Unayumba sana aisee kwenye harakati zako za kuendelea kutetea RR.
Kwanza kwenye moja ya post zangu hapa niliitaja Lexus ambayo ni version ya Luxury version ya LC (just in case u ataka kufananisha upande wa luxury peke yake). Na nikasema hii ni luxury pia, reliable zaidi kuliko RR, na inakupa value ya hela yako maradufu. Ukweli ni kwamba LC 200, 300 na lexus version zake ni category 1 na RR, usihamishe mada. Hatufananishi na 70 series hapa wala prado.
Tukija kwenye matumizi, wala usilete kitu ambacho hata LR wenye kwenye hili tangazo wanakukana. Hebu anagalia hilo tangazo RR inapitishwa wapi. Halafu wewe unasema mtu akiinunua RR isitumike hivyo, ili tu kuiondoa kwenye mpamabano na LC. Kwa hiyo hapo wanavyoipitisha kwenye matope, maji na mawe walikuwa wanamaanisha nini, labda utusaidie na hapo. Na kumbuka hapa tunaifananisha RR na 300 au 200 huko, sio 70 series. 70 series itapambana na kina defender huko, na kwa hakika story itakuwa ile ile.
Waarabu wanapeleka jangwani LC kwa sababu rahisi tu kuwa ndo gari inayomudu huko, hizo nyingine wataenda kuziacha huko.
LC, Lexus zenye air suspension zipo labda kama huzijui, LC Uingereza hapo zipo tena manual kabisa. Sema tu Ulaya kwa ujumla wanatumia brand nyingi sana za magari.
Mwisho naona umetaka tusifananishe LC na RR, ajabu sana.