Interview ya Ommy Dimpoz: Bifu lake na Diamond, hastahili lawama

Interview ya Ommy Dimpoz: Bifu lake na Diamond, hastahili lawama

cloudz wachonganishi sana!
haikuwepo haja ya kuwaita tofauti..
kwanini wasingewaita wote jana
kila mtu akajieleza..
wakakosoana

kesi za upande mmoja ngumu kuzijudge kwakweli
Hahaha imepeenya hiyo.

Ommy amewafanya mmekua wapole kama kuku mwenye mdondo.

Nadhani leo mmepata somo.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kwenye mambo ya shutma lazima usikilize pande zote ndo utausoma mziki katika hali ya kawaida hawezi kuongea mazuri aliofanyiwa na domo japo naamini yapo
Sikiliza interview ommy amemshukuru Diamond kuwa anamchango mkubwa sana kwenye mziki wake na mafanikio yake kwa ujumla.

Na ukisikia mabaya mond aliyomfanyia ommy utakiri ommy ni mtu na nusu, ana moyo wa chuma.

Iv mavoko hakujiuliza kwanini sheta hakujieka chini ya mond mpaka nae kizembe tena na uwezo ule ukiomtisha uyo mond alafu kwenda kujieka chini yake? Mavoko kama ni ivo bas kaenda kupoteza utamu na maneno yake kuntu kama ile roho yangu mambo ya mchuzi wa pweza na huku pacha wangu mrithi wa bibi!. Dah mond Ovyo sana!.
una pigo za ki-lady gaga
zigo la kuvunja chaga
kifaranga kimetaga
[emoji85][emoji85]
sijawahi kumpenda mavoko tangu "uzuri wako"
ila kwenye kokoro
ni shida napiga kutwa mara7

Umeongea jambo la msingi ambalo binadamu wengi hawajiulizi. Ommy kafanikiwa kupata huruma ya raia Ila yeye ndio alianza maana alijua kabisa kauli Yake kuhusu kununua viewers itakuwa Na impact kwahiyo Kama ana basara Kama ambavyo wengi wanasema hakupaswa kuongea ile kauli kwenye media
mi kwa upande wangu sijaona kosa la Diamond. Swala la kufichana baadhi ya vitu kwenye bussiness ni jambo la kawaida. Na ndio maana hata uwe na uswahiba na mzee Mengi usitegemee atakushirikisha mipango yake ya biashara. NEVER. Wakati Diamond anaenda kushuti south hakumtaarifu mshkaji(sio meneja wake) ila wakati wanazindua hiyo video akampa mwaliko mwana. And that's friendship. Nadhani kilichotokea kwa hao jamaa ni mmoja kushindwa kutofautisha URAFIKI nini na KAZI nini.

Wakati Jana mchana alikuwa xxl na yeye huko visiwan kaenda SAA ngapi, ongea ulicho na uhakika nacho
Halafu kitendo hicho ni muda mfupi tu , so it's possible maana yule mama c kwa kumwonea wivu mwanae..mxiuuu shame on them!![emoji57] [emoji57] [emoji57]
Kuna watu wanafikiria kwa masaburi.... Jana tunamsikiliza xxl... Kumbe alikuwa anahojiwa akiwa visiwa vya Mayotte.... mtumeeeee.....

Kuna watu wanafikiria kwa masaburi.... Jana tunamsikiliza xxl... Kumbe alikuwa anahojiwa akiwa visiwa vya Mayotte.... mtumeeeee.....
Kama hukusikiliza bora ukakaa kimya, au kama hukuelewa ni vema ukauliza kwanza. Haya mambo ya team yanawafanya watu wazima wanabehave km mazuzu ama watoto. Acheni kudhalilisha uwezo wenu wa kureason sometimes. Hakuna ulazma wa kuchangia kila uzi. Mingine baki kuwa msomaji tu km unahisi neno lako haliwezi kukizidi kimya chako busara

Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.

Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi hicho hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy amewahi kuzifanya ili kuomba wayamalize.

