Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 18,069
- 25,172
- Thread starter
- #21
Mbona wewe nawe unaleta longo longo tu hujaleta mfano wowote hap. Umeleta quoti ya online dictionary ukiwa umeitafsiri vibaya.Weka mfano hapa tuuangalie acha longolongo.
Ngoja nikueleze kitu kimoja. Wakati wa ukoloni, mashamba ya karanga yaliyokuwa yanamilikiwa na wakoloni pale Kongwa yalishambuliwa sana panya. Wakoloni wale wakajiri watu wa kupambana na panya hao. Waafrika waliojiriwa kufanya kazi hiyo walikuwa wakiitwa "Rat Catchers" halafu wazungu na wahindi waliokuwa anafanya kazi hiyo hiyo walikuwa wanaitwa "Rodent Officers."
Sasa wewe unasumbuliwa sana akili ya kutokujua tofauti ya "Rat Catcher" na "Rodent Officer" katika scenario kama hiyo. Ni Ufinyu mkubwa sana wa akili unaokusumbua ukitaka utamaduni na mazingira ya waingereza wakati huo ndiyo yendelee kutawala hadi leo. Unaonekana kuelemewa sana na uzito wa kukariri mambo.
Marahemu Senator McCain alizaliwa Panma, lakini wakati anagombea urasi kwa mara ya kwanzi kulikuwa na watu waliotaka kumpinga kwa madai kuwa alizaliwa Overseas.