Instagram vs Reality

Instagram vs Reality

PRJ2012

Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
30
Reaction score
25
Mimi ni shabiki mkubwa sana wa kushop online. Mara nyingi ninapohitaji vitu kama nguo, begi hata viatu, naingia zangu mtandaoni nanunua chapchap mambo yanaenda.

Juzi kati hapa ndo nikaamini kuwa sio kinachong'aa ni dhahabu. Niliona kitu kwenye Instagram account moja kubwa tu kama kawaida yangu nikachukua namba nikamcheki muuzaji inbobo tukaelewana kila kitu na baada ya masaa mawili or so mzigo ukawa delivered kwangu.

Niliumia sana nilipofungua package yangu kwani kile nilichokiona na kile kilichokuwa Instagram ni vitu viwili tofauti. Bidhaa ilikuwa imechoka, quality yake mbovu na ukiangalia nilishalipia kila kitu.

Swali langu: Kwanini wafanyabiashara wa mtandaoni wanafanya hivi? Hawaoni kama wanaharibu? Huu ni utapeli jamani na biashara haziendi hivyo.

Badilikeni ndugu zangu!
CCFBD984-2FD8-4927-8CA6-FAC9087D7F59.jpeg
 
Back
Top Bottom