilicho bakia kukiishi inauma sana tena sana, moyo hauwezi kuongea ila huwa unatoa ishara kwa kupitia macho na baadhi ya sehemu za mwili, najiona mkiwa sana kwenye haya maisha ila niseme tu nikushukuru sana wewe na wengine ambao mlikuwa marafiki wema sana kwa kaka yangu. Nimepatwa na Mikasa mizito sana nimempoteza mheshimiwa raisi ambaye amehusika kuyatengeneza maisha yangu kwa asilimia 40 na zilizo salia zote alizitengeneza kaka yangu lakini kabla hata sijajua nafanyaje kuhusu hilo wameamua kunichukulia pacha wangu, yule kwangu hakuwa kaka tu alikuwa kama pacha, alikuwa kama baba, sikuwahi kuijua shida kwa miaka mingi sana japo tumeishi kwenye maisha ya shida sana”

“Alikuwa tayari kulalia kikombe cha maji yule mwanaume ila hakuwahi kuruhusu mdogo wake nilie kisa njaa, kwangu alikuwa role model wangu na ndiyo mfano bora zaidi ambao nitaufuata siku zote kwenye maisha yangu lakini pamoja na yote ambayo ameyafanya haya bado mpumbavu mimi nimeshindwa kumlinda kabisa. Nitakuwa na dhambi kubwa sana ya Kwenda kujibu kwa MUNGU kama sitageuka na kuwa mtu katili sana kwa sasa MUNGU anisamehe sana kwa sababu naenda kuyaanza maisha yangu mapya kwa kuugeuzia mgongo wema wangu ambao nimeutenda kwa binadamu wasiokuwa na shukrani kwenye haya maisha” Aliongea kwa uchungu sana IGP alikuwa anamtazama kijana huyo na kumuonea sana huruma, walikuwa wamefika tayari ndani ya hospitali ya taifa ya Mhimbili, walishuka na kuanza kuelekea ndani ambapo walikumbana na waandishi wa habari waliokuwa wengi sana baada ya kumuona IGP walimtaka aseme chochote kile kwa kila kilichokuwa kimetokea kwa sababu juzi tu kwenye hospitali hiyo uliletwa mwili wa mheshimiwa raisi ambao jana yake ulipelekwa ndani ya makao makuu ya jeshi la wananchi na jana hiyo hiyo kwenye hospitali hiyo hiyo ulikuwa umeletwa mwili wa mheshimiwa jaji mkuu hivyo taharuki ilikuwa ni kubwa sana hata hivyo hakuna alicho wajibu mzee huyo zaidi zaidi askari walimsaidia kumtengenezea njia yeye na Jason mpaka wakafanikiwa kupita hapo na kuingia ndani, walipanda lifti na kuelekea kwenye vyumba vya VIP huko ndiko ilikuwepo hiyo miili ya ndugu zake .

“Dokta samahani sana huyu hapa ndiye ndugu wa pekee wa marehemu ambaye ulipewa taarifa zake kwamba alikuwa nje ya nchi na ndo amefika saivi hivyo yupo hapa kwa ajili ya kuiona miili ya ndugu zake kabla ya Kwenda kuzikwa hapo kesho hivyo naombeni sana mpeni ushirikiano kwa kila anacho kitaka” Daktari alimpa mkono IGP na kuonyesha kwamba alikuwa amemuelewa vizuri sana na hilo jambo angelifanyia kazi kwa muda mfupi ujao, alimchukua Jason akatoka naye nje ya chumba chake na kuelelea naye mkono wake wa kulia, walitembea kwa sekunde thelathini tu kisha wakakunja mkono wa kushoto huko walianza kukumbana na hali ya ubaridi sana ila mwanaume huyo alikuwa siriasi sana hakuwa ametamka neno lolote lile tangu aingie ndani ya hospitali hiyo.

Daktari huyo alifungua moja ya mlango ambao ndani yake kulikuwa na baridi kali sana
“Sasa wewe waweza Kwenda nahitaji kuwa pekeyangu humu ndani” Dakatari alishtuka mtu huyo alovyosema kwamba anahitaji kubaki yeye mwenyewe, alitaka kuongea kitu ila aliyakumbuka maneno ya IGP kwamba mtu huyo asikilizwe kwa kila ambacho alikuwa anakitaka yeye hivyo ilimlazimu kuondoka na mwanaume akausukuma mlango na kuufunga na komeo kwa ndani, mbele yake yalikuwa ni majokofu ambayo yaliandikwa majina ya familia yake, moja lilikuwa la kaka yake, shemeji yake na mtoto wa kaka yake, alihesabu hatua tatu mpaka lilipokuwa jokofu ambalo lilikuwa na jina la kaka yake, alilifungua lakini alicho kiona kilimshtua sana.

