G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Upo uwezekano kuwa mzee wetu Alli Hassan Mwinyi alipewa uongozi wa nchi bila kuwa na upeo imara wa kiuongozi.
Tofauti kabisa na wazee wenzake, huyu amekuwa hata haelewi umuhimu wa uwepo wa katiba Tanzania. Haelewi maana ya uongozi wa katiba katika nchi.
Ni aibu kwa mzee kama Mwinyi ambaye anatazamwa kama kiongozi baba wa nchi aliyebakia akihimiza eti katiba iende likizo kwa muda ili jambo ambalo kimsingi hata halina maana lifanyike.
Ni aibu kubwa kumpa jukwaa huyu mzee kisha anaongea haya huku ikiaminiwa kuwa aliwahi kuwa Rais wa nchi tena chaguo la Mwalimu Nyerere. Ndiyo maana huwa nabakia kujiuliza sana uko wapi umakini wa baba wa taifa tunaoaminishwa kama tu alituletea mrithi wa hovyo kama mzee Mwinyi.
Ni katika utawala wake tuliwahi kuwa na naibu waziri mkuu asiyetambulika kikatiba. Hivyo sina wasiwasi kuwa anamaanisha ayasemayo. Huyu mzee ni heri asiwe anapewa kipaza sauti kuongea, aachwe apumzike na uzee wake!