Ipi inalipa kati ya Reustarant na M Pesa?

Anzisha ka-take away kwa mil. 5. Hapo pembeni weka Mpesa n.k. Biashara ya chakula inalipa sana lakini LAZIMA uwe na wapishi wazuri na wahudumu wanaoweza kukaribisha wateja vizuri. Ndio maana nimekuambia uanze na ka take away kenye chips, soda, juice, supu. Wateja wakizidi uingie sasa kwenye vyakula vya restaurant. Lakini uwe na eneo la kutosha ambapo wateja ni wengi kulingana na chakula unachopika
 
Biashara zote hizo ni nzuri sana na zina faida sana tu ila kinachohitajika ni location nzuri na uwezo wa kukabiliana na changamoto. Kingine labda nikupe nyongeza ,, biashara nyingne inayolipa vzr kbs ni biashara ya vinywaji vya jumla (pombe, soda, maji etc)
 
Kulipa kwake inategemea na mazingira unayotaka kufungua biashara yako.
 
Asanteni wadau,jukwaa hili nalipenda sana,lina watu makini na siyo wakuruukaji,wanaakili sana
 
Hizi risk zilishawahi kunikumba, dogo niliyemuweka dukani alivamiwa na majizi yenye silaha na kumpokonya cash yote pamoja na simu mbili zenye tilly,

Dogo alikatwakatwa mapanga almanusura afe, tena uvamizi huo ulifanyika saa 2 usiku tu.

Hatari sana,
 
Da anyway kuvamiwa unaweza kuvamiwa popote hata usipokuwa mfanya biashara ila la msingi ni wapi unafanya biashara ila la msingi ni wapi unafanya na muda walau ikiwa mwisho saa mbili inakuwa sawa inategemea na aina ya biashara unayofanya
 
Ila najua mwisho uliendelea na business coz hawakukomba mtaji walikomba faida ya siku hiyo pekee
 

Mgahawa ni risk sana, unatakiwa ubahatishe location nzuri, usafi na resonable price ya msosi...changamoto inayokuja ni gharama kubwa za kudesign restaurant yenye hadhi...!!! competition ya mama ntilie waliozagaa kila kona na misosi yao ya buku ni shida nyingine na mda wote wanawaza kwenda kwa mganga tuu wakuharibie,kuvunjika kwa vikombe na glass kila sku, kupata wapishi wenye viwango... ...weather condition nayo huleta hasara sana mfano kipind cha mvua za asubuhi mpak jion hufukuza wateja...na hapo wafanyakazi wanataka chao, na vyakula vingi vikilala bila kuliwa ni mziki mwingine...Hii biashara stress sana...Faida utaipata ukipata location safi yenye watu wa mahofsini wengi (permanent customers) na msosi wako uwe wa ukweli with reasonable price... 24 hours uwe eneo la kazi...mana cashier akipiga hata 5000 umeumia.....

KILA LAKHERI MKUU...
 
Biashara inayolipa mkuu ni ya vyakula hayo mambo ya Mpesa matapeli wengi ukipata kuibiwa siku moja unaweza kuvunja Mtaji wote lakin Restaurant ukipatia Location nzuri hasa maeneo karibu na Vyuo vikuu au Ofisi Ofisi au Karibu na Soko Kubwa mkuu huwa inalipa sana!!
 
Kama ulikuwa kichwani mwangu yaani,nimegundua hilo na hilo.limenipa wasi hadi nikaanziha uzi kwani nimeona restarant hata muhudumu akiiba hawezi kuiba mtaji lakini Mpesa anaweza akakupiga mtaji within a day
 
Unariski vp na ile ni biashara pesa kwa pesa? Biashara ikibuma unaondoka na mtaji wako unaangalia mambo mengine, restaurant, biashara ya viduka vya reja reja ndo pasua kichwa mkuu. All in all location ndo matter
Mkuu iyo point, unasemaje mpesa ni risk while mtaji uko nao mkononi? Kama ni usalama watu wangapi wanatembea na hizo laki nane mpaka million at once?

Labda Kwa waajiriwa risk waliyo nayo ni watu wanao waweka kukimbia na pesa hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalia fursa ya kule Chongoleani Tanga kwenye bomba la mafuta.

Tafuta eneo, jenga kibanda cha muda (kumbuka bomba litachukua zaidi ya mwaka kujengwa), na uanze sasa biashara ya mgahawa.

Ni lazima wewe mwenyewe uswepo na usimamie na uajiri wasichana na wavulana wachache wa Tanga wakusaidie kupika misosi na chai ya mkandaa.

Pia uwe huishiwi bidhaa yaani unatawala soko.

Yaani hiyo milioni 8 yatosha kabisa hiyo.

Bomba likikamlika unavunja kambi na unarudi ulikotoka au utakuwa umehamia kabisa huko Tanga.

Karibu Tanga.

Hakika nakuambia, hutajuta.
 

Baada ya kitambo hicho uliamua kipi na unapimaje mwenendo wake??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…