Nikusaidia kidogo, risk za M-PESA ni kwamba
1. Wahudumu wa M-PESA toka Vodacom wengi wao ni wezi, hivyo wakati wa kutoa commissiob mwisho wa mwezi huwa wanakuibia sana...hata uwe makini vipi wao wanaweza wakaweka ukaiona SMS alafu wanaitoa hiyo commission bila kuleta SMS na huwezi gundua.
2. Biashara hii inawindwa sana na majambazi, fuatilia matukio yake....unaweza kuuawa kwa shilingi laki 2 mbili. Wanakuja kukuvamia....jilinde kiusalama
3. Mtoa huduma utakayempatia laini akusaidie anaweza kukuibia au akatokomea na pesa zako kusiko julikana
4. Hii biashara inabidi umuelimishe mkeo sana kuhusu biashara hiyo...maana utakuta mwenzio anaona una pesa nyingi hivyo kuamua kufanya matumizi yasiyo yalazