iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

Sijabisha ila nakuahangaa umeikataa TECNO meikubali INFINIX wakati Tecno ina kamera nzuri zaidi kuliko hiyo INFINIX, Mimi mwenyewe iPhone sio mzuka wangu kabisa na hata ikitokea nimeiokota au kupewa nitaiza tu
 
Simu ni mpya while there's barely any additions with every iOS update. Lol[emoji38]
 
Nimevuta kiti nikajua unaleta madini
Hii si kwa geeks tu, inakuwaje kwa mtu wa kawaida ambaye hajui hata custom rom ni nini!? Kwenye iPhone inakuja notification ya update na unabonyeza mambo yanajipa

Geeks kitu gani, mbona ishu simpo tu unacheki youtube unafata maelekezo mambo yanajipa labda kama mtu ana kichwa kizito kama chako kinachoona haya mambo ni magumu, Sisi android ni kama community hatusubirii, Huko iPhone simu kama iPhone 6 plain hakuna notification za ku update simu inakuwa kopo tu, Pia hata huku android "notification ya update na unabonyeza mambo yanajipa"

At least iPhone 6S ni toleo la mwaka 2015 hadi sasa inapata support, hebu nitajie ni simu gani ya Android toleo la mwaka 2015 ambayo OEM bado anatoa support hadi leo.

Kma nlivyokwambia, Android ni Open source simu hata kampuni ikiacha kufanyia updates kuna custom roms kibao tu mtandaoni na ziko poa, Mfano nikushangaze kitu ??? Samsung galaxy s2 ya mwaka 2011 kuna rom zake za android 10, Huko iphone matoleo kama 3, 4, 5 na 6 yalishapigwa pini kitambo simu imekuwa kama kopo la chooni, point yangu inaendelea kutilia mkazo iPhone ni gereza


Iphone ni prestige goods zenye demand iliyokuwa affected sana na fashion na demographics, Hio simu yako huwezi kujitamba na wewe unamiliki iPhone mkuu!!, Ndio una iPhone ila ni ya kale sana, Ni kama vile katika kizazi hiki cha surauali nyembaba wewe unavaa bado masuruali mapana, bado hazijachakaa lakini unaonekana mshamba uliepitwa na wakati. Nilishasema mwanzoni kwenye point ya kwanza ya post kwamba hizi zsimu inabidi uwe vizuri kiuchumi, Matokeo yake ukilazimisha ndio hivyo tena, Jichange hata milioni 3 mkuu ukanunue mpya.
 
android mambo ni mengi mkuu, linganisha kimuonekano simu ya kampuni moja android ya 2015 na ya 2016,uataelewa ni kwanini ni upuuzi kukomaa na simu ya android ya 2015 mpaka leo. mbali na muonekano haiko compatible na mambo mengi ya mwaka huu, warranty yenyewe inataka miaka 2 mwisho, kama huwezi kununua flagship kuna matoleo andamizi ya kila mwaka.

leo hii una update simu yako kupata ios latest lakini hujui hata unapata faida gani, maana hata upate tatizo serious uko nje ya mkataba tayari.

muhimu kila mtu aenjoy anachotaka, ila haya mabishano huwa naona watu wa ios kama walipoenda walikwenda kwa jambo jingine kuliko lililopo, ndio sababu wanashindwa kukubali kwamba, ios imefungwa haina uhuru kweli, ila linapokuja swala kwenye vitu walivyoamua kuwapa, wamewapa kwa kiwango bora.
 
milion tatu kisa showoff, usilete utani bana.
 
Simu ni mpya while there's barely any additions with every iOS update. Lol[emoji38]
Mkuu wanasema tundu la iPhone ni old fashion πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, Mkosaji hakosagi maneno

Simu ikikaa chaji kidogo wanatetea hii simu sio ya mtu mwenye mambo mengi

Kabla ya iPhone kuwa na line mbili wakawa wanazuga line moja kwa smartphone inatosha huku wakiwa na vitochi vya kuwekea line za pili

Simu haiweki ringtone unayotaka wametia mkazo na visingizio vile vile..

huwa nawauzigi sana hawa watu ofisini wakianzishaga mabishano ofisini, Huwa nawaziba kabisa mdomo yani ni kimya hakuna kuendelea mabishanoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
saa hizi wana face id[emoji38][emoji38], 2022 wanakuja na ultrasonic fingerprint kwenye display, utaona iship watakavyolipuka kwa vigeregere.
 
milion tatu kisa showoff, usilete utani bana.
Wadau wanashindwa kuelewa kwamba iPhone ni simu ambazo inabidi uende nazo sambamba, Sasa mtu tangu mwaka 2016 alivyojibana kununua iPhone anayo hadi leo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. Nilishaweka wazi pointi ya kwanza hii simu kama haupo vizuri kiuchumi utapitwa sana na matoleo mengi.

