iPhone kweli ni simu kali sana ila watumiaji wake wengi ni washamba wanaodhani kutumia iPhone kunawaweka kwenye daraja la juu!
Nakumbuka kisa kimoja mwaka 2019 nilikuwa Bar na washkaji zangu kadhaa, kati yetu hapo wawili walikuwa na iPhones, ghafla ukaanza ubishi wa simu hapo...wale jamaa wa iPhone walijitamba sana kuwa simu hizo hazitumiwi na wachovu kama sisi lazima uwe na pesa ya bundle n.k. ghafla si muhudumu akaleta Bill ikiwa inasoma 160k na kuendelea....hamtaamini wale jamaa wa iPhone hawakuwa hata na 20k kila mmoja mfukoni mwao ili hata wachangie bill.... So embarassing! Aibu yao niliiona mimi.....
Sio wote wenye iPhone wana maisha mazuri, zile simu zinapumbaza sana vijana....kuna wachache wanastahili kuzimiliki ila wengine ni mkumbo na kupeana stress tu