Jason kaona nini? yeye ana nini hasa mpaka hataki kujulikana? Siri gani hizo ambazo anazo alimficha hata kaka yake? Atamjua mhusiKa? Na vipi kuhusu raisi alikuwa na mahusiano naye gani mpaka aseme kwamba amechangia kumtengeneza kwa asilimia 40?.INNOCENT KILLER sehemu ya 8 natia nukta.

shusha vitu mkuu arostooo
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 9

SONGA NAYO............
Jason kitu alicho kiona baada ya kuuona mwili wa kaka yake kilimfanya aume meno kwa hasira sana, aliuangalia kwa dakika kumi bila kukwepesha macho yake. Mwili huo ulikuwa na tobo la risasi kwenye paji la uso wa kaka yake, alisogelea sehemu ambapo lilikuwa limeandikwa jina la shemeji yake napo aliangalia kwa umakini sana na kuona kitu kile kile risasi ilipita kwenye paji la uso.

Alikumbuka vizuri kwamba shemeji yake alichomwa na kisu maeneo ya tumboni aliyafumba macho yake akijaribu kuvuta hisia kwa mtu kukosa huruma mpaka kufikia hatu ya kuweza kumchoma kisu mwanamke mjamzito namna hiyo, inahitajika mtu kuwa na roho ngumu sana.

Alienda kumalizia kwenye jokofu lililokuwa na jina la mtoto ambaye alikuwa anapenda sana alivyokuwa anamuita baba mdogo, huyo ndiye pekee aliwahi kumfanya naye ajihisi ni baba kwenye hii dunia, alivuta taratibu sana kuonyesha kwamba hakuwa tayari kuona kilichokuwa mbele yake ila hakukuwa na namna alihitaji kujihakikishia mwenyewe kile ambacho kilikuwa kimetokea, mtoto alikuwa ameyafumba macho kama vile alilala na angeamka ila ni kitu ambacho kilikuwa ni ndoto tu na isingewezekana kuwa kweli hata kama ungekuwaje.

Kama alivyokuwa ametegemea hata huo mwili pia ulikuwa una risasi kwenye paji la uso, aliinama na kumbusu mtoto huyu kwa dakika nzima akiwa ameinamisha uso wake hapo alinyanyuka na kuanza kuzunguka humo ndani kama mtu aliye changanyikiwa mpaka akaenda kukaa kwenye kona ya hicho chumba cha kuhifadhia maiti licha ya kuwepo kwa baridi kali sana humo ndani ila kwake haikuwa sababu ya msingi sana ya kumfanya kutoka haraka.

Yaliisha masaa mawili mazima ndipo mlango huo ulipo funguliwa na mwanaume huyo akatoka na kuurudishia mlango kama ulivyokuwa, alitembea taratibu mpaka kwenye ile ofisi ambayo kwa mara ya kwanza alipelekwa na IGP, aliingia bila hata kugonga na kumfanya IGP na daktari huyo kushtuka sana hawakujiandaa na ujio wake humo ndani.

“Nina maongezi nawewe nifuate” aliongea na IGP kisha akatoka nje kumsubiria mtu wake huyo, IGP alibaki anaangaliana na daktari tu mle ndani

“Hivi huyu ndiye mfiwa kweli? Mbona hana hata wasiwasi wala dalili za kuonyesha kwamba ni mtu mwenye majuto kupotelewa na familia yake? Halafu mbona kama anakuchukulia kawaida sana kwamba hajui kama wewe ni kiongozi mkubwa kwenye nchi hii” daktari alimuuliza IGP akiwa anajiandaa kutoka Kwenda kuongea na mtu wake huyo, IGP aligeuka na kulazimisha tabasamu

“Jambo usilo lijua ni sawa na usiku wa giza hivyo kuna mambo usilazimishe kuyajua yatakuja kuhatarisha maisha yako, kuhusu familia hakuna binadamu ambaye anafiwa na familia anayo ipenda sana halafu akafurahia au kuwa kawaida sema kuna watu wamefunzwa kuwa wanaume unaweza ukamuona anacheka sana ila moyo wake unalia kuliko unavyo fikiria wewe shida yako umezoea sana hizo kazi za kubembelezana na wagonjwa hivyo hata kulia kwako ni rahisi sana yule hayupo vile mpaka unamuona yupo siriasi sana jua ni mtu ambaye anatokwa machozi kila dakika ila hayo machozi wewe hapo huwezi kuyaona kwa sababu umechagua kuyaamini sana macho yako kuliko hisia” IGP alijibu kwa mafumbo na kumuacha daktari huyo kwenye njia panda wakati huo aliubamiza mlango huo na kutoka nje ambapo alikohoa kidogo baada ya kumkaribia Jason ili kumpa taarifa kwamba alikuwa amefika.

“Kwanini unanipa taarifa nusu nusu?” swali la Jason lilimshtua kidogo mheshimiwa

“Una maanisha nini kusema hivyo?”
“Unajua wale waliokufa ni akina nani kwangu?
“Ni familia yako”

“Sasa mbona unanipa taarifa kama vile nimefiwa na jirani yangu au mtumishi mwenzengu?”
“Taarifa ipi hiyo ambayo wewe unaihitaji na haujaipata kama ulivyokuwa umetarajia?”

