Interview ya Ommy Dimpoz: Bifu lake na Diamond, hastahili lawama

Interview ya Ommy Dimpoz: Bifu lake na Diamond, hastahili lawama

Nawashangaa mnaosema huyo ommy ni mstaarabu sijui nini, hv haya yote yameanzia wapi? mbona hata siku moja diamond hakuwa kumuongelea, na yeye sio mwehu aitwe tu kwenye interview jana aanza kumuongelea vile, huyu ommy ndo aliyaanzisha tena baada ya kutoa nyimbo na kiba alivyoona haiendi akaamua kutafuta ngazi ambayo ni diamond, akaanza choko choko sijui ananunua views youtube, sijui mziki wake mzuri ila wa mond wa ujanja ujanja, mond yalipomfika hapa ndo akaamua kumtapikia na kumuharishia, leo hii baada ya kuona maji ya shingo ndo anajifanya kutafuta sympathy kwa kujifanya amejishusha, akwende hukoo
 
Wakati Jana mchana alikuwa xxl na yeye huko visiwan kaenda SAA ngapi, ongea ulicho na uhakika nacho
Halafu kitendo hicho ni muda mfupi tu , so it's possible maana yule mama c kwa kumwonea wivu mwanae..mxiuuu shame on them!![emoji57] [emoji57] [emoji57]
hizo ni fununu na muda mwingi tu anakuwa nje bila mama yake kwa hiyo ukitazama utaona hizo ni fununu.
walianza mara freemasons, mara anabeba madawa now wamekuja na hili...
 
Naona watu mna muhukumu diamond platnumz, lkn jamaa huwaga wanamuanza wenyewe mara ananunua view, mara wao wanafanya mziki mzuri kuliko wengine ni janja. Tatizo la diamond platnumz the way anavyoreact huwaga aanareact vibaya sana, lkn kwa Tanzania hii hamna superstar anayesemwa vibaya na kuimbwa vibaya kama diamond platnumz. Najua ommy leo anaonekana innocent lkn njia nzuri ya kumjua nani mgomvi ni kuwakutanisha pamoja na kuwasikiliza alafu ndio uje na output na ndio thumuni la mahakama, hata mshtakiwa huwa anajitetea unaweza kukuta anaonewa. KIBA mna muona mkimya lkn vita vyake Kuna watu anawatanguliza (Kenya KIBA na sallam walipiga picha, kwa kutumia simu ya kiba wakati wa coke studio mwaka jana, lkn mtu wa kwanza kuipost ni shilole kiuno), KIBA na OMMY wana mafumbo, jamaa akiwajibu mnaona anakosea LKN MKAE MKIJUA HAMNA MTU MBAYA KAMA MTU MKIMYA HASA AKIAMUA KUFANYA UBAYA, KUMGUNDUA HUWA INACHUKIA MUDA NA HATA MKIMGUNDUA KUPONYA MADONDA ITACHUKUA MUDA. Na ww ommy ww si mtu wa kwanza kufanya kolabo na kiba, mbona FA yupo cool, hana vijembe kama ulivyokuwa navyo ww, tundaman, blue wote wapo cool, badilikeni msije mkashindwa kuzikana mwisho wa siku.
 
Hujui huu ugomvi,Beef ni Kiba na Diamond Dimpoz ameingilia ndio maana yanamkuta,jiulize miaka yote Dimpoz na Diamond walipishana lakini uliwahi kusikia wanatukanana?
Kwahiyo hapo sasa nahis mgomvi kati beef hilo ashajulikana ni nan, yule anaetoa sana mapovuu ndo mgomvi
 
Kaburi mbona lipo tu bila hata kujichimbia?!uchawi ungekuwa unaleta utajiri basi waganga wa kienyeji wote wangekuwa mabilionea
Eeeh kama nawe ulifikiria kumlala maza ako upate utajiri uache kabisa kufikiria hizo mambo!
Afu uache ushabiki mandazi ndio unapelekea hadi uone kulala na maza ni kitu cha kawaida!
 
Diamond na Ali Kiba wana beef kubwa sana,Diamond na Dimpoz walikuwa washkaji sana na leo ameongea hilo but walipishana lakini ugomvi wao haukuwa mkubwa kiasi hiki.Baada ya Dimpoz kufanya kolabo na Kiba nae amejiunga timu Kiba huko Instagram kumponda Diamond ndio ugomvi ukafumuka tena juzi .Diamond wakati anahojiwa juzi madongo mengi alikuwa anampiga Ally Kiba siyo Dimpoz so kitendo cha Kiba kukaa kimya kinampa credit beef inaonekana siyo yake
Real man dont talk shiit!!
 
Kwa mtu kama wewe hutarajiwi kuongea tofauti na hicho manake ulishaonesha sura yako halisi zaidi ya miaka miwili iliyopita:Kinyume chake, ndo kwanza anazidi kupiga show za nje ya mipaka!! Tukimalizia na hii:Unaonesha wazi upo mkao wa kula kushadadia baya lolote hata kama ni la kipuuzi! Hebu weka hapa hilo "gazeti" kama si kwamba unazungumzia vigazeti vya udaku!!!
Teh teh teh teeeeh!!! Yaani nyie bwana! Nacheeeka kama mazuri.
 
Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.

Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi hicho hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy amewahi kuzifanya ili kuomba wayamalize.

Hitmaker huyo wa Wanjera amesema katika urafiki wao wote na Diamond, ni yeye ndiye alikuwa mwaminifu (loyal) zaidi katika kuuenzi lakini kuna wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa vinavyohusiana na kazi.

Amesema mara zote alikuwa akimshirikisha kwenye mipango yake ikiwa ni pamoja na kumsikilizisha nyimbo zake kabla ya kutoka ili kumuomba ushauri na kutolea mfano alivyomsikilizisha wimbo wake Tupogo na kumweleza kuwa amepanga kuongeza vionjo vya saxaphone kwa kumtumia King Malou. Hata hivyo anadai kuwa siku chache baadaye alishangaa kumkuta Diamond akiwa na mpiga saxaphone huyo akiingia kionjo kwenye wimbo wake ‘Number 1’ katika studio za MJ Records.

“Nikajiuliza kuwa pengine labda alikuwa na wazo kama hilo, sikutaka kujiuliza mengi, unajua sometimes ukijiuliza mengi utaenda far zaidi, nikauchuna tu,” alisema Ommy.

Anasema baadaye alisikia akimuambia Marco Chali kuwa amchomee CD kwakuwa anasafiri na walipomaliza Ommy alimuuliza kuhusu safari hiyo lakini Diamond alimuambia kuwa alikuwa akimdanganya tu producer huyo wa MJ Records na kwamba hakuna safari yoyote.

“Kesho yake naona anapost picha yupo kwenye ndege, nikajiuliza ‘huyu si nilimuuliza jana kama anasafiri, si ni mwanangu’, nikasema anyway labda ni safari imejitokeza ghafla you never know,” ameeleza Ommy.

Baadaye mshkaji wao Halima Kimwana alikuja kumwambia kuwa Diamond alienda Afrika Kusini kufanya video yake kitendo kilichomwacha na maswali mengi lakini anadai alipuuzia. Amesema baada ya muda ndipo Diamond alipofanya uzinduzi wa video ya Number 1 na yeye mwenyewe kualikwa.

Amesimulia tukio jingine ambalo lilimuumiza ni baada ya kumuomba Diamond waende pamoja Marekani kwenye tuzo za Afrimma kwa gharama zake mwenyewe ili amsaidie kumtafutia connection.

“Sasa kila siku nikiuliza safari lini naona mtu anaingilia huku anatokea huku.”

Anadai swahiba wake huyo aliendelea kumchenga hadi alipokuja kugundua amesafiri bila kumwambia na siku hiyo akawa hapokei simu zake. “Baada ya kupita masaa mengi, jioni anakuja kunicheck yuko transit South Africa ‘mwanangu ilitokea ghafla nikasafiri.’ Kwahiyo nikajiuliza nikasema hapa kuna style za kupunguzwa. Kibinadamu unajua lazima uchekeche.”

Ommy pia alielezea jinsi ambavyo alikuwa mtu wa kwanza afanye collabo na Davido na alikuwa tayari kutoa $3,000 lakini baadaye Sallam, meneja wa Diamond, alikuja kumweleza kuwa Dangote yupo tayari kutoa $5,000 ili wafanye naye. Anasema aliachana na collabo hiyo na kutafuta nyingine na Iyanya ambayo nayo pia alikuja kugundua baadaye rafiki yake huyo ameshaiwahi.

Hata hivyo Ommy amedai kuwa kitendo cha yeye kumtumia Wema Sepetu kwenye video ya Wanjera ilikuwa kama sababu tu ya Diamond kuvunja ushkaji wake. Amesema ni kwasababu amekuwa na urafiki na Wema hata kabla ya kukutana na Chibu na kwamba hadi ‘first kiss’ yao aliishuhudia kwa macho yake.

Ommy ambaye jina lake ni Omari Nyembo, amesema kukosana kwao hakukuwa sababu ya yeye kumchukia pia Wema kwakuwa urafiki wao haukusika na kwamba kipindi Ommy anaenda SA kufanya video hiyo, Wema alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine na kukanusha kuwahi kutoka naye kimapenzi.

“Kwahiyo nikaona kuna suala lilikuwa kwamba mtu ametafuta sababu. Hebu niambie Wema amekuwa na mahusiano na watu wangapi wengine ambao leo hii bado unaona D yuko nao close? Kwanini nilipokuwa naye mimi tu ndio imekuwa tatizo?” amehoji staa huyo.

Kuhusu tuhuma za kutaka ‘kupumuliwa’ zilizotolewa na Diamond kwenye post yake ya Instagram dhidi yake, Ommy amesema pale ‘mtu anapotaka kukutana hakuchagulii tusi.’

“Sometime unapoitoa kauli, huwezi kujua itamwathiri mtu kwa kiasi gani, pengine itamwathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu kuna mtu ataichukua ile kauli kiushabiki. Hata kwenye comments, mimi ninaweza kuzima comments zangu kwenye Instagram lakini nimeziacha na ukisoma comments utaona kabisa mwingine anakutukana ‘we shoga.’ Lakini as long as mimi ninajua mzima hainiathiri, kwanza hakuna tusi jipya, imeanza kutukanwa mimba!”
 
Jealousy, hatred bado ni tatizo linalowatafuna wasanii wengi hapa nchini, kwa maelezo ya Ommy..Diamond angekuwa na roho nzuri angemfanikishia mambo mengi sana ya kimuziki mwenzake..lakini kwa sababu ya tamaa yake ndio maana haya yakaibuka...huu ni upuuzi kwa watu wanaojielewa...
 
Back
Top Bottom