Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
- Thread starter
- #41
Neno magamba lilianzishwa na JK ikiwa ni ishara ya kukiri kuwepo kwa mafisadi ndani ya CCM! Miongoni mwa mafisadi hao ni viongozi waandamizi wa CCM ambao walitumia madaraka yao vibaya wakiwa watumishi waandamizi wa serikali!Poa mkuu Ileje, nimekupata point yako, tuamini tu vijana wetu wanafanya kazi japo kunajitokeza madhaifu madogo madogo upande wa utekelezaji ambayo yanaweza kuharibu hata yale mazuri lakini wao wanakua hawahusiki moja kwa moja. Kitu kingine nachopenda, tusiwe na negative altitude na hawa wenzetu, asilimia kubwa ya mijadala humu JF nimeona ikipondwa lakini ikumbukwe hata kama kuna baadhi yao wanaenda kinyume na maadili yao ya kazi, basi ni wachache na wasifanye kitengo hiko kionekane kina-under perform. Uzalendo wetu uanzie ktk ku-support hii sekta muhim na sio kuipa wakati mgumu kwa kashfa na malalamiko ya kutoridhishwa na kila wanalofanya. Naamini mtu akishakua baba au mama, then mwanae ni mwanae tu, anapokosea au kupotoka, then mzazi anajitahidi kumrekebisha na kumshauri kwa upole na si kutangaza kwa majirani kwamba mwanangu hafai hata kwa dawa. Hivyo basi, najua JF ina watu tofauti tofauti. Kwa wale walio na experience ktk field hiyo, toeni mchango wenu. TZ ikianguka leo sio TISS wala serikali iliyopo, ni watanzania wote tutakua tumeanguka. Kuna muda naona kama unit ya utaifa inapotea kabisa, haipiti siku sijaona neno magamba humu ndani hata kwa issue ambayo ni nyeti. Hapa nilipo naangalia documentary ya Rwanda Genocide, jamani msiombe mpoteze amani katika nchi, huwa ni balaa.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Cha kushangaza pamoja na JK kuapa kuwang'oa lakini hadi leo zaidi ya miaka mitatu imepita hakuna kilichofanyika! Huu ni udhaifu na umeathiri sana heshima ya CCM mbele ya wananchi! Hivyo mahasimu wao katika siasa wataendelea kuitaja CCM kama magamba kwa kuwa imeshindwa kujisafisha!