Hivi interview afanye MUSSA, GEA HABIB, JOSE MARA bora kidooogo yule HUSNA hua anajitahidi.
Mussa ndio alimkalia kooni binti wa watu eti aseme ilikuaje akaelezea kidogo walivyokutana akaona haitoshi ooh nani alimuanza mwenzie kumtamkia, mara ooh alivyokuja ulimpokeaje, mara ooh ilichukua muda gani kuja kwa wazazi wako, mara ooh mwenzio ana watoto watatu je wewe una wangapi, mara ooh utamruhusu aoe mke mwingine? (hapa ndio walimkalia koon mdada wa watu anashindwa kujibu wamekazana tuu ikabidi Kiba aingilie kati hawataki mpk ajibu heee niliwashangaa sana)
Kuna siku Chriss Brown alishawahi kuvunja vioo vya studio kwa kulazimishwa aongelee kuhusu Rihanna wakati alisema hataki.
Kama mtu jambo lake hataki kuliongea asilazimishwe kwani wao ndio wanachelewesha interview na kufanya iwe mbaya.
Nilishaona interview ya Mimi Mars alisema maisha yake binafsi yabaki kua binafsi aulizwe kuhusu kazi zake, hata hao mashabiki wamempendea Kazi zake na sio maisha yake binafsi. Nilipenda sana jibu lake.
Ref: Jayz and Beyonce.