Huku android wenye uchumi wa chini wanaenda sambamba na matokeo ya simu hizi za laki hadi laki 4, wenye uchumi wa kati wanakwenda sambamba na matoleo ya hizi simu za laki 4 hadi laki 8, Mapedeshee nao wanakwenda sambamba na simu zao zinazocheza kwenye milioni na kuendelea.

Uzuri wa android hata ukifulia unakuja huku kwenye simu za laki na kama kawaida unaenda nazo sambamba, Huko iPhones ukifulia hakuna mbadala labda ununue matoleo ya zamani kwa simu za mitumba, Kuna mtoa mchangiaji humu ana iPhone 6s tangu 2016 yawezekana uchumi umeyumba akaona abaki na hio simu mpaka leo, Dadaeki simu ya iPhone latest milioni 3 kibindoni kuna laki 5 tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
saa hizi wana face id[emoji38][emoji38], 2022 wanakuja na ultrasonic fingerprint kwenye display, utaona iship watakavyolipuka kwa vigeregere.
2022 apple atatua tatizo alilotengeneza mwenyewe na kujisifu kaongeza feautures, anaweza kurudisha tundu la ear phone mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na earphone za waya zikaanza kuuzwa laki 3
 
[emoji38] [emoji38] sasa mpuuzi mmona ana laki 7 anaacha kwenda kuchukua a51s ale maisha, anakwenda kuparamia kifungo cha iphone 7plus.anasahau ameachwa na simu 6 mbele, ili asimame na wanaume.
 
2022 apple atatua tatizo alilotengeneza mwenyewe na kujisifu kaongeza feautures, anaweza kurudisha tundu la ear phone mkuu [emoji23][emoji23][emoji23] na earphone za waya zikaanza kuuzwa laki 3
ila kusema ametoa ile jack kwa kuongeza nafasi ya betry, huu uongo hata ccm bongo hawafanyi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mimi nina unlimited internet access, na muda mwingi natumia Wi-Fi.

Lakini simu ambayo hairuhusu hata SD card kwangu naona ni ya kijima.

Simu yangu ina space 128 GB.

Halafu nimeweka SD card ya 512 GB.

Jumla 640 GB.

Hapo nina nafasi kubwa sana ya kuweka vitu vyangu vingi sana. Na kwenda navyo hata sehemu isiyo na internet nikaendelea kuwa na access.

Na hapa nasubiri SD card za 1TB ziwe affordable niweke 1TB SD card kwenye simu yangu.

Kwenye iPhone unaweza kuweka SD card?
 
Nashukuru mkuu kwa uelewa wako, mleta mada angekuwa anajua kuwa kila mtu anaenjoy anachokipata wala asingeleta uzi wa mabishano kama huu, kuna watu wanapenda kula pili pili na ndio starehe yake lakini hakuna mtu asiyejua kuwa pili pili ni kali, hivyo hivyo usichokipenda wewe sio lazima mtu mwingine asikipende pia
 
IPhone hawana hiyo feature wao wamejizatiti kwenye internal pekee kuanzia betr, memory nk. kila jambo wao wameliwekea kipengele.

Iphone sometimes ni kama vazi la nyelamumu, ishu ndogo tu ya dakika mbili inaweza ikakulazimu uvue bwanga lote

Na kuna iPad ambazo hazitumii hata simcard lakini bado wazee wa mkumbo utawaona kitaa wamenata.
 
Geeks kitu gani, mbona ishu simpo tu unacheki youtube unafata maelekezo mambo yanajipa
Ha ha ha hah πŸ˜‚ πŸ˜‚ user wa kawaida unawajua lakini?
labda kama mtu ana kichwa kizito kama chako kinachoona haya mambo ni magumu,
Duh, tayari umeshaanza kuni insult kitu ambacho sikutegemea, nilijua tutaenda hoja kwa hoja
Sisi android ni kama community hatusubirii, Huko iPhone simu kama iPhone 6 plain hakuna notification za ku update simu inakuwa kopo tu, Pia hata huku android "notification ya update na unabonyeza mambo yanajipa"
Naona umekomaa na iPhone 6 tu, hujajibu hoja yangu, ni OEM gani android anatoa support at least hata miaka minne tu kwa simu hata hizi flagship?
Nimekuuliza vipi kuhusu users wa kawaida ambao hata hawajui nini maana ya ROM, achana na makopo ya chooni
Iphone ni prestige goods zenye demand iliyokuwa affected sana na fashion na demographics, Hio simu yako huwezi kujitamba na wewe unamiliki iPhone mkuu!!,
Ha ha ha ha haaaah, πŸ˜‚πŸ˜‚ kumbe basi namiliki kopo la chooni kama unavyooita wewe? nilikuwa sijui
Ndio una iPhone ila ni ya kale sana,
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ yaani nashindwa kukuelewa mkuu, mbona umepanic hivi, sielewi unasimamia wapi, namiliki iPhone au similiki?
Ni kama vile katika kizazi hiki cha surauali nyembaba wewe unavaa bado masuruali mapana, bado hazijachakaa lakini unaonekana mshamba uliepitwa na wakati.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Nimegundua bila kuni insult huwezi kujenga hoja ya maana, anyway simama kwenye mada achana na masuruali
Nilishasema mwanzoni kwenye point ya kwanza ya post kwamba hizi zsimu inabidi uwe vizuri kiuchumi, Matokeo yake ukilazimisha ndio hivyo tena, Jichange hata milioni 3 mkuu ukanunue mpya.
Hili ndilo tatizo la kukariri, unataka kuwaambiaje watumiaji wenzio wa simu za Android kama Samsung ambao wanatumia simu za laki mbili ilihali kuna simu kama Galaxy Fold inayouzwa zaidi ya 3M? Kama unanunua simu kwa fashion basi usidhani kila mtu mwenye simu kanunua kuendana na fasion, mimi binafsi nanunua simu au kitu chochote kulingana na mahitaji yangu, hii iPhone 6S niliyonayo inakidhi mahitaji yangu wala sihitaji simu ya 3M na mi siyo mtu wa fashion

Ukiniquote hii comment ukajibu kwa hoja zenye maana tutakwenda hoja kwa hoja, vinginevyo kwaheri
 
[emoji38] [emoji38] sasa mpuuzi mmona ana laki 7 anaacha kwenda kuchukua a51s ale maisha, anakwenda kuparamia kifungo cha iphone 7plus.anasahau ameachwa na simu 6 mbele, ili asimame na wanaume.
Kama ni mtu wa fashion ni sawa ila kama ndo inakidhi mahitaji yake kwa nini anunue kitu ambacho hakihitaji?
 
Duh, kwa hiyo mtu akikwapua simu ndo basi keshakimbia na mzigo wote
 
Nadhan point ni kuwa android users hawaweki simu zao kwa muda mrefu zaidi ya miaka mi 3. Android phones are getting cheaper every year and better. So hata OEMs hawahangaiki na ku support simu miaka zaid ya mi 3 sababu percentage ya wanaokua bado wanazitumia ni ndogo sana.
Kwa mfano galaxy s8 ilikua ni simu gatari sana ilivyotoka na ilikua inauzwa almost 2M. Miaka imeenda now hyo simu tayari inapitwa mambo mengi sana na Midrange phones kma Galaxy A50, A51, A70, Xiaomi redmi note 9 pro, nk ambazo brand new ni sawa na s8 refurbished dukani. Ni wachache sana watakao chagua kununua hyo s8 compared to other alternatives brand new for about the same price.

Kwa iPhones yaan ni matoleo machache tu every year na tofauti ya bei kati ya hayo matoleo ni ndogo sana. Mtu akiangalia kununua iPhone 7 plus na iPhone 11 anaona bora achukue tu iPhone 7 sababu hamna brand new alternative iPhone kwa bei ya iPhone 7 refurbished.

Android phones get cheaper every year (ukiachana na huyu mpumbav samsung aliyeamua kupandisha bei ya flagship zake mwaka huu na kuzitoa features kma hi note 20. Takataka kabisa) while still getting better. Mtu haoni umehimu wa kuweka simu lake la zamani wakat mpya zimetoka na bei ndogo kuliko aliyonunulia yake miaka hiyo na zina features nyingi nzuri zaidi.

Sema tunapoenda huku mbeleni android versions hazitakua na maana sana. Sababu Google ameamua kufanya security updates kuwa modular na kuweza kuwa installed kwenye simu zote bila OEM kuhusika (Google Project Mailine) na pia Google play services inaleta features mpya kila mara hata kwa simu hata za zamani.
Mfano:
1. COVID exposure notifications zimeletwa bila kuhitaji version update yoyote wakati on iOS walihitaji version update nzima
2. Nearby share (mbadala native wa Airdrop kwa simu za android) inaletwa kwa kupitia Google play services(GMS) kwa simu zote kuanzia android 6+
3. Bedtime routines imekuja pia kupita GMS
4. Earthquake alerts
5. Android emergency location service (kwa baadhi ya simu ukipiga emergency number kama 911 itakuonesha na kuwatumia location yako bila wewe kuangalia)

Hzo ni baadhi tu ambazo zimekuja bila hata version update yoyote kutoka kwa OEM. Straight from Google. Tunakoenda huko version updates hazitakua na maana tena kma ilivyo windows 10 sasahv.

Nadhani tunaweza jadiliana vizuri tu bila kutukanana.
 
Huu ndio ujengaji wa hoja sio mtu akishindwa kujenga hoja anaanza kukutusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…