Intelijensia ya Tanzania imekwenda likizo au imekufa?!

Intelijensia ya Tanzania imekwenda likizo au imekufa?!

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Ni jambo la kustaajabisha sana kuwa intelijensia ya Tanzania ilishindwa kubaini kutokea kwa ghasia kubwa za Mtwara!

Kumetokea nini ndani ya taasisi hiyo nyeti:
  1. Kukosekana kwa weledi?
  2. Kuwapuuza wananchi wa Mtwara?
  3. Kupuuza maoni na madai ya wana-Mtwara?
  4. Kutowajibika kwa kufanya kazi zisizowahusu wala zinazoshahibiana na ujuzi wao?
  5. Kukosa uzalendo? au
  6. Wameichoka serikali iliyopo madarakani?!
 
...intelijensia ya taasisi ipi mkuu,TISS, POLISI, JWTZ n.k, in any case vyombo hivi nahisi vina compromise na interest za viongozi wake....
 
Hiki kitengo kilishafutwa miaka miiingi
Sasa hivi kuna wapiga dili tu
 
mkuu Ileje,nakusihi usiwalaumu hao jamaa kwani wameagizwa kuelekeza nguvu zao kwa chadema na waandishi wanaoikosoa serekali ya ccm
 
Last edited by a moderator:
...intelijensia ya taasisi ipi mkuu,TISS, POLISI, JWTZ n.k, in any case vyombo hivi nahisi vina compromise na interest za viongozi wake....
Intelijensia kwa mapana yake yote kwa kuwa mwisho wa siku ni kuhakikisha nchi ina amani, rasilimali zake hazifisadiwi na watanzania wote wanatimiza wajibu wao katika nyanja mbalimbali!
 
Wakimwambia hasiki, anasema ni upepo tu utapita, So wameamua liwalo na liwe
 
Wakimwambia hasiki, anasema ni upepo tu utapita, So wameamua liwalo na liwe
Mara zote ushauri wa kitaalamu ukipuuzwa madhara yake ni kama haya!
 
Nadhani hata nyie MODS mmechangayikiwa! Uzi huu unajadili siasa za Mtwara!
 
mmmh hata sina jibu ila ngoja nipitie pitie maoni ya wengine naweza pat majibu mazuri zaidi aisee....
 
inamaanisha Usalama wa taifa wanazidiwa akili na wanasiasa,au kwa maana nyingine watu walioko kwenye idara hiyo ni vilaza(tiss) ambao wanawaongozwa na maitelejensia(wanasiasa)
 
Ni jambo la kustaajabisha sana kuwa intelijensia ya Tanzania ilishindwa kubaini kutokea kwa ghasia kubwa za Mtwara!

Kumetokea nini ndani ya taasisi hiyo nyeti:
  1. Kukosekana kwa weledi?
  2. Kuwapuuza wananchi wa Mtwara?
  3. Kupuuza maoni na madai ya wana-Mtwara?
  4. Kutowajibika kwa kufanya kazi zisizowahusu wala zinazoshahibiana na ujuzi wao?
  5. Kukosa uzalendo? au
  6. Wameichoka serikali iliyopo madarakani?!

Mimi nina mtazamo tofauti kidogo. Labda kama sina taarifa rasmi lakini sidhani kama kuna taarifa rasmi kuwa usalama wamekiri kutobainika au kubaini vurugu za mtwala. Ifike muda tujue utendaji kazi wa hawa wenzetu hauko wazi kivile kwamba leo Ileje au Mkubya atajua kila lililofanyika. Sidhani kama huwa taarifa zao wanaziripoti katika umma isipokuwa kwa mamlaka husika. kama jambo linahitaji JWTZ kutaarifiwa, then taarifa watapewa wao, kama ni mambo ya ndani then mamlaka husika watapewa taarifa na ushauri wa nini kifanyike. sasa kutokea kwa vurugu au kutotokea sidhani kama kuna-justify nukuu yako hapo.

