Intelijensia ya Tanzania imekwenda likizo au imekufa?!

Intelijensia ya Tanzania imekwenda likizo au imekufa?!

Ukifuatilia mjadala huu, mambo mengi yameelezwa, kuna waliojaribu kuelezea areas of weakness na nini kifanyike. Hii ndio nayopenda mimi, kwamba bila kum-attack mtu, tuseme japo areas of weakness 3 tu, na way foward. Mfano, "area of weakness ni link ya kitengo na utawala wa wajumbe wa nyumba kumi"; kwanini? nini kifanyike? kwa sasa tusiendelee kurumbana, mtu atoe breakpoint ni wapi na suruhisho lake, kwa kutaja taasis and not a person.

Mjumbe wa Nyumba kumi ndiye alikuwa afisa usalama wa taifa namba moja, akisaidiwa wa mgambo wa kijiji. Chama kilijua nani ana uzalendo wa kutosha kuwa mjumbe wa nyumba kumi. Uzalendo hauna siri. Tuna vyama vingi sasa. Hivi vyama vinawajua wanachama wao. Vitajua nani ana uzalendo tosha kupewa nafasi ya mjumbe wa nyumba kumi. Tuanzie hapo na uhalifu wa aina nyingi sana utapungua sana kama si kuisha kabisa.
 
Kwani wana Intellijensia wao malaika au mungu mpaka wajue yaliyomo kwenye kichwa cha kila mtu?
 
Najua ni watu muhimu sana kwa taifa lolote lile, si Tanzania tu. Lakini tuangalie utendaji kazi wao pia. je TISS wanafanya kazi kwa mfumo gani? Mimi sio mwanasheria hivyo kama nitatafsiri vibaya naomba radhi but TISS Act ya Mwaka 1996 ilosainiwa 20 January 1997, inabainisha baadhi ya mambo yafuatayo;

(PART II
................
5.-(1) Subject to the control of the Minister, the functions of the Functions
Service shall be- of TISS
(a) to obtain, correlate, and evaluate intelligence relevant to security,
and to communicate any such intelligence to the Minister and to
persons whom, and in the manner which, the Director-General
considers it to be in the interests of security;
(b) to advise Ministers, where the Director-General is satisfied that
it is necessary to do so, in respect of matters -relevant to security,
so far as those matters relate to departments or portfolios of
which they are in charge;
(c) to cooperate as far as practicable and necessary with such other
organs of state and public authorities within or outside Tanzania
as are capable of assisting the Service in the performance of its
functions.
(d) to inform the President, and any other person or authority which
the Minister may so direct, of any new area of potential espionage,
sabotage, terrorism or subversion in respect of which the Director-
General has considered it necessary to institute surveillance.

(2) It shall not be a function of the Service-
(a) to enforce measures for security; or
(b) to institute surveillance of any person or category of persons by
reason only of his or their involvement in lawful protest, or dissent
in respect of any matter affecting the Constitution, the laws or
the Government of Tanzania)

Sasa katika hayo hapo juu, tuangalie ni haki kuwanyooshea kidole moja kwa moja kama kazi yao (rejea 5 (1) d hapo juu!!! Pia rejea 2 (a) and (b). Narejea pendekezo langu, hii taasis ni nyeti na nzito, hatupaswi kuibeza kwa namna yoyote ile ilhali hata report anapewa waziri au rais au mamlaka husika tu na sio kwingineko. waweza kudhani haifanyi kazi lakini sitaki kuamini hilo.

Wewe brother una maneno mengi sana yasiyo na tija. Ukweli ni kwamba kunawalakini katika utendaji kutokana na mambo yanavyoenda. Kuleta quotes hakuna tija ni vizuri vyombo vyetu vya usalama vichukue nafasi hii kujitazama upya au kujirekebisha pale penye mapungufu. Kwa mfano wewe unasema vurugu za mtwara zimechochewa na foreign agents/interests.