“Umenipa maelezo mengi sana lakini hakuna sehemu ambayo umenielezea kwamba familia yangu imekufaje na hicho ndicho nilichokuwa nakihitaji”

“Bado sijakuelewa”

“Una kichwa Kizito sana sijui ulipewaje hiyo nafasi”

“Sasa nafasi yangu inahusiana vipi na swali lako?”
“Nimekuuliza walikufaje? Mbona hujanambia kama miili yote ilimuwa na risasi kwenye kichwa”

“Daaah nilikuwa mbali sana haya majukumu naona kabisa kwamba yananizidi sasa ndiyo maana hata sikuwaza huko kwa sababu nilijua utayapata kwenye ripoti ya madaktari wanavyokupatia taarifa ya vifo vyao”

“Mhhhhhhh kiwepesi tu namna hiyo”

“Yes, imegundulika kwamba wote mpaka walinzi walipigwa risasi za kwenye paji la uso ndiyo maana nilisema kwamba muuaji ni mmoja tu na sio wengi kwa sababu aina ya mauaji iliyotumika ilikuwa ni moja tu basi”

“Sijajua kwamba ni kwanini kiwepesi tu namna hiyo ulininyima hizo taarifa ila kwa sasa nahitaji niandaliwe hiyo ripoti na daktari nitakuja kuichukua na huyo daktari mwenyewe nitahitaji kukutana naye, pia utanipa namba ya nyumba ya huyo askari ambaye alifika pale mapema sana kuja kufanya uchunguzi baada ya tukio, hivyo sivihitaji saivi labda tu namba ya nyumba ya huyo askari nitumiwe ndani ya muda mfupi ila ripoti ya daktari naihitaji siku moja baada ya msiba”

“Kwa muda huu hapa nina vitu viwili, kitu cha kwanza naihitaji hiyo video ambayo inaonyesha mheshimiwa raisi akishambuliwa na huyo mtu mpaka kufa na kingine nataka kujua kwanini ulinambia uongo” ishu ya video IGP hakushtuka sana japo alisita ni kama alitarajia mtu huyo angeiomba tu kwa namna yoyote ile ila kilicho mshtua sana ile ya kusema kwanini alimwambia uongo, alibaki anawaza uongo upi wakati asilimia zote alikuwa anatoa maelezo ya kitu ambacho anakijua? Ilimbidi alijibu ili asije akashtukiwa.

“Uongo upi huo ambao unausema?” Jason alimwangalia sana mzee huyo

“Najua kwenye ile simu hakukuwa tu na zile sms tatu kama ulivyosema wewe, kuna sms uliamua kuzimezea na sijajua kwanini na kwa sababu zipi, hilo utaenda kujitafakari mwenyewe kisha tutaongea vizuri siku nyingine kwa sasa nionyesha hiyo video ya kuuawa kwa raisi” Aliongea bila kitetemeshi chochote kile, IGP hakuongea kitu chochote zaidi alinyoosha kwenye njia ambayo ilikuwa inawapeleka kwenye lifti, walishuka mpka chini na kuelekea kwenye gari yake ambapo waliingia na kufunga milango yote, alitoa simu kwenye droo yake na kumpatia Jason ambaye aliifungua na kuangalia kwa dakika tano video hiyo fupi ambayo ilikuwa inajirudia rudia.

“Pumbavuu, inawezekana vipi raisi wa nchi auawe kirahisi sana namna hii?” aliongea kwa hasira sana akiwa amemkazia macho IGP ambaye alibaki ameinama tu

“Si nakuuliza wewe hapo au haunisikii? Nitajibu vipi hili suala kwa watu ambao mliaminika mtamlinda huyu mtu ndo mkaacha afe kizembe sana namna hii, shiiiiiiit this is lunatic” alifoka kwa hasira sana Jason na mzee huyo ambaye kwa umri alikuwa mkubwa sana alikuwa ametulia tu akimsikiliza kijana huyo hakutaka kabisa kumuingilia kwenye hizo hasira zake.

“Ok kama huwezi kunijibu hilo kwanini mmeruhusu ahukumiwe mtu ambaye siyo muuaji? Ina maana huu ulikuwa ni mpango endelevu wa kumuua na kaka yangu sio?” hayo maswali ya Jason yalimshtua mzee huyo baada ya kusikia kwamba walikuwa wamemhukumu mtu ambaye alikuwa hahusiki na chochote kabisa

“Mbona sijakuelewa”
“Mzee ujue nakuheshimu sana na nadhani unajua miongoni mwa vijana ambao huwa wanakupenda sana namimi nipo na unalijua hilo ila usitake tuende kuwa maadui hapo mbeleni nitakusahau kama sijawahi kukuona kwenye maisha yangu. Ni nani ambaye alimkamata huyo mtu ambaye amenyongwa kama muuaji? Nani alifanya huo uchunguzi?”

