Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Barua hii ya tarehe 20 Septemba 2024 inayotajwa kupelekwa polisi mikoa ya Ilala na Kinondoni ni dhahiri imeonesha namna chama hiko wanavyozichanga vyema karata kuelekea maandamano ya 23 Septemba 2024.
Tumeshuhudia mrundikano wa polisi kutoka mikoani kuletwa Dar kudhibiti maandamano haya matukufu. Hivyo suala la availability ya polisi ni zaidi ya KIWANGO ndani ya Dar kwa sasa.
Kosa zuri la kiufundi walilofanya mamlaka na polisi ni kuyaangalia haya maandamano kama tishio la amani yao ya kuendesha operesheni ya utekaji nyara na mauaji kwa raia. Hivyo wakajipanga kuyadhibiti kwa kuleta askari wengi kutokamikoa yote TZ waje Dar na kuwaacha maaskari wachache mikoani. Tumeona silaha zikiingizwa kuimaria nia ovu ya kutaka kuwadhuru waandamanaji kwa kigezo cha kulinda amani.
Good timing ni kwamba, askari wapo na hakuna sababu ya kuharamisha maandamano kwa sababu askari Dar wapo wa kutosha kulinda na kusindikiza maandamano haya ya amani. Hivyo geti kubwa la kwanza kuelekea maandamano ya 23 Septemba limeshavukwa na sasa lango la pili ni maandamano kufanyika kama yalivyopangwa na kila mpenda haki ajitokeze kuunga mkono maandamano yanayotetea HAKI YA KUISHI kwa Watanzania wote.
TUkutane kwenye maandamano.
SAMIA MUST GO
Erythrocyte Mshana Jr Retired Tlaatlaah Lucas Mwashambwa Earthmover chiembe Pascal Mayalla Mzee Kigogo Mzee Mwanakijiji Jambazi Mdude_Nyagali NAPENDA NCHI YANGU Mama Amon Depal