  • what did they do to prevent foreign agencies to instigate such chaos if at all it is true?
  • Can foreign agencies/companies perpetuate such a plot in a day/seven month period?
  • When did they know about such plots against our interests? what did they do to fight against them?
  • What do they do to protect our interests in Gas contracts and the like?
  • why grand schemes go un-prevented well in advance?
  • why do they deal with postmortem issues of economic sabotage while they have first-hand information during perpetuation by the greed-people? why, why?!
  • In my opinion, they are not doing enough on prevention that is why most scandals are uncovered while damage is done and little to be saved.
No wonder after implementation of gas projects ukaambiwa mikata ya gesi inamapungufu makubwa yenye kufifisha maslai ya Taifa. Hapa ndiyo watu wanajaribu kutoa tahadhari yasijetokea mengine kwani ya madini yametokea wakati vyombo vyetu vya usalama vikiwepo bila kuzuwia! They need to be preventive rather than detective because contracts take long time to be prepared for them to see and cushion our interest. Intil. agencies are not always supported to be reactive. Kelele hizi wasichukulie kama wanazalilisha bali changamoto ya kuweka maslai ya nchi mbele kuliko mengine yote kwani Tanzania itakuwepo kwa miaka mingi kuliko sisi sote.

Mungu ibariki Tanzania!
 
Ile act. iliowapa ufizi (sio meno) mijamaa ya TISS imewaambia wagundue na washauri kitaalam ha ha ha ha ha!!
Kinachonichekesha wakuu ushauri ni ushauri tu hata uwe wa kitaalamu unaweza kupigwa na chini na anaeshauriwa
 
Totos Boss, nadhani wewe act ile umeisoma vzr na hiki ndicho nilikua nasema kuwa hatuna hakika ya kusema wamelala. Kwamba limitations walizopewa ni kutoa ushauri wa kitaalam tu, actions zitachukuliwa na waliopewa ushauri. Sasa ufanyiwe kazi au upigwe chini hilo ni jambo lingine na kwa vile ushauri wao hawauweki katika media, wananchi ndio hapo wanapata courage ya kuwanyooshea vidole kuwa hawafanyi kazi yao ipasavyo but hatujui nyuma ya pazia kilichojiri.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Tuweke nguvu za kutosha katika kuiboresha zaidi rasimu ya katiba, hatimaye ipitishwe ili iweze kusaidia katika kuondoa matatizo na changamoto zinazotukabili. Kwa maoni yangu, ni vyema mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama yakaboreshwa zaidi, ili kuvipa vyombo hivyo Mamlaka na Uwezo wa kutekeleza Majukumu Yao kwa Weledi na Ufanisi zaidi.
 
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo. Labda kama sina taarifa rasmi lakini sidhani kama kuna taarifa rasmi kuwa usalama wamekiri kutobainika au kubaini vurugu za mtwala. Ifike muda tujue utendaji kazi wa hawa wenzetu hauko wazi kivile kwamba leo Ileje au Mkubya atajua kila lililofanyika. Sidhani kama huwa taarifa zao wanaziripoti katika umma isipokuwa kwa mamlaka husika. kama jambo linahitaji JWTZ kutaarifiwa, then taarifa watapewa wao, kama ni mambo ya ndani then mamlaka husika watapewa taarifa na ushauri wa nini kifanyike. sasa kutokea kwa vurugu au kutotokea sidhani kama kuna-justify nukuu yako hapo.

Bado naamini hawa watu wanafanya kazi kubwa sana ambayo kwa raia wa kawaida kufahamu yanayojiri nchi hii ni vigumu sana. Hivyo basi, tusitoe lawama tukiegemea katika nyanja ya kisiasa zaidi. Sidhani kama wanaripoti kwa rais wa nchi then kila wanalosikia watali-publish kwa umma. narudia tena, sijui mfumo wa utendaji wao hasa katika kutoa taarifa lakini nina imani wanafanya kazi kubwa sana ambazo hatupaswi kuwapuuza. Pia ifike muda hiki chombo kipewe hadhi yake stahiki, ni chombo muhimu sana kwa ustawi wa nchi lakini sisi kila leo ni kukikosoa na kuto-appreciate hata mazuri wanayofanya ambayo pia nina hakika mtoa mada anaweza asiwe na ufahamu kuwa TISS wamefanya hili na hili for this year ambalo wanapaswa kupongezwa. tusiwakatishe tamaa, kama mtu ana ushauri atoe kwao lakini muda wa lawama kwa sasa haujengi. huo ni mtazamo wangu.

Maelezo yako ni sahihi na ukweli mtupu. Mtu anatoa lawama tu, kuwapuuza watendaji wa TISS, kuwakejeli, wakati hajui operations zao ,hajui wamefanya nini kumuweka salama hata akawa na uhuru wa ku post humu JF... Kwakweli inasikitisha sana. siku hizi watanzania, baadhi, wamekuwa ni watu wa kuilaumu na kuipuuza na kuikejeli TISS kila kunapotokea jambo ambalo halijawafurahisha. nadhani huu sio utamaduni mzuri, unapaswa kuachwa. Do you really know their SUCCESSES AND FAILURES??? How do you assess them if you do not know???? This is the million dollar question to all critics.
 
