Leo kuna uzi unasema kuwa hawajamaa wamesha ungana. Pamoja na bwans Wetangula na bi Marha Karua.
Kwa wanaojua vizuri siasa za Kenya za Ukabila tupige hesabu hizi; Kama wakikuyu wote ambao ni 20% ya wakenya wote wakiungana na watu wa Ruto sijui ni ?%. Vs Watu wote wa Odinga ambao ni 12% na watu wa Kilonzo ?% na wa Wetangula ?% na wa Marha Karua sijui ni wa kabila gani na sijui wale wa miji kenda wa Jamhuri ya Mombasa wanaunga mkono nani . Mizani ya ushindi itakaaje kati ya makundi ya miunganiko hii?
Bwana AB TICHAZ anaweza kusaidia majibu.
Mkuu ngoja nikupe darasa dogo hapo juu.
Kuhusu hao mabwana wawili, nitasema ni Uhuru Kenyatta peke yake ndiye aliye na command ya kura
kubwa sana ya wakikuyu. Huyu Ruto hana nguvu ya kiasi hicho ukilinganisha upande wa wa Kalenjin.
Ukweli ni kwamba kuna uhasama flani kati ya haya makabila mawili kuhusu maswala ya ardhi tangia jadi.
Yule Rais wa kwanza hayati Jomo Kenyatta alinyakua mashamba kibao ya wa-Kalenjin na kuwagawia
wakikuyu. Hili swala limekua linasumbua mda mrefu na hata baada ya ile kura ya 2007 wa-Kalenjin wakaona
wamepata kisingizio cha kunazisha fujo la kuwatimua wakikuyu mitaa ya Rift Valley.
Baada ya muafaka kupatikana kulikua na maswala kadhaa yalichukuliwa kama ajenda kuu na ilikua ni muhimu
yashughulikiwe. Ishu mojapo muhimu ilikua swala la ardhi. Hata hivyo miaka mitano imepita na serikali ya
Kibaki haijafanya lolote in that regard.
Sasa leo hii Wa-Kalenjin vijijini wanaona huyu Ruto kwa kweli keshakua hayawani ikiwa anaingia mkataba wa
kura na Uhuru Kenyatta...mwanae Jomo Kenyatta aliyeiba mashamba yao!!!...Kwa ufupi, wakiungana na Uhuru
ndo basi tena, wasahau kama ardhi itarudi. Mtazamo wao ni kwamba Ruto kaenda kwenye huu mkataba peke yake
na hajabeba jamii ya wakalenjin. Wenyewe ilugha wanasema "Achicha Wendi kityo"...kwa ufupi huo mlima utaenda
kuupanda pekeyo...sisi hatumo.
Mtazamo wa pili ni kwamba wakenya kwa sasa wamechoka kutawaliwa na kabila moja na kwa sasa wanataka kitu
tofauti. Ukitazama kwa undani unaona pia kua huu ushirikiano kati ya Ruto na Uhuru ni kwa sababu wanaandamwa
na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC)...wanajua hii kitu sio mchezo kulingana na kwamba Kenya ilitia
sahihi mkataba wa ku-ratify ICC na huwezi ukajiiondooa kiholelaholela. The only way wanaweza ku-survive ni iwapo
watakua Rais na kukiuka sheria zozote za kimataifa kama vile Al-Bashir wa Sudan.
Ukileta swala la ukabila basi hapo ishu inaganda maana haya ni makabila mawili ambayo kwa akili zao fupi hawaoni
kama yale makabili mengine si yataungana against them? Hii ndio inaitwa conterproductive move ambao watajuta
nayo. Leo haya 'makabila mengine yanaelekea upande wa Raila Odinga na ODM na itakua vigumu kupambana na
wimbi kama hili.....Tazama picha zitakupa muelekeo.