Bado naamini hawa watu wanafanya kazi kubwa sana ambayo kwa raia wa kawaida kufahamu yanayojiri nchi hii ni vigumu sana. Hivyo basi, tusitoe lawama tukiegemea katika nyanja ya kisiasa zaidi. Sidhani kama wanaripoti kwa rais wa nchi then kila wanalosikia watali-publish kwa umma. narudia tena, sijui mfumo wa utendaji wao hasa katika kutoa taarifa lakini nina imani wanafanya kazi kubwa sana ambazo hatupaswi kuwapuuza. Pia ifike muda hiki chombo kipewe hadhi yake stahiki, ni chombo muhimu sana kwa ustawi wa nchi lakini sisi kila leo ni kukikosoa na kuto-appreciate hata mazuri wanayofanya ambayo pia nina hakika mtoa mada anaweza asiwe na ufahamu kuwa TISS wamefanya hili na hili for this year ambalo wanapaswa kupongezwa. tusiwakatishe tamaa, kama mtu ana ushauri atoe kwao lakini muda wa lawama kwa sasa haujengi. huo ni mtazamo wangu.
 
Kumbuka kuwa hawa watu ndiyo mboni ya serikali! Hivyo kama serikali inashindwa kufanyia kazi taarifa zao basi huu ni udhaifu mkubwa ambao hauvumiliki!

Kwa nafasi yao wanaweza hata kufanya jitihada za kuiondoa serikali hii kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kulishawishi bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na serikali!

Kwa kifupi naweza kufupisha mawazo yako kuwa unasema "SERIKALI HII NI DHAIFU"!
 
intelijensia huwa inafanya kazi wakati wa maandamano ya chadema, aibu yao
 
Kumbuka kuwa hawa watu ndiyo mboni ya serikali! Hivyo kama serikali inashindwa kufanyia kazi taarifa zao basi huu ni udhaifu mkubwa ambao hauvumiliki!

Kwa nafasi yao wanaweza hata kufanya jitihada za kuiondoa serikali hii kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kulishawishi bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na serikali!

Kwa kifupi naweza kufupisha mawazo yako kuwa unasema "SERIKALI HII NI DHAIFU"!

Najua ni watu muhimu sana kwa taifa lolote lile, si Tanzania tu. Lakini tuangalie utendaji kazi wao pia. je TISS wanafanya kazi kwa mfumo gani? Mimi sio mwanasheria hivyo kama nitatafsiri vibaya naomba radhi but TISS Act ya Mwaka 1996 ilosainiwa 20 January 1997, inabainisha baadhi ya mambo yafuatayo;

(PART II
................
5.-(1) Subject to the control of the Minister, the functions of the Functions
Service shall be- of TISS
(a) to obtain, correlate, and evaluate intelligence relevant to security,
and to communicate any such intelligence to the Minister and to
persons whom, and in the manner which, the Director-General
considers it to be in the interests of security;
(b) to advise Ministers, where the Director-General is satisfied that
it is necessary to do so, in respect of matters -relevant to security,
so far as those matters relate to departments or portfolios of
which they are in charge;
(c) to cooperate as far as practicable and necessary with such other
organs of state and public authorities within or outside Tanzania
as are capable of assisting the Service in the performance of its
functions.
(d) to inform the President, and any other person or authority which
the Minister may so direct, of any new area of potential espionage,
sabotage, terrorism or subversion in respect of which the Director-
General has considered it necessary to institute surveillance.

(2) It shall not be a function of the Service-
(a) to enforce measures for security; or
(b) to institute surveillance of any person or category of persons by
reason only of his or their involvement in lawful protest, or dissent
in respect of any matter affecting the Constitution, the laws or
the Government of Tanzania)

Sasa katika hayo hapo juu, tuangalie ni haki kuwanyooshea kidole moja kwa moja kama kazi yao (rejea 5 (1) d hapo juu!!! Pia rejea 2 (a) and (b). Narejea pendekezo langu, hii taasis ni nyeti na nzito, hatupaswi kuibeza kwa namna yoyote ile ilhali hata report anapewa waziri au rais au mamlaka husika tu na sio kwingineko. waweza kudhani haifanyi kazi lakini sitaki kuamini hilo.
 
TISS inaendeshwa kwa interest za watu fulani!!!
 
bado wanafanya kazi sema saivi wapo upande wa ccm
 
Kama viashiria vya kutokea kwa fujo vilikuwepo mapema(vipeperushi na sms kama alivyokiri waziri husika bungeni), kwanini hazikufanyika juhudi za kuzuia,badala yake wanajikita kupiga mabomu na kusababisha vifo!
 
Back
Top Bottom