Nataka kujiaminisha kuwa wewe ni mmoja wa watendaji wa TISS kwa namna unavyokuja na hoja ya kuwatetea!

Kwa taarifa yako watendaji wa TISS wanafahamika na ofisi zao zinafahamika! Tunaishi nao mitaani na tunayajua vizuri maadili ya baadhi ya watendaji kwa kuwa tunakula nao, tunakunywa nao na tunacheza nao!

Taaluma ya TISS haijaanza leo, ipo tangu tunapata uhuru na tunajua utendaji wao wa kazi! Tunalinganisha wale wa kale na hawa wa leo na kupima uzalendo wao! Tunawaona wengine wanavyofanya biashara za kifisadi kiuwazi bila kificho lakini hawachukuliwi hatua!! Ndiyo sababu wengine wanatuhumiwa waziwazi katika vyombo vya habari kwa majina! Simu zao zinafahamika na hata wewe unaweza kumpigia sasa hivi kwa kuwa zimeorodheshwa! Mambo haya hayahitaji utaalamu mkubwa sana wa ki-TISS!

So my friend there are general indicators to measure their perfomance!
 
Eti general indicators! Wewe unajua TISS ina watumishi wangapi? hao unaokunywa nao na kula nao unajua kazi zao wakati hawako katika upeo wa macho yako? au unadhani kunywa na mtu au kucheza nae pool basi ndio tayari umeijua TISS yote na watendaji wake wote na ueledi wao kiutendaji? poor analysis and very biased! Nw kujua ofisi za TISS kunakufanya uijue TISS???? Unazijua ofisi zao wewe? Au unakalia tu porojo za mitaani na propaganda. I am sure 100% huna unalolijua kuhusu kazi za TISS, mafanikio yao na mapungufu yao kiutendaji hadi uweze kuwaweka kwenye mzani kuwapima na kuwa Rate! So wewe endelea tu na post zako humu JF kujifurahisha nafsi yako. Huna unalolijua... Kama namba zao zimechapishwa kwenye magazeti wapigie basi halafu wakuelekeze ofisini kwao ili uende mkajadili mapungufu unayoyasema na kisha uwashauri cha kufanya. Au nenda kwenye hizo ofisi zao unazosema unazijua then waeleze mapungufu hayo unayosema may be watajirekebisha au watakuajiri wewe mjuaji ufanye hizo kazi za kiusalama.
 
Maelezo yako ni sahihi na ukweli mtupu. Mtu anatoa lawama tu, kuwapuuza watendaji wa TISS, kuwakejeli, wakati hajui operations zao ,hajui wamefanya nini kumuweka salama hata akawa na uhuru wa ku post humu JF... Kwakweli inasikitisha sana. siku hizi watanzania, baadhi, wamekuwa ni watu wa kuilaumu na kuipuuza na kuikejeli TISS kila kunapotokea jambo ambalo halijawafurahisha. nadhani huu sio utamaduni mzuri, unapaswa kuachwa. Do you really know their SUCCESSES AND FAILURES??? How do you assess them if you do not know???? This is the million dollar question to all critics.

Asante Metsada, nadhani wengi hatujui mfumo wao wa kazi ndio maana yote haya yanatokea na sijui kama kuna mfumo wa kutoa elimu hiyo na je pia ni sahihi kutoa elimu hiyo kwa watanzania walio wengi ili hii negative altitude iondoke. Ifike stage ambayo Ileje akiwa na vital information from any source basi aende ktk hizo ofisi zao anazozijua akawape briefing. Hili gap lililojegwa kwa wananchi waliowengi kwamba TISS haifanyi kazi zake liondoke ili hao watanzania wawe pia source of information.

Hizi siasa pia kuachwa kuongelea mpaka mambo ya ndani kabisa yaliyo nyeti tupunguze. Wanasiasa na intelligence agents wa nchi zingine wanachukua mambo mengi sana humu JF, mfano ile shutuma ya wanyarwanda kuhusu rais wa Tz, wame site JF kama source yao kama niliisoma vzr. Anyway, nachosema ni umakini wa information tunazotoa na pia utaifa, chochote kikitokea ni Tz nzima na sio chama cha siasa au tiss au polisi, tuwakosoe katika kuwajenga na si kuwakatisha tamaa.
 
