Kwa mtazamao wangu,hii ni vita ya kibiashara sisi na jirani yetu,kwanini kila mara iwe na Arusha au Znz?baada ya wao kuboronga Mombasa na Nairobi sasa wanataka kuwaaminisha wageni kuwa hata Tz siyo salama.
TISS watizame nje ya siasa na dini
Naomba mnisamehe kwa kuwa nadokeza umbea wenye ukweli.
Kwamba siku za milipuko ya bomu darajani Zanzibar siku chache silizopita, siku hizo walikuwepo Wakenya waliofanana na watu wa Usalama na walikaa katika mahoteli maeneo hayo ya Dajani.
Nadokeza tu.
Kaka uko sahihi tena sana. Kwani hujaona mtu anasoma sana, halafu kwenye mtihani anafikiri sana. Majibu yakitoka ameambulia 5 ya 100. Sasa imagine asingesoma na kufikiri sana angepata nn. Sijaona thread ya hovyo humu jf kama ya huyo jamaaThat has to be the most pointless per thoughts pored into it because no matter how hard you think, and no matter how hard you try to convince people, and no matter how passionately you believe
Hivi ni kwanini tu wepesi wa kupeleka vidole kwa nchi nyingine? Je, usalama si suaka la serikali kulifanyia kazi? Serikali dhaifu imefanya hata utendaji wa taasisi nyeti kuwa dhaifu na kutowajibika. Muda mwingi vyomba vyetu vya usalama vipo busy na wapinzani, sijui lini hawa viongozi wetu wataamka toka usingizi huu wa uzembe na ujinga.
Kwa mtazamao wangu,hii ni vita ya kibiashara sisi na jirani yetu,kwanini kila mara iwe na Arusha au Znz?baada ya wao kuboronga Mombasa na Nairobi sasa wanataka kuwaaminisha wageni kuwa hata Tz siyo salama.
TISS watizame nje ya siasa na dini
Yaani kuna kila dalili stronghold za CHADEMA zipo matatizoni!
Wakenya walilipua uzinduzi wa Kanisa Katoliki ili wapate manufaa gani ktk eneo ambalo moja ya Wageni walio kuwa wamehudhuria ni Viongozi wa Kanisa toka Kenya??
Nakuunga mkono.
Yanayotokea Arusha ni Vita ya Utalii.
Kenya wameamua tukose wote.
Kwa mtazamao wangu,hii ni vita ya kibiashara sisi na jirani yetu,kwanini kila mara iwe na Arusha au Znz?baada ya wao kuboronga Mombasa na Nairobi sasa wanataka kuwaaminisha wageni kuwa hata Tz siyo salama.
TISS watizame nje ya siasa na dini
mkuu hata pale Arusha kwenye mkutano wa chadema Lukuvi aliitangazia dunia kuwa wapinzani wamejiripua ili kupata huruma ya wana nchi hivyo hiyo tume huru wanayoitaka iundwe kuchunguza haitahundwa, jamani milipuko na tindikali ni miradi ya ccm, kitulacho kipo nguoni mwetu kabla hatujatoka nje tujiangalie kwanza.Wa Tgk kwa visingizio.
Ilipokuwa inatokea kule Znz mlisema UAMSHO. Je huko Arusha mnarudikusingizia wakenya.
Poleni sana msitafute mchawi wachawi ni nyie wenyewe
.
Mkuu sijataja Kenya kwenye comment yangu!.
Nina hofu kuwa mabomu ya Arusha na Zanzibar yana harufu ya kubalance biashara ya utalii na Kenya baada ya al-shabab kuiandama biashara ya utalii Kenya kwa mabomu na mauaji. Juzi nilimsikia mtangazaji wa BBC raia wa Kenya kipindi cha focus on Africa akihanikiza uhusiano wa mabomu ya Arusha ya juzi na Serengeti na utalii. Hebu tuungane tuelekeze pua, masikio na macho yetu kuelekea mpaka na Kenya na watu wake tunaweza kutagundua kitu.
