Mwanamuziki wa Bongo Flava, Ali
Kiba amefunguka kuhusu mambo
yaliyomkwaza kutoka kwa Diamond
miaka michache iliyopita baada ya
mkali huyo kutoka na wimbo wa
Kamwambie uliogeuka kuwa wimbo
wa taifa wa Bongo Flava kwa muda.
Akiongea na kipindi cha Mkasi, Ali
Kiba ameeleza kuwa yeye ndiye mtu
aliyepitisha ombi la Diamond
kurekodi katika studio za SharoBaro
kwa kuwa wakati huo alikuwa mdau
mkubwa katika uongozi wa studio
hizo lakini matokeo yake yalimgeukia
hadi kuamua kujitoa katika team
hiyo.
Ameeleza kuwa mara baada ya
Diamond kutoka na Kamwambie,
aliona gazeti moja lililokuwa
lililomkariri akisema kuwa yeye ndiye
fimbo ya Alikiba na amekuja
kumfunika.
Hata hivyo maneno yaliyowekwa
kaitika gazeti hilo yalianza kuaminika
kwa Ali Kiba baada ya kukutana nae
mara kadhaa kwenye shows.
Lakini nilishawahi kukaa na
Diamond katika mikutano ya Shows
ambazo tunaitwa pamoja wasanii na
nini na nini. Mimi napendaga
kuongea nae kama mdogo wangu kwa
sababu the way nilivyokuwa
nikimtreat ni kama wadogo zangu
wengine akina Bob Junior akina
nani
Nilimsikia akiongea sana
kwamba nimekufunika kwenye show
fulani, nimekufunika kwenye show
fulani. Kwa kweli the way nilivyokuwa
nikimtreat kama mdogo wangu. Kwa
hiyo yeye alikuwa ameconcentrate
sana katika kunifunika. Alieleza Ali
Kiba.
Mimi sio mtu wa kumind sawa. Kwa
hiyo alivyokuwa anaongea
anajifurahisha. Hata kama
amenifunika mimi nilikuwa naweza
kumpigia makofi vilevile. Si nataka
afanikiwe. Kwanza nafurahi. Napenda
sana challenge. Inakufanya
unaaamke. Aliongeza.
Kujirudia kwa neno kufunika kila
walipokuwa akikaa na Diamond
kuligeuka kuwa kero kwa Ali Kiba
huku mengine yakipenya kutoka kwa
watu wake wa karibu.
Kwa hiyo kitu ambacho kilikuwa
kinahappen tukiwa karibu hivi, ni
hivyo vitu ambavyo akizungumziwa
nimekufunikaa..nimekufunika.
Nikawa nikitoa video nasikia
maneno, kwamba Ali amesikia
maneno nimetoa hii na yeye ametoa
hii. Mi sijawahi kumsikia mwenyewe
akisema. Ila watu wake wa karibu wa
karibu wanakuja wanasema. Unaweza
kumjua mtu tabia yake kwa
kumuangalia, kwa kuishi nae.
Ali ameeleza kuwa hata baada ya
kuamua kukaa kimya amlee mwanae
wa kiume alisikia tena maneno
kutoka kwa mwimbaji kwa Diamond
kuwa amemkimbia.
Hata hivyo, hii ilikuwa story ya
zamani ambayo wengi wanaweza
kuwa nayo lakini ikamhusu mtu
ambaye kwa sasa amekuwa rafiki wa
kudumu.
Hivi karibuni Ali Kiba alisema kuwa
hana tatizo lolote na Diamond na
kuwataka watu wasimgombanishe na
msanii huyo.
Ni muda wa biashara. Yaliyopita si
ndwele (maradhi) tugange yajayo
kwa maendeleo ya Bongo Flava.
Kilichobaki ni ushindani wa
kibiashara kama alivyosema Babu
Tale.