“Tulipewa taarifa kwamba huyo muuaji alikamatwa na jeshi la wananchi hivyo sisi hatukuwa na namna zaidi ya kufuata mamlaka zilizokuwa zimemshikilia kwa sababu walituambia itabaki kuwa hivyo na hapo ndipo tulipo ingilia kati kuanza kufanya uchunguzi lakini tulizuiliwa na kuambiwa kwamba watu wa ikulu watahusika na hilo na sisi tutashughulika na mengine ambayo yataendelea mbele” IGP alijibu jibu ambalo ni kama mtu huyo lilimuacha njiapanda sana kwa namna alivyo jibiwa kiwepesi sana

“Huyo aliyewapa hiyo amri ni nani?”
“CDF alitupatia hiyo taarifa kwamba imeamuliwa iwe hivyo”

“Huyo CDF anahusika nini na mheshimiwa raisi mpaka yeye ndiye atoe amri ya taarifa ya uchunguzi? Na yeye anahusika nini na ikulu? Sasa naomba umpe taarifa kwamba leo usiku nataka nikutane naye tukiwa wawili tu, akiukuuliza nani mwambie mdogo wake jaji anakuhitaji sana kuliko hata maisha yake nadhani yeye ndiye aje anipe hayo majibu sahihi”

“Sawa hilo nalifanyia kazi lakini sijakuelewa ulivyosema kwamba amehukumiwa mtu ambaye hahusiki” IGP alihitaji sana kuzijua hizo taarifa

“Kaka amekufa baada ya hukumu na yule mtu kunyongwa sio?”

“Ndiyo”

“Umeona namna raisi alivyokufa”

“Ndiyo alipigwa risasi”

“Ya wapi?”

“kwenye paji la uso”

“Na familia yangu imeuliwa vipi?”

“Kwa risasi za paji la uso” hapo sasa hata IGP akili yake ilifunguka, alijiona kuwa ni mzembe sana kushindwa kung’amua hicho kitu mapema ni mchezo mdogo sana ambao hata mtoto mdogo anaweza kuutegua bila hata kutumia nguvu.

“Muuaji hapa ni mmoja, maana yake mtu aliyeweza kumuua mheshimiwa raisi ni yule yule ambaye aliiua familia yangu, sasa kama alikamatwa na kunyongwa kivipi aue familia yangu baada ya kufa? ni kitu ambacho hakiwezekani inamaanisha huyo mtu yupo hai ila kuna mchezo tu wa akili ndogo wameamua kuucheza sasa naingia mimi mwenyewe kwenye huu mchezo nikacheze nao hilo draft ambalo wamelichora wao wenyewe na sheria wamezitunga wao wenyewe” aliongea kwa msisitizo sana Jason akiwa anaufungua mlango ili atoke humo ndani.

“CDF nimwambie mkutane saa ngapi?”

“Mwambie saa 6 kamili usiku nitakuwa nje ya nyumba yake na unitumie namba ya nyumba ya huyo askari wako muda huu” mwanaume aliongea hivyo na kuondoka IGP alibaki anashangaa jasho likiwa linamtoka, kwa muda mfupi sana aliona mambo yanaenda kuwa mabaya kuliko hata ilivyokuwa imekadiriwa, alichukua simu yake na kuitafuta namba ambayo alikuwa ameisevu Jaiwelo Mkupi Makubilo huyu ndiye ambaye alikuwa CDF mwenyewe mkuu wa majeshi, aliruhusu simu hiyo iweze kupiga, iliita kidogo na kupokelewa.

“Nakuja kwako ndani ya dakika thelathini zijazo” hakusubiri hata kujibiwa alikata simu na kuwasha gari yake kisha akaondoka kwa kasi sana hilo eneo.

Jason Japhary ni nani huyu kijana mpaka anajiamini sana namna hii mbele ya watu wakubwa sana serikalini kama hawa wakati kuna watu wanamjua kama ni kijana laini sana asiye na makuu na mtu waweza kumuita mtoto wa mama? ……. bado tupo taratibu twende pamoja michezo ya akili imeanza tukaitafutie majibu halisia.

Chuma kabisa hiki, umetisha sana mkuu
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 10

SONGA NAYO............
Ndani ya dakika thelathini na tano mheshimiwa IGP alikuwa anaingia getini kwa CDF gari yake ilikuwa inajulikana sana hivyo alifufuliwa geti bila wasiwasi, baada ya kushuka alinyoosha moja kwa moja mpaka sehemu ya nyuma ya nyumba hiyo, alikuja mwanamke mmoja mzuri sana ambaye alimletea kahawa ambayo ndiyo ilikuwa kitu pendwa saa kwa mzee huyo kisha akampa maelekezo kwamba mtu huyo alikuwa hayupo wakati anampigia simu hivyo atarudi ndani ya dakika 15 zijazo, haikuwa shida sana kwake kuweza kusubiri hapo huku akiendelea kupata kahawa yake.

Dakika ishirini zilitosha kusikia hatua za buti kubwa ambazo hakuwa na shaka na mtu ambaye alikuwa amezivaa, alijua ni mkuu wa majeshi ndiye ambaye alikuwa amefika hiyo sehemu, akiwa anaangalia mbele sehemu ambayo ilipandwa miti mizuri kwa mpangilio iliyokuwa karibu na bwana la kuogelea ambayo iliifanya sehemu hiyo kuwa ya kuvutia sana alitamka kwa sauti moja ya utulivu sana.