CCM yajifua kijeshi Mbeya

Yadaiwa kuunda kambi kwa maagizo ya Mwigulu

na Christopher Nyenyembe, Mbeya

HOFU ya vitendo vya kijangili imezuka mkoani hapa baada ya kuwepo kwa tuhuma za kambi tatu zinazoendesha mafunzo ya kijeshi, zikidaiwa kuendeshwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tuhuma hizi nzito zilizotolewa na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, zimedai kuwa kambi hizo zimeanzishwa kutokana na agizo la Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.

Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija alisema kuwa kambi hizo zimewekwa katika shule tatu za sekondari zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM ambako vijana wa chama hicho wanapatiwa mafunzo ya kijeshi.

Mwambigija alisema kambi hizo zilizoko Ivumwe, Itende na Igawilo, zinaendesha mafunzo hayo huku vijana wakisikika wakitamka maneno ya ‘kata kucha’, ‘ng’oa meno’, ‘ingiza chupa’ na mengine yanayotishia usalama wa watu.

“Tumepata taarifa kuwa vijana hao wanatekeleza maagizo yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba. Vijana hao wapo Ivumwe, Itende na Igawilo, wanatamka maneno hatarishi, wakiimba, kata kucha, ng’oa meno, ingiza chupa na mengine hatuwezi kuyataja, ni hatarishi sana,” alisema Mwambigija.

Mwenyekiti huyo alisema wamegundua kuwa hatua hiyo inalenga pia kuwatisha wananchi wasijitokeze katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Iyela jijini Mbeya unaotarajiwa kufanyika Juni 16.

“Baada ya kufuatilia tumeona mwenendo wa mazoezi hayo una lengo la kuwatisha wapiga kura na kuwafanya wananchi waogope kujitokeza siku ya kupiga kura.

“CHADEMA tunataka kuona uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki, na CCM walipewa muda wa kufanya kampeni, hawajafanya kiasi cha kutosha, kwa hali hiyo wasitumie mbinu nyingine ili kuvuruga uchaguzi,” alisema.

Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Kanda ya Nyanda za Juu, Lucas Mwampiki ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA Mbeya Mjini, alisema kwa kutumia mbinu za kiintelijensia walifika zilipo kambi hizo kushuhudia hamasa na mafunzo waliyokuwa wakipewa vijana hao.

“Mafunzo na matamshi wanayopatiwa vijana hao hayana sura ya uzalendo, na sijawahi kuona wala kusikia chama kikongwe kikiwafundisha vijana wake maneno hatarishi.

“Sisi tumetekeleza wajibu wetu baada ya kugundua kuwa kambi za wenzetu hazina lengo zuri na uchaguzi huu. Nimeongea na RPC, RCO RSO na CID na viongozi wetu wa chama ngazi ya juu ili kuwajulisha kile kinachoweza kutokea,” alisema Mwampiki.

Baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya wilaya walipohojiwa kuhusu kuwepo kwa kambi hizo, hususan muda huu wa kampeni za udiwani, walikiri na kusema wanatekeleza maagizo ya Mwigulu.

Wakiongea kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, viongozi wawili wa CCM walisema kuwa wanajua maelekezo yaliyotolewa kuhusu mafunzo katika kambi hizo, lakini wakasema anayetakiwa kuzungumza ni Mwigulu mwenyewe.

“Kambi zipo, lakini kwangu binafsi sielewi vijana waliowekwa kambini wanafundishwa nini, maana huko sijafika bado,” alisema mmoja wa viongozi hao.

Alipotafutwa kwa njia ya simu, Mwigulu hakuweza kupatikana kwa vile simu yake ilikuwa imezimwa wakati wote. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, bado ilionekana haijafunguliwa.

Aidha, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Boyd Mwabulanga, alisema kuwa tangu kampeni zilipoanza wamegundua kuwepo kwa vitendo visivyoridhisha ikiwemo mbinu za kughushi shahada za kupigia kura.

Mwabulanga alisema kuwa wanawaomba wenzao CCM kuacha kutumia mbinu chafu zenye lengo la kuwaogopesha wananchi na mikakati iliyoandaliwa ya kutumia vyombo vya dola ikiwemo kupiga mabomu ya machozi ili watu waogope na kushindwa kujitokeza siku ya upigaji kura.

