Ipi faida ya Mzee Alli Hassan Mwinyi kuwepo Dodoma kama Baba wa Taifa aliyebakia?

Ipi faida ya Mzee Alli Hassan Mwinyi kuwepo Dodoma kama Baba wa Taifa aliyebakia?

Kiukweli, nami nimejiuliza sana alichokiongea, sijui ni nini hiki!
 
Mkuu, huyu Mzee ni wa kumsamehe bure tu, kwa kuwa alitamka hivyo kwa kusukumwa na mhemuko uliotokana na mwanaye kuweza kuchaguliwa kuwa mpeperusha bendera wa nafasi ya uraisi kwa upande wa Tanzania Visiwani. Hili lilikuwa ni tamanio lake la muda mrefu, na hivyo kuona kuwa amepewa upendeleo mkuu.

Pia ukweli ni lazima uwekwe wazi, ktk michakato ambao CCM iliweza kutuletea viongozi pasipo kuchukua tahadhari yoyote ile, ilikuwa ni kipindi cha awamu ya kwanza na hatimaye Mzee Mwinyi akaingia madarakani. Na pia katika kipindi cha awamu ya nne na hatimaye Mheshimiwa wa sasa akaingia madarakani.

Lakini jambo moja linanishangaza na kunifanya niweze kutafakari kwa kina zaidi. Majina ya kwanza ya Rais wa awamu ya kwanza lilikuwa ni Julius, awamu ya nne lilikuwa ni Jakaya, na awamu hii ya tano ni John. Japo mimi si mpiga ramli, lakini huu mfanano wa herufi za kwanza za herufi "J" ktk majina yao, zinatupa "general rule" kuwa hawapo makini kusimamia vyema michakato ya kutuletea warithi wazuri wa nafasi za pale wanapostaafu. Kwa pengine hata kwa John tutegemee mambo kama hayo.
Awamu ya sita Kuna J mwengine anapiga jaramba [emoji3][emoji3] nadhani anajulikana na Ni presidential material

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuwa chaguo la Nyerere. Watu wazima wanalijua Hilo.
 
Mkuu unaweza kuwekea nukuu au sauti yake halisi mahali ambapo amesema(amehimiza) "katiba iende likizo"?
Mbona mara zote amesema inawekana kubadili katiba.

Nafasi ya kubadili katiba ipo kisheria, katiba inaruhusu utaratibu wa kufanya mabadiliko ya katiba iwe maboresho madogo au kuandika mpya.
Tuache watu watoe maoni yao kama tunavyodai uhuru wa kutoa maoni.

Kanini mnakuwa madikteta kwa kukataa wengine wasitoe maoni yao?
Suala la msingi hapa iwapo maoni ya wengi yataheshiiwa kikatiba hata kama wewe na mimi hatupendi hayo wanayotaka wengine tofauti na mitizamo au misimamo yetu.

Kwani maoni yake ni maamuzi ya serikali? Acha atoe maoni kisha watu waamue kama yana tija au la.

NB: Mimi sitaki kabisa habari ya kubadili katiba. Naamini litakuwa moja ya makosa makubwa sana kuwahi kufanywa na Mh. Magufuli.
Tukumbuke mtizamo wangu siyo sheria au ndicho kitu sahihi. Naweza kuwa sipo sahihi kabisa.

Kuna mtanzania ambaye hajui kuwa katiba inaweza kubadilishwa brother !!...

Mbona mchakato ulikuwepo na ulikula billions of shillings ila toka 2015 hadi leo ni kimya kirefu maana kila mtu anajua misingi ya katiba iliyotarajia kupitishwa..

Katika bunge la kutoa pongezi kwa JPM, issue ya kubadili vifungu vya katiba ikaibuliwa tena lakini sio kama muendelezo wa mchakato uliopita ila kubadili kifungu cha ukomo wa madaraka ilhali issue hii haikuibuliwa kama drive ya mchakato wa awali..

Watu kwa sasa naona wanapinga hii kitu sio kwa sababu hawataki katiba ibadilishwe ila wanapinga dhima ya sasa iliyopo..

Hicho ndicho nachokiona.. i stand to be corrected
 
Yaaani mtoto wake kupitishwa na Magufuli kugombea uraisi Zanzibar anaona basi taifa lote tumtunuku magufuli kwa kumzawadia miaka mitano zaidi. This is very stupid kwa kweli.

Hadi wajumbe wa CCM walianza kumshangaa na walikuwa wananong’ona sana. Kama anakata kumshukuru Magufuli kwa kumpitisha mtoto wake kwenda kugombea Zanzibar basi amshukuru peke yake sio Eti kushauri taifa tuvunje katiba.

Kwa mara ya kwanza niliona hadi Magufuli alijishtukia akachomekea mzee amalize kuongea.
Anataka wamalize uongozi pamoja na mwanae maana Hussein anaanza miaka 10 na Magufuli kabakiza Miaka 5.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom