Suala la milipuko ya mabomu Tanzania hasa Arusha na Zanzibar, kuna 0.87 probability wameungana Serikali ya Rwanda na Kenya, na Uganda ikiwezekana Uganda imeshirikishwa, 0.13 tunawaachia vyombo vya usalama vifanye kazi yake na kupata majibu.
0.87 uhalisia wake ni huu
Kama ilivyoelezwa na vyombo vya usalama na bahadhi ya wadau kuwa aina ya mabomu yanayotumika katika matukio haya yanafanana. Hii inadhihilisha kuwa ni kikundi kimoja au muunganiko wa makundi tofauti yanayoshirikiana.
Mosi Rwanda(Paul Kagame), kwa suala la M23 ambao wanaaminika kuwa ni wanyarwanda (Nyuma ya Kagame).
Paul Kagame ana tabia ya kujihami mapema sana pale anapokuwa amefanya tukio baya au anapotarajia kufanya. Tukumbuke kuwa mara tu baada ya M23 kuanza harakati zake kagame alikanusha vikali kuhusika kwake huku jumuiya ya kimataifa(UN) na wengine wakithibitisha kuhusika kwa kagame juu ya M23, Siku chache zilizopita Kagame alieleza kupitia vyombo vya habari kuwa
Tanzania na Rwanda ni ndugu na haina haja ya kuwatenga ndugu hawa
huku kesho yake akijua kuwa anakutana katika kikao cha northen corridor kilichofanyika Kigali ambapo walikutana Kagame, Kenyatta, Museven na raisi wa Sudan kusini. Kulikuwa na ulazima gani wa kutamka maneno hayo kama si kujihami kabla ya tukio lililotarajiwa kufanyika siku inayofuata.
Pili, Kenya(Kenyatta)
Serikali ya kenya baada ya bandari zao kudorola pamoja na vita ya Utalii kuhusu wageni wanaokuja Arusha kwa ajili ya mbuga zilizo karibu, Kama tunavyofahamu Mlima kilimanjaro upo TZ lakini watalii wengi wakigeni huja kuona mlima huo wakipitia Kenya tusisahau hata ndege za kenya sasa zinaandikwa mount kilimanjaro kwa wao kujitangaza zaidi. Inawezekana ni vita ya mapato ya utalii kuweka milipuko ya mabomu wakilenga kuwafanya watalii waogope kuja Tanzania. Kwa nini milipuko iwe tu Arusha na Zanzibar isiwe Ukerewe, Mbeya ama Nanyumbu? Lah asha kuna kitu nyuma ya pazia.
Uganda(Museveni),
Inawezekana anashirikishwa kutokana na ukaribu mkubwa wa yeye na Kagame, hata M23 ambao kagame anahusishwa nao, baada ya kushindwa na majeshi ya UN(Tanzania ikiwemo) waasi wa M23 wanadaiwa kukimbilia Uganda, Je srikali ya Uganda haijui, hii inadhihirisha wazi ukaribu wake na Kagame.
Suala la kujiuliza kuna ajenda gani ya siri inayowafanya Kagame, Kenyatta na Museveni kukutana mara kwa mara na kutoihusisha Tanzania kwenye vikao hivyo? Tusisahau pia kauli ya Kagame aliyowahi kuitoa kuwa Akipewa Tanzania kuiongoza bandari pekee inatosha kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tajiri, Je ni wivu wa kiuchumi wanaotaka kufanya ili kuwaaminisha wafanyabiashara wa nje na ndani ya Afrika kuwa Tanzania si mahali salama?
Watanzania tunaipenda nchi yetu wala hatuhitaji uhasama na nchi yoyote, tunapenda tuendelee kuwa na amani hatuhitaji mabomu, watuachie Tanzania yetu na watanzania tutakuwa wa mwisho kuikana nchi yetu