Kadhalika, alisema kuna tuhuma kwamba CCM wameanza mbinu chafu za kughushi shahada za kupigia kura maeneo ya Kabwe jijini Mbeya na kumtaja mtu mwenye mashine inayotumika kughushi.

Pia alisema kuwa baadhi ya wajumbe wa nyumba kumi kumi (mabalozi) wa CCM wamenaswa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama, lakini siku ya pili wameshangaa kuwaona wakitamba mitaani hali ambayo inazidisha kiburi na kuonyesha dhahiri CCM wanavyotegemea polisi.

Kauli ya RPC

Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Mbeya, Diwani amekiri kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa uongozi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, na kudai kuwa wanafuatilia suala hilo.

“Tumepata habari hizo na tunafuatilia kwa njia na mbinu zetu, na hadi sasa tunajua kuna mafunzo ya vijana wa CCM yanaendelea,” alisema Kamanda Diwani.

Hata hivyo, Kamanda Diwani alidai kuwa wanachojua ni kuwepo kwa mafunzo ya kawaida kwa vijana wa CCM, na ndiyo maana yanafanyika ndani na kwamba hayahatarishi amani na usalama.

“Lakini bado tunawaomba CHADEMA watusaidie kufuatilia na kama watagundua tofauti na haya tunayoyajua hadi sasa, watuarifu. Kwa sasa hatuwezi kumkamata yeyote kama wanavyotaka tufanye,” alisema.

Tuhuma hizo zinakuja kukiwa na taarifa za kuvamiwa na kujeruhiwa vibaya kwa makada wa CHADEMA mkoani Arusha kunakohusishwa na kampeni za uchaguzi.

Mapema wiki hii, kundi la vijana wanaoaminika kuwa wafuasi wa CCM walivamia mkutano wa CHADEMA na kuwajeruhi vibaya baadhi ya watu, jambo lililosababisha kuzuka kwa ghasia kubwa.
 
Eti general indicators! Wewe unajua TISS ina watumishi wangapi? hao unaokunywa nao na kula nao unajua kazi zao wakati hawako katika upeo wa macho yako? au unadhani kunywa na mtu au kucheza nae pool basi ndio tayari umeijua TISS yote na watendaji wake wote na ueledi wao kiutendaji? poor analysis and very biased! Nw kujua ofisi za TISS kunakufanya uijue TISS???? Unazijua ofisi zao wewe? Au unakalia tu porojo za mitaani na propaganda. I am sure 100% huna unalolijua kuhusu kazi za TISS, mafanikio yao na mapungufu yao kiutendaji hadi uweze kuwaweka kwenye mzani kuwapima na kuwa Rate! So wewe endelea tu na post zako humu JF kujifurahisha nafsi yako. Huna unalolijua... Kama namba zao zimechapishwa kwenye magazeti wapigie basi halafu wakuelekeze ofisini kwao ili uende mkajadili mapungufu unayoyasema na kisha uwashauri cha kufanya. Au nenda kwenye hizo ofisi zao unazosema unazijua then waeleze mapungufu hayo unayosema may be watajirekebisha au watakuajiri wewe mjuaji ufanye hizo kazi za kiusalama.
Ndugu yangu hapa hatugombani bali tunajadili kwa hoja!
  • Kwamba TISS ina watumishi wangapi, siyo hoja na wala sihitaji kujua idadi yao!
  • Wala sihitaji kujua kazi wanazofanya wanapokuwa mbali na upeo wa macho yangu, bali nahitaji kuona matokeo ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kudhibitimambo yote yanayohatarisha usalama wa taifa!
  • Sijadai kuijua TISS lakini nahoji weledi wao kutokana na matukio hatarishi yanayojitokeza wazi wazi kama mihadhara ya dini na video zinazosambazwa bila kudhibitiwa!
  • Swala la kuzijua ofisi za TISS ni muhimu sana na jambo hili tumewahi kuambiwa na Ofisa usalama wa mkoa mmoja ambaye hivi sasa amestaafu, kwamba ni muhimu kuzifahamu ofisi hizo pamoja na maofisa waandamizi wa ofisi hizo ili kuwapa taarifa zo zote ambazo unadhani zinahatarisha usalama. Ndiyo sababu sasa hivi ni sera ya usalama wa taifa kwa viongozi wote waandamizi kujitambulisha kwa wananchi!
  • Mimi nazifahamu ofisi za usalama wa taifa za mikoa yote niliyoishi na hata ofisi ya TISS makao makuu ya taifa naifahamu na naweza kukupeleka kama itahitaji!
  • Nami nina hakika kwa 100% kuwa hujui upeo wangu wa kuielewa TISS, hivyo kinachokutoa povu hapo ni propaganda zako zisizo na mbele wala nyuma na porojo tu!
  • Napenda kukufahamisha kuwa JF ni mtandao wa kijamii ambao unatuwezesha kujadili hoja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii nk na pia ni moja ya njia ya kuwasilisha maoni yetu kwa serikali, viongozi mbalimbali wa taasisi zikiwemo za binafsi, dini nk. Nina hakika hata watendaji wa TISS wanapata habari hapa!
  • Mwisho sihitaji ajira TISS kwani nina ajira ambayo naipenda sana lakini pia sijazuiwa kuwapa taarifa TISS kwani nawafahamu baadhi yao na ofisi zao pia!
​Nahitimisha kwa kukushauri kujifunza kujadili hoja na siyo kufoka!
 