“Kila nikisikia kuhusu hizo hatua za hivyo viatu basi huwa nakumbuka mbali sana, mwaka ule tupo kwenye mafunzo ya jeshi kule Msangi Tabora tulikuwa watu watano ambao tulishibana kwa kila kitu, siku ile rafiki yetu mmoja alipo kufa kwa sababu ya kukuokoa siwezi kuisahau kabisa ile ni moja ya stori mbaya sana kwetu lakini ni kumbukumbu moja nzuri sana kwenye maisha yetu sisi kama marafiki” alivuta pumzi kidogo kuacha hayo maneno yamuingie vyema mtu ambaye alikuwa akimpa hiyo taarifa.

“Tuliingia kwenye orodha ya marafiki bora zaidi kuwahi kutokea hapa duniani, tulibaki wanne ambao tuliapa kubebana na kusaidiana kwenye kila hatua ambayo tungeipiga kwenye maisha yetu na ilibaki kuwa hivyo hata pale mwenzetu alipo fanikiwa kuwa raisi wa nchi basi hakuweza kabisa kutuacha alimpa kila mtu kitengo ambacho alikuwa anakihitaji na kukielewa kwa upana lakini kati yetu wote tulikuwa tunamtegemea sana jaji mkuu kwa sababu ametusaidia sana na ndiye mtu ambaye tulikuwa tunamtegemea kwenye kila mpango wetu, alikuwa ni mtu mwenye akili zaidi kati yetu sisi wanne lakini hata hivyo imekuwa pigo kubwa sana kuwapoteza marafiki wote wawili tena kwenye mazingira ya kutatanisha sana na kwa muda mfupi mno” aliongea na kushushia kahawa yake, mkuu wa majeshi alikuwa akisikiliza huku amesimama akiwa ndani ya kombati ya jeshi ambayo ilimpendeza sana pamoja na buti kubwa sana nyeusi ambayo ilikuwa imesafishwa vizuri mno begani kwake kukiwa kumejaa nyota za vyeo mbali mbali, aliisogea pembeni na kuketi kwenye hicho kiti ambacho kilikuwa kinawatosha watu wawili akaingiza mfukoni na kutoa pombe ndogo lakini kali sana ambayo ilikuwa kwenye kibati akamkabidhi rafiki yake huyo kama alivyo dai na kuendelea kuinywa ya kwake huku akiwa anakunja uso wake kwa ukali wa pombe hiyo.

“Maisha hayana tafsiri halisi ila namna tunavyokuwa tunayaishi ndivyo yanavyotupa tafsiri sahihi ni namna gani tunapaswa kuyachukulia, hiki ndicho kitu pekee ambacho ninaweza kukifanya kwa ajili ya rafiki ambaye aliamua kuyatoa maisha yake siku ile kwa ajili yangu, ile kamba ambayo alinirushia na yeye kuamua kudondoka ili mimi niidake na kupona yeye akaishia kudondokea kwenye yale mawe yaliyokuwa yamechongoka sana basi huwa inanifanya niumie sana ila kwa baadae nilikuja kugundua kwamba kwenye maisha kila kinacho toke abasi huwa kina sababu nzito sana nyuma yake huenda mimi kubaki hai kulikuwa na sababu nzito sana na hiki ndicho ambacho mimi huwa nabaki namuenzi”

“Alikuwa anaipenda sana hii pombe na tangu siku ile amekufa basi mimi niliapa kwamba ningeinywa hii pombe mpaka siku naingia kaburini na ndicho ambacho huwa nakifanya kila siku mpaka sasa. Kuwa na marafiki ambao kwako ni kama familia huwa ni kitu bora zaidi kwenye maisha ya mwanadamu hususani unapokuwa unapata nafasi ya kufurahi pamoja na hao marafiki zako, kama ulivyosema tuliishi zaidi hata ya ndugu kwa sisi wanne ambao tulikuwa tumebaki na ndiyo maana mpaka leo wote tumeishi maisha mazuri sana kwa sababu tuliamua kumpigania mmoja kutimiza ndoto yake kisha na yeye akatutimizia ndoto zetu sisi ila kama tungeamua kila mtu aanze kuwa na wivu na mwenzie basi saivi usikute tungeishia kuwa wapiga debe kama sio kuwa vibaka huko mtaani ila kwa sasa tunachagua tule nini na nchi gani tuende kwa sababu tuna kila kitu kwenye maisha, ni wakati mgumu sana tutapitia kuwapoteza hawa watu wawili mhimu sana kwenye maisha yetu nitawaombea siku zote huko waliko waweze kupumzika kwa amani kwa maana wamefanya mambo makubwa sana kwetu na kwa nchi yetu pia” mheshimiwa CDF aliongea akiwa anaongeza kinywaji kingine kwenye mdomo wake na kumfanya IGP atabasamu kwa maumivu kwa sababu sio kwamba walikuwa wanafanya mazungumzo ya kuweza kufurahishana ila bali mazungumzo yao waliamua kujikumbushia zaidi nyakati za furaha ambazo wao waliziishi wakati wapo na wenzao.