Hitmaker huyo wa Wanjera amesema katika urafiki wao wote na Diamond, ni yeye ndiye alikuwa mwaminifu (loyal) zaidi katika kuuenzi lakini kuna wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa vinavyohusiana na kazi.

Amesema mara zote alikuwa akimshirikisha kwenye mipango yake ikiwa ni pamoja na kumsikilizisha nyimbo zake kabla ya kutoka ili kumuomba ushauri na kutolea mfano alivyomsikilizisha wimbo wake Tupogo na kumweleza kuwa amepanga kuongeza vionjo vya saxaphone kwa kumtumia King Malou. Hata hivyo anadai kuwa siku chache baadaye alishangaa kumkuta Diamond akiwa na mpiga saxaphone huyo akiingia kionjo kwenye wimbo wake ‘Number 1’ katika studio za MJ Records.

“Nikajiuliza kuwa pengine labda alikuwa na wazo kama hilo, sikutaka kujiuliza mengi, unajua sometimes ukijiuliza mengi utaenda far zaidi, nikauchuna tu,” alisema Ommy.

Anasema baadaye alisikia akimuambia Marco Chali kuwa amchomee CD kwakuwa anasafiri na walipomaliza Ommy alimuuliza kuhusu safari hiyo lakini Diamond alimuambia kuwa alikuwa akimdanganya tu producer huyo wa MJ Records na kwamba hakuna safari yoyote.

“Kesho yake naona anapost picha yupo kwenye ndege, nikajiuliza ‘huyu si nilimuuliza jana kama anasafiri, si ni mwanangu’, nikasema anyway labda ni safari imejitokeza ghafla you never know,” ameeleza Ommy.

Baadaye mshkaji wao Halima Kimwana alikuja kumwambia kuwa Diamond alienda Afrika Kusini kufanya video yake kitendo kilichomwacha na maswali mengi lakini anadai alipuuzia. Amesema baada ya muda ndipo Diamond alipofanya uzinduzi wa video ya Number 1 na yeye mwenyewe kualikwa.

Amesimulia tukio jingine ambalo lilimuumiza ni baada ya kumuomba Diamond waende pamoja Marekani kwenye tuzo za Afrimma kwa gharama zake mwenyewe ili amsaidie kumtafutia connection.

“Sasa kila siku nikiuliza safari lini naona mtu anaingilia huku anatokea huku.”

Anadai swahiba wake huyo aliendelea kumchenga hadi alipokuja kugundua amesafiri bila kumwambia na siku hiyo akawa hapokei simu zake. “Baada ya kupita masaa mengi, jioni anakuja kunicheck yuko transit South Africa ‘mwanangu ilitokea ghafla nikasafiri.’ Kwahiyo nikajiuliza nikasema hapa kuna style za kupunguzwa. Kibinadamu unajua lazima uchekeche.”

Ommy pia alielezea jinsi ambavyo alikuwa mtu wa kwanza afanye collabo na Davido na alikuwa tayari kutoa $3,000 lakini baadaye Sallam, meneja wa Diamond, alikuja kumweleza kuwa Dangote yupo tayari kutoa $5,000 ili wafanye naye. Anasema aliachana na collabo hiyo na kutafuta nyingine na Iyanya ambayo nayo pia alikuja kugundua baadaye rafiki yake huyo ameshaiwahi.

Hata hivyo Ommy amedai kuwa kitendo cha yeye kumtumia Wema Sepetu kwenye video ya Wanjera ilikuwa kama sababu tu ya Diamond kuvunja ushkaji wake. Amesema ni kwasababu amekuwa na urafiki na Wema hata kabla ya kukutana na Chibu na kwamba hadi ‘first kiss’ yao aliishuhudia kwa macho yake.

Ommy ambaye jina lake ni Omari Nyembo, amesema kukosana kwao hakukuwa sababu ya yeye kumchukia pia Wema kwakuwa urafiki wao haukusika na kwamba kipindi Ommy anaenda SA kufanya video hiyo, Wema alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine na kukanusha kuwahi kutoka naye kimapenzi.