Ni jambo la kustaajabisha sana kuwa intelijensia ya Tanzania ilishindwa kubaini kutokea kwa ghasia kubwa za Mtwara!

Kumetokea nini ndani ya taasisi hiyo nyeti:
  1. Kukosekana kwa weledi?
  2. Kuwapuuza wananchi wa Mtwara?
  3. Kupuuza maoni na madai ya wana-Mtwara?
  4. Kutowajibika kwa kufanya kazi zisizowahusu wala zinazoshahibiana na ujuzi wao?
  5. Kukosa uzalendo? au
  6. Wameichoka serikali iliyopo madarakani?!

Wanazamishana kwenye visima/mabwawa ya maji.
 
Ndugu yangu hapa hatugombani bali tunajadili kwa hoja!
  • Kwamba TISS ina watumishi wangapi, siyo hoja na wala sihitaji kujua idadi yao!
  • Wala sihitaji kujua kazi wanazofanya wanapokuwa mbali na upeo wa macho yangu, bali nahitaji kuona matokeo ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kudhibitimambo yote yanayohatarisha usalama wa taifa!
  • Sijadai kuijua TISS lakini nahoji weledi wao kutokana na matukio hatarishi yanayojitokeza wazi wazi kama mihadhara ya dini na video zinazosambazwa bila kudhibitiwa!
  • Swala la kuzijua ofisi za TISS ni muhimu sana na jambo hili tumewahi kuambiwa na Ofisa usalama wa mkoa mmoja ambaye hivi sasa amestaafu, kwamba ni muhimu kuzifahamu ofisi hizo pamoja na maofisa waandamizi wa ofisi hizo ili kuwapa taarifa zo zote ambazo unadhani zinahatarisha usalama. Ndiyo sababu sasa hivi ni sera ya usalama wa taifa kwa viongozi wote waandamizi kujitambulisha kwa wananchi!
  • Mimi nazifahamu ofisi za usalama wa taifa za mikoa yote niliyoishi na hata ofisi ya TISS makao makuu ya taifa naifahamu na naweza kukupeleka kama itahitaji!
  • Nami nina hakika kwa 100% kuwa hujui upeo wangu wa kuielewa TISS, hivyo kinachokutoa povu hapo ni propaganda zako zisizo na mbele wala nyuma na porojo tu!
  • Napenda kukufahamisha kuwa JF ni mtandao wa kijamii ambao unatuwezesha kujadili hoja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii nk na pia ni moja ya njia ya kuwasilisha maoni yetu kwa serikali, viongozi mbalimbali wa taasisi zikiwemo za binafsi, dini nk. Nina hakika hata watendaji wa TISS wanapata habari hapa!
  • Mwisho sihitaji ajira TISS kwani nina ajira ambayo naipenda sana lakini pia sijazuiwa kuwapa taarifa TISS kwani nawafahamu baadhi yao na ofisi zao pia!
​Nahitimisha kwa kukushauri kujifunza kujadili hoja na siyo kufoka!

Tatizo lako unakosoa sana kana kwamba unajua utendaji wa TISS. Endapo ungekuwa unajua ni operations zipi wamefanikiwa na wapi wamekwama then ndio unaweza kukosoa na kuwa rate katika mzani. Ila sio mbaya, una uhuru wa kikatiba kutoa maoni yako, so endelea tu.
 
Back
Top Bottom