Suala la milipuko ya mabomu Tanzania hasa Arusha na Zanzibar, kuna 0.87 probability wameungana Serikali ya Rwanda na Kenya, na Uganda ikiwezekana Uganda imeshirikishwa, 0.13 tunawaachia vyombo vya usalama vifanye kazi yake na kupata majibu.
0.87 uhalisia wake ni huu
Kama ilivyoelezwa na vyombo vya usalama na bahadhi ya wadau kuwa aina ya mabomu yanayotumika katika matukio haya yanafanana. Hii inadhihilisha kuwa ni kikundi kimoja au muunganiko wa makundi tofauti yanayoshirikiana.
Mosi Rwanda(Paul Kagame), kwa suala la M23 ambao wanaaminika kuwa ni wanyarwanda (Nyuma ya Kagame).
Paul Kagame ana tabia ya kujihami mapema sana pale anapokuwa amefanya tukio baya au anapotarajia kufanya. Tukumbuke kuwa mara tu baada ya M23 kuanza harakati zake kagame alikanusha vikali kuhusika kwake huku jumuiya ya kimataifa(UN) na wengine wakithibitisha kuhusika kwa kagame juu ya M23, Siku chache zilizopita Kagame alieleza kupitia vyombo vya habari kuwa Tanzania na Rwanda ni ndugu na haina haja ya kuwatenga ndugu hawa huku kesho yake akijua kuwa anakutana katika kikao cha northen corridor kilichofanyika Kigali ambapo walikutana Kagame, Kenyatta, Museven na raisi wa Sudan kusini. Kulikuwa na ulazima gani wa kutamka maneno hayo kama si kujihami kabla ya tukio lililotarajiwa kufanyika siku inayofuata.
Pili, Kenya(Kenyatta)
Serikali ya kenya baada ya bandari zao kudorola pamoja na vita ya Utalii kuhusu wageni wanaokuja Arusha kwa ajili ya mbuga zilizo karibu, Kama tunavyofahamu Mlima kilimanjaro upo TZ lakini watalii wengi wakigeni huja kuona mlima huo wakipitia Kenya tusisahau hata ndege za kenya sasa zinaandikwa mount kilimanjaro kwa wao kujitangaza zaidi. Inawezekana ni vita ya mapato ya utalii kuweka milipuko ya mabomu wakilenga kuwafanya watalii waogope kuja Tanzania. Kwa nini milipuko iwe tu Arusha na Zanzibar isiwe Ukerewe, Mbeya ama Nanyumbu? Lah asha kuna kitu nyuma ya pazia.
Uganda(Museveni),
Inawezekana anashirikishwa kutokana na ukaribu mkubwa wa yeye na Kagame, hata M23 ambao kagame anahusishwa nao, baada ya kushindwa na majeshi ya UN(Tanzania ikiwemo) waasi wa M23 wanadaiwa kukimbilia Uganda, Je srikali ya Uganda haijui, hii inadhihirisha wazi ukaribu wake na Kagame.
Suala la kujiuliza kuna ajenda gani ya siri inayowafanya Kagame, Kenyatta na Museveni kukutana mara kwa mara na kutoihusisha Tanzania kwenye vikao hivyo? Tusisahau pia kauli ya Kagame aliyowahi kuitoa kuwa Akipewa Tanzania kuiongoza bandari pekee inatosha kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tajiri, Je ni wivu wa kiuchumi wanaotaka kufanya ili kuwaaminisha wafanyabiashara wa nje na ndani ya Afrika kuwa Tanzania si mahali salama?
Watanzania tunaipenda nchi yetu wala hatuhitaji uhasama na nchi yoyote, tunapenda tuendelee kuwa na amani hatuhitaji mabomu, watuachie Tanzania yetu na watanzania tutakuwa wa mwisho kuikana nchi yetu
Wa Tgk kwa visingizio.
Ilipokuwa inatokea kule Znz mlisema UAMSHO. Je huko Arusha mnarudikusingizia wakenya.
Poleni sana msitafute mchawi wachawi ni nyie wenyewe
.