“Kwahiyo nikaona kuna suala lilikuwa kwamba mtu ametafuta sababu. Hebu niambie Wema amekuwa na mahusiano na watu wangapi wengine ambao leo hii bado unaona D yuko nao close? Kwanini nilipokuwa naye mimi tu ndio imekuwa tatizo?” amehoji staa huyo.

Kuhusu tuhuma za kutaka ‘kupumuliwa’ zilizotolewa na Diamond kwenye post yake ya Instagram dhidi yake, Ommy amesema pale ‘mtu anapotaka kukutana hakuchagulii tusi.’

“Sometime unapoitoa kauli, huwezi kujua itamwathiri mtu kwa kiasi gani, pengine itamwathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu kuna mtu ataichukua ile kauli kiushabiki. Hata kwenye comments, mimi ninaweza kuzima comments zangu kwenye Instagram lakini nimeziacha na ukisoma comments utaona kabisa mwingine anakutukana ‘we shoga.’ Lakini as long as mimi ninajua mzima hainiathiri, kwanza hakuna tusi jipya, imeanza kutukanwa mimba!”
Daah sio sir kama ni kweli katendwa haya mond hajafanya fresh kbs,kumbe Ommy kaumizwa kwa kias kikubwa sana na swaiba wake

Iv mavoko hakujiuliza kwanini sheta hakujieka chini ya mond mpaka nae kizembe tena na uwezo ule ukiomtisha uyo mond alafu kwenda kujieka chini yake? Mavoko kama ni ivo bas kaenda kupoteza utamu na maneno yake kuntu kama ile roho yangu mambo ya mchuzi wa pweza na huku pacha wangu mrithi wa bibi!. Dah mond Ovyo sana!.
Umesahau maneno kuntu ya kwenye Silali mkuu?
Aiseee ule ndio wimbo wangu bora wa Rich Mavoko wa miaka yote.

Muda utatuambia,ataukumbuka ushauri wa Baraka kukiwa kumeshakucha.

Atashindwaje kua mstaarabu wakat mond kamwaga mboga angetokwa povu tu angeanikwa kweupeeee na bado ndio dawa ya waropokaji nani alimuanza mwenzie izo sympathy zako kwenye interview hazitabadilisha ukweli wa upunga mrs mwarabu ommy msambwanda leo ndo umeshika adabu eeh siulijifanya kujitoa akili kumdiss mond unabahat umejishusha tungeanika kila kitu ebooo moto umewasha mwenyewe na unakuunguza tungemwaga mpaka audio zako unabahati haya kampikie mwarabu huko
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]mbavu zangu mieeee

Binamu Warumi leo umesema ukweli bila ushabiki....

Ila domo uswazi+ubinafsi ndio tatizo
Tatizo domo ana roho ya kwanini sasa anataka tu yeye afanikiwe hafu bado hafichi ushamba na uswahili hajui kuwa yeye ni star, kanibore alivoanza kumshambulia ommy na maneno makali nadhani kosa la onmy ni kuzoeana na kiba na wema sepetu.

Habari wana jf samahanini napenda kuuliza bifu la ommy dimpoz na diamond lilianzaje?maana toka ommy dimpoz atoe nyimbo yake ya kajiandae ndipo bifu lilipoanza ila ilipotoka nyimbo ya rich mavoko bifu ndo lilikolea zaidi au ndo wanatafuta kiki?
d8fc2eed9ee0ee17dddf553ff082012d.jpg

Tatizo kubwa la Diamond ni uswahili na kujiona hizo pesa na mafanikio ndio kamaliza kila kitu hajui kuna maisha pia.
Kana dharau sana haka kajamaa si juzi juzi tu kalimdhalilisha ex wa Zari mtandaoni?? Huyo Zari nae atakua kaingia choo cha kiume kwa haka kajamaa sema ndo kakubali yaishe " chuna nikuchune"..
Ommy ameongea kwa staha na busara ya hali ya juu. Diamond apewe taarifa tu mr Nice nae alikua hukohuko juu na akina R.Kelly, Tyson wote pia walikua huko juu lakini sasa hivi ni watu wa kitaa.. kila mpanda ngazi hushuka pia..

Back
Top Bottom