“Nilikuwa najua kama kuna kufa ila sikuwahi kuwaza kama tutakuja kuanza kupotea mmoja mmoja kimaajabu na kwa vifo vya kutisha sana namna hii inanifanya naanza kuogopa sana kwa sababu sijui kama kesho utafuata wewe au nitakuwa ni mimi, kuna muda natamani niendelee kuaiamini dunia lakini nashindwa najikuta hata nafsi yangu siiamini bado na sina jibu la kujipa. Hivi unafanya nini pale yule mtu ambaye ni wa mhimu sana kwenye maisha yako halafu unakuta ana ukakasi mkubwa kwenye kuyapunguza maisha ya watu wengine ambao nao ni wa mhimu kama yeye kwenye maisha yako pia?” IGP aliuliza kitu ambacho kilimshtua sana CDF lilikuwa ni kama swali la mtego hata hivi hakuhitaji kuonekana kwamba yeye ndiye kashtuka sana, aliangalia juu angani kisha akayarudisha macho yake chini.

“Kama huyo mtu anaweza kuleta madhara makubwa kwa wenzie basi ni wazi hatatakiwa kuwepo kati yao au kati ya watu wa aina yoyote ile kwa sababu hatakuwa sehemu ya furaha ya binadamu wenzie zaidi atasababisha hata ile furaha ndogo iliyopo kwa wenzake kutoweka hivyo hatakiwi kuwepo kwenye kundi la hao watu kwa namna yoyote iwe kwa nguvu au kwa kupenda inabidi atolewe” IGP alikuwa anasikiliza kwa umakini sana hayo maelezo, alikunywa tena hiyo pombe mpaka alitokwa na machozi kwa namna pombe hiyo ilivyokuwa kali.

“Hii pombe inatakiwa kuinywa kwenye baridi ina joto kali sana, sasa vipi kama huyo mtu yupo miongoni mwetu mimi na wewe inakuwaje?” aliuliza wakati huu akiwa anamkazia macho CDF, CDF alimshangaa mtu huyo kwanini anampa hayo maelekezo

“Una maanisha nini?”
“Unajua wewe ni rafiki yangu tena zaidi hata ya rafiki tumeshakuwa ndugu tayari naomba uniambie ni kitu gani ambacho unanificha kwenye hii kesi ya jaji mkuu kuweza kuuawa?”

“Mhhhhhhhh kwahiyo una amini mimi naweza kukuficha nini kuhusu rafiki yangu mwenyewe, inamaanisha kwamba siku hizi hauniamini kiasi hicho ndugu yangu?”

“Wala sio hivyo hakuna sehemu hata moja ambayo nimesema sikuamini, unajua kwa kilicho tokea Mark kuweza kuuawa nyuma yake kuna mambo ya siri ambayo yanaendelea, baada ya lile tukio tuliipata simu yake ile simu niliipeleka kwa vijana wangu ili tuweze kujua kama labda kuna watu alikuwa ana matatizo nao kabla ya kupatwa na umauti, ni kweli ilikuwa hivyo kuna namba ilimtishia usiku mmoja kabla ya kesi kwamba kama akifanya kitu cha hovyo na kumhukumu yule mfungwa basi anauawa yeye na familia yake jambo ambalo liliendelea mpaka asubuhi kabla hajaingia kwenye chumba cha kusikilizia kesi na hata baada ya kutoka huko kuna sms ambayo ilimtaka aweze kufika kwake ndani ya dakika 15 ili aiokoe familia yake” alikohoa kidogo kisha akaendelea

“Lakini kwenye zile sms ambazo zilipatikana pale kuna sms ambayo kabla ya kuingia kwenye kesi ilitumwa muda mmoja na ile nyingine ya kumtisha na kumuahidi bilioni kumi lakini hata baada ya kutoka mle ndani kuna sms nyingine ambayo ilitumwa sambamba na ile sms tena, baada ya uchunguzi namba ambayo ilitumika ni ya kwako mwenyewe, baada ya kulijua hilo nikaamua kuchukua ushahidi wote huo na kuwapa vijana majukumu mengine, sasa nahitaji uniambie ukweli vipi unahusika kwenye hili jambo la kumuua Mark na kama ni kweli kwanini? Kuna nini mpaka ufikie hatua ya kumpunguza ndugu yetu?” maelezo na maswali mfululizo ambayo aliulizwa yalimfanya kwanza ainame kwa muda wa dakika tano kisha akanyanyua uso wake na kumwangalia IGP

“Siwezi kumuua mtu wa karibu kwangu kama yule, namuua kwa sababu ipi? Namuuaje rafiki yangu ambaye tumetoka kwenye sifuri naye pamoja? Mimi sipo kwa ajili ya kuua watu mimi nipo kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wa nchi hii wapo salama, mipaka ya nchi ipo salama na hata mheshimiwa raisi yupo salama sasa naanzaje kumuua Mark? Mimi nilifanya vile kwa sababu nilijua ile video italeta matatizo makubwa sana ndiyo maana nikamwambia asifanye yale maamuzi” alitulia baada ya kujibu, IGP alimwangalia sana rafiki yake kwa sababu alimpa majibu mepesi sana.

