Interview: Koti jeusi la kodrai na suruwali ya kadeti nyeupe

Interview: Koti jeusi la kodrai na suruwali ya kadeti nyeupe

Nimeamini kweli sisi watanzania ni wagumu kuelewa. Ndugu yangu unayetafuta kazi, kwenye intavyuu vaa NOTI. Haya mambo ya suti kwenye madaladala ni kujitafutia majasho ufike unanuka kikwapa mpk waahirishe zoezi bure. Mi nakwambia ukienda kamili kama nilivyokwambia, hakuna atakayejali kama umevaa kodrai au mbunju au hata kama umeenda uchi kabisa.

Ila lingine tu nikushauri, endapo utaukataa ushauri wangu hapo juu wa kwenda na laki 4, hayo mambo yenu ya mitindo nayo yanategemea unaomba kazi gani. Kama kazi yenyewe unayoomba ni ya BARMAN kwenye kasino, hiyo kodrai yako na kadet safi kabisa. Unaweza pia kufuga tudevu kama kibeberu cha kusini na viatu vya raizon.

You should be smiling at all times at any cost, sawa sawa?!
 
Ukipendeza sana mi skuchukui bana, ofcn kwangu kuna warembo wengi sana.
 
Vaa mavazi ambayo kesho ukiajiriwa unaweza kuyavaa kazini.Dadisi kampuni ina utamaduni gani ikiwa pamoja na mavazi angalau usionekane tofauti sana pia na wewe usivae mavazi yatakoyokufanya usiwe na amani.
 
mkuu mimi nilipiga shati la mikono mirefu rangi ya kung'aa ya zambarau na tai nyekundu, suruali ya kushona ya njano na chini nilimaliza na kidonge, halafu nilipiga uturi flani hivi wa kichokozi, mfukoni nilikuwa na kitana [muhimu sana hii], nilipigwa maswali ooh sijui designer wako nani? uturi umeununua wapi? sh ngapi? na maswali machache yanayohusiana na kazi yangu basi jamaa wakanipa kazi hapo hapo huku wachimba chumvi wengine wakisubiri kwenye benchi kuingia
 
wadau huwa nikivaa hayo mavazi huwa natoka chicha sana, je naweza kwenda kwenye interview nikiwa nimevaa hivyo?
asanteni. na je shati ya draft naweza kuvaa kwenye interview?

ideally ni mavazi yapi mazuri ya kuvaa kwa interview

asante

hivo hivo eeh! bomba sana.
 
Dahmasuala ya kuvaa suruali za vitambaa na tai yanaboa.nikivaa tai nahisi kama nanyongwa hila kutokana na hali halisi ya tz (severe lack of jobs) itabidi nivae tu.....
 
Mbona mnachulia mambo kirahisi rahisi hivyo?! tusi-generalize interview. Muonekano wako una alama za kutosha kabisa kwenye interview. Iwe kuvaa suti, au mavazi ya aina yoyoteile ina tegemeana na aina ya kazi unayoenda kuifanyia interview. Ofisa wa benki, kwa mfano, hawezi kuvaa kama dereva au fundi magari, nesi hawezi kuvaa kama mwalimu, secretary hawezi kuvaa kama anaenda night club. kwa hiyo mavazi yanategemea kazi uliyoiomba.
 
Back
Top Bottom