International Schools zina nini cha zaidi?

Kafwifwilo FM ipo huko Sudan kusini
 
Kids learn Music, Art, makerspace( engineering), drama or guidance, and the most important part ni being inquirers
 
Tofauti ni kwamba ukisoma shule za kata utaishia kuwa polisi, Dr., mwl, bank teller etc lakini ukisoma international schools utaishia CEO wa hallotel, Voda, UNDP, WHO etc na tofauti hii inatokana na kwamba wewe ulisoma elimu yooote kwa gharama ya tsh. Mil. 20 (ikiwemo bumu la HESLB, mahindi ya kuchemsha na mkaango na hata bwimbwi (unga wa mkaango), yebo , ugali ngogwe etc) lakini mwenzio hii ni ada ya muhula mmoja.
 
Kwanza, international schools zinatumia mitaala ya kimataifa kama vile Cambridge Curriculum, IB na Waldorf. Mtoto wa Cambridge Bongo akihamia India aunMatekani, ataenda Cambridge ya huko na kuendelea pale pale alipoishia huku bongo.
Siyo St. Mary's wantumia NECTA halafu wanajiita international.

Pili, approach ya ufundishaji ni tofauti na wa NECTA.
NECTA walimu wanapiga lecture, wanakaririsha wanafunzi. International curriculums zinatumia hands on activities na namna zinazomfanya mtoto awe mchunguzi na mchambuzi.
Watoto wa primary tu wanafanya research (kwa level yao) na kuzifanyia presentations, wanafanya experiments, Wana classify vitu n.k

Ukija kwenye computer na ICT, wana computers, smartboards, hata ubao si wa chaki, mostly wantumia boardmarkers.

Pia, watoto wa international wanapewa nafasi ya kuexplore Dunia.
School trips sio limited kwa nchini tu. Wakubwa wanaenda nchi zingine kama Egypt, Italy n.k kutokana na matakwa yao.

Pamoja na hayo, content ya international schools ni tofauti sana na NECTA.
Mf. English tunayosoma NECTA ni basic English grammar. English ya Cambridge ni Ile ya Native speakers. So by darasa la tatu utakuta watoto wanachambua phrasal nouns au writing techniques zilizotumika kwenye text, vitu ambavyo sie tulisoma kwenye Language ya A-level.
Hata content nyingine ni recent katika technology, history ni ya Dunia nzima kama Roman Empire, Greece, Sumerians, e.t.c sio NECTA watoto wetu wanasoma John Speke na IBEACO za mwaka 1890s huko.


Mambo ni mengi... Siwezi andika yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…