“Mimi sijajia hapa kwa sababu ya hilo jambo kama kutakuwa kuna umuhimu wa kuliongelea basi tutakutana mimi nawewe ila kama utanificha basi linaweza kuja kukuletea matatizo makubwa sana kwa sababu sasa halipo kwenye mikono yangu lipo kwenye mikono ya mtu mwingine ambaye naye kaahidi kulifuatilia mwenyewe”

“Mhhhhhh nani huyo?” swali lake lilimfanya IGP amwangalie sana mwenzake

“Jason”
“Ndo nani?”
“Wanadamu huwa tunabadilika sana hivyo sikushangai kusema humjui huyo kijana, nakukumbusha tu Mark udhaifu wake mkubwa ulikuwa unaujua?”

“Daaah nilikuwa mbali sana yule bwana mdogo si alikuwa kusoma?”
“Sasa ataendelea na masomo na **** msiba wa kaka yake?”
“Enhe sasa yeye anahusikaje na hili? Kwa sababu yeye kaahidiwa kusaidiwa kila kitu na serikali na hata sisi hatuwezi kumtupa tutampatia kila kitu ambacho yeye atakuwa anakihitaji”

“Sasa huyo ndiye ambaye amesema hili suala anaenda kulifuatilia kwa mkono wake mwenyewe”

“Inawezekanaje na vyombo vya usalama vipo? Anaanzia wapi yule ambaye haijui sheria hata kusema A inasemaje anaenda kumfuatilia nani zaidi atajiingiza kwenye matatizo tu hivyo hatutakiwi kabisa kuruhusu hilo jambo liweze kutokea, haiwezekani tusije kumpoteza kama kaka yake”

“Mhhhhhhh wewe ni mkuu wa majeshi ndiyo lakini una uhakika gani kwamba hiyo sheria haijui?”

“Yule mtoto nilikuwa nakutana naye mara chache sana muda mwingi huwa ni mtu wa kuzunguka nchi za watu kusoma huko sasa hiyo sheria anaijulia wapi na sijawahi kumsikia wakisema anasomea sheria, si anasomea uhandisi yule mtoto”

“Sasa huyo ndiye ambaye amenifanya nije hapa siku ya leo kukufuata na kama siyo yeye tusingekutana kwa wakati huu hapa” CDF alizidisha umakini ili aweze kuzipata habari hizo

“Anataka nini?”

“Kwenye maelezo yangu baada ya yeye kuhitaji taarifa za vifo vya wana familia wake kuna sehemu ambayo niliruka kuhusu sms zako na wala sikuhitaji kabisa kumhusisha kwa chochote kile alinikalia kimya tu mpaka nilipo mpeleka hospitali ya mhimbili Kwenda kuiona hiyo miili ya ndugu zake ndipo alipoweza kuniuliza hicho kitu nimeshtuka sana”

“Ameniuliza kwanini namdanganya kuhusu sms ambazo nilizikuta mle ndani, sijui amejuaje kama kuna sms mule nimezifuta ambazo ni zako lakini pia ameniuliza kwanini tumeruhusu mtu ambaye hahusiki kabisa na mauaji akauawa mbele ya mahakama maana yake ni kwamba tulitengeneza mtego ndugu yake afe”

“Umeniacha kidogo hapo ebu fafanua kiundani kidogo” CDF aliuliza kwa wasiwasi baada ya kuona kuna sehemu kama hajaelewa vizuri

“Ndugu zake wote wamekufa huku wakiwa wamepigwa risasi za kichwa kwenye paji la uso na hata raisi ilikuwa ni hivyo hivyo, kama raisi aliuawa na mtu ambaye wewe ulisema mlimkamata na akanyongwa mbele ya mahakama maana yake kama angekuwepo muuaji mwingine basi aina ya mauaji ingekuwa ni tofauti lakini cha ajabu hata ndugu zake wameuliwa vile vile tu kama raisi hapo inaonekana kabisa kwamba muuaji alikuwa ni mtu mmoja. Swali lake kwamba kama ni mtu mmoja ndiye anahusika maana yake ni kwamba aliye nyongwa mahakamani siyo mhusika ila mhusika yupo sasa kwanini tulimhukumu mtu ambaye siye mhusika? Ndugu yangu niwe muwazi tu hilo swali na uzee wangu huu limenishinda kabisa kulijibu hivyo alilazimika kuniuliza mtu aliye toa amri ya mtu huyo kukamatwa ikabidi nikutaje wewe kama ulivyokuwa umeamuru”

“Enhe kama ni hivyo kwahiyo yeye anataka iweje?”
“Anahitaji sana akutane nawewe ili wewe uje umjibu hayo maswali mwenyewe maana kuna vitu ambavyo kwa mimi vilikuwa nje ya uwezo wangu kwa sababu sivijui nadhani wewe una maelezo mengi zaidi, kuna makosa mengi sana ya wazi ambayo yamefanyika kwenye hii kesi naona kabisa huko mbeleni yanaenda kuleta matatizo makubwa sana”

“Huyo mtoto anajiona nani kwani mpaka aanze kutupelekesha namna hii kama ametuajiri yeye, inatakiwa asubiri mpaka pale nitakapo pata nafasi yangu ndipo naweza kumtafuta tukae naye”

