Internet Outage: Unatumia mtandao gani wenye nafuu kwenye hili janga?

Kuna kitu nimefikiria kwa hili tukio la leo la internet kuwa chini, sisi tulio ulimwengu wa mitandao tumeona isiyokuwa kawaida, siku imekuwa ngumu na wengi wamepata gharama na hasara kwa kiasi chake!
Siku hao wa miliki wa internet na mamlaka zikiamua kuzima kabisa mtandao wa internet taharuki itakuwa kubwa mno kiasi cha kuona maisha yamefika mwisho!

Wakati huo huo kuna watu hawajui kama kuna chochote kilichotokea ama kinachoendelea, wasio kuwa na simu za data na wasio kuwa na simu kabisa kwao hakuna kilicho badilika leo!
Maisha yanatafakarisha sana.
 
Umesema hivi mpaka nimeogopa. For real hii kitu ikae sawa na isije ikajirudia mbeleni, imenipotezea shughuli kubwa sana leo.
Na hapa nimeland juzi kwaajili ya kazi hiyo. Daaah
 
Theory yangu mkuu,

Uliosumbua ni waya wa Baharini, ila waya za Kwetu humu ndani hazijaathirika, site ambayo ina server South ama Kenya ama nchi ambayo ni ya Africa unaweza ukai access bila shida ila server za Mabara tofauti zinazotumia route za Bahari zinasumbua.

Kwangu dogo kashinda youtube haijamsumbua, ila site nyengine bila bila.
 
Hapana sio kweli, Facebook insta mitandao kama redcafe ya UK ilikua huwezi ku access, hata Hio youtube ni spidi ndogo sana ya kobe
 
Internet haiwezi kuzimwa its just sisi kwetu tumeegemea sehemu moja, I think mitandao yote inatumia mkonga.

Tukio kama hili liliwahi tokea around 2011/12 meli iligonga submarine cable na Internet kukata siku kadhaa, Mitandao ikahamia satelite, access ikawepo ila kwa speed ndogo around 80KBps (640kbps) ila ipo,

Leo ni kama vile mitandao imejisahau hakuna backup kabisa ya internet zao.

Tofauti na Bahari kuna Fiber ya ndani ya Africa ambayo ina Konect na bahari nyengine za mbali kama Mediterranean na Atlantic na zipo pia kampuni mbalimbali za Satelite internet, zote hizi hazijaathirika.
 
Nadhani hili ndio linaloleta changamoto, labda inaweza kuna vizuizi kutoka kwenye mamlaka.
 
Tunahitaji internet mbadala. Nyakati hizi internet ndiyo uchumi.
 
Voda yangu 4G+ na haiwezi kufungua telegram kaz kwelikweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…