“Amesema anataka leo na anakuja saa sita kamili usiku utamkuta nje ya geti lako na amesisitiza sana mkutane kwa sababu kama ukizidisha hata dakika moja humkuti huwa ni mtu wa kwenda na muda sana”

“Hivi ndiye huyu mtoto mdogo wake na Mark ambaye ndiye anatoa hizo amri au ni nani?”
“Ndiye huyo huyo”
“Kivipi yaani mpaka mtu na utu uzima wako unatii kila kitu kwa huyo mtoto”

“Ni mtoto sio?”
“Yes, wewe huoni kama ni mtoto mdogo yule hata kama kafiwa hata sisi yule ni rafiki yetu inatakiwa awe mpole asitupelekeshe”

“Sawa ni kwa sababu tu humjui ndiyo maana una hiyo jeuri ya kuongea hivyo ila nakusihi sana jitahidi sana msije kuingia kwenye mgogoro wowote ni vyema ukamsikiliza”

“Kamwambie nitamsikiliza pale nitakapo muita mimi”

“Hayo maneno utamwambia mwenyewe akija hapa kwako kwa mdomo wako”
“Huyo kijana kuna nini kwani upande wake mpaka unahaha hivyo IGP mzima kabisa”

“Ipo siku utakuja kumjua na ndipo utakuja kuyakumbuka maneno yangu, mimi naenda itakapo hitajika tutakutana tena”

Huyu Jason ni nani hasa mpaka IGP anaonekana anamuogopa sana mtoto laini kama yule?

Marafiki wawili hawa mazungumzo yao yaliishia sehemu mbaya kidogo ya kutokuwa na maelewano mazuri hata kidogo japo walianza vizuri hiyo ni kawaida kwenye maisha ya mwanadamu yeyote hakuna mtu ambaye atakuwa upande wake milele ukitoa wazazi wake hata ndugu wanaweza kutokomea na kuzipambania familia zao, ila wazazi usije ukawasahau kamwe hata kama walikukosea vipi as the saying goes Go EAST, GO WEST, HOME IS ALWAYS THE BEST.

Wasalaaam

Hatari sana
 
Tahadhali Kwa ambao hampendi alosto huyu hua hamaliza ko tusome ikifika mda akasema inaisha hapo msimtukane
 
Brother nina uhakika 100% bado haunifahamu ama umesoma hadithi moja tu pekee kutoka kwangu.

Kusema huwa simalizi nadhani umenikosea pakubwa sana unless kama unafanya jokes.

Nimeleta simulizi 4 hapa jf na hii ni ya 5.

1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA (Niliileta hapa mpaka mwisho)

2. NATAKA KUFA HAKIMU (niliileta mpaka mwisho)

3. HATIMA YA UJINGA WAKE (niliileta mpaka mwisho)

4. GEREZA LA HAZWA (Hii ndo haikuisha nadhani iliishia 96. Nikaja kuomba execuse hapa kwamba kuna watu wanahitaji niwatolee kitabu (nakala ngumu). So nikaomba tusiendelee kuisoma humu maana itakuwa haina maana mtu kaimaliza huku halafu tena anunue kitabu. Nakumbuka watu walikuja kudhihaki sana, sikumbuki kama ulikuwa mmoja wao

Wengine wakadai kama nataka kufanya biashara niende kwenye threads za biashara (sikumjibu mtu), wengine wakadai kwamba kama vipi modes waitoe tu na kweli ikatolewa) japo kuna watu walinielewa pia na baadae nilikuja kuamua kutaka kuiendeleza ila ikawa imetolewa.

5. INNOCENT KILLER (ndo hii tunaisoma hapa)

Hivi mkuu nikikwambia uthibitishe kauli yako kwa hayo maelezo ya hapo juu unaweza?

Nadhani ni wakati sahihi watu kujifunza COMMUNICATION SKILLS na kuachana na kutu kinaitwa MANIPULATION mkuu. Hapo mtu ambaye atakuwa anaanza kusoma kwa mara ya kwanza anaweza kuhisi kwamba ni kweli nipo hivyo kitu ambacho siyo sahihi.

NB
Hii nilisema nitakuwa naipost mara mbili kwa wiki kwa sababu mpaka sasa bado naiandika japo imefika mbali kidogo (sehemu ya 90). Nilifanya hivyo sikutaka tusome halafu tuje kustop njiani lakini huwa naileta zaidi ya mara mbili kwa wiki mpaka mara 4 na itakuwa zaidi muda unavyo zidi kwenda.

TUJIFUNZE KUZUIA HISIA MKUU JAPO NAKUELEWA maana hata mimi nimewahi kuwa msomaji kabla ya kuwa mwandishi.

Amani itawale japo nina imani huenda haukuongea kwa nia mbaya ila watu wengine wanaweza kuichukulia kwa namna tofauti, nadhani kikubwa ni kueleweshana tu, bado najifunza.

Baadae kidogo naweka mwendelezo hapa [emoji120]
 
Mkuu Hawa hawakujui mzigo lazima uishe sisi ni mashahidi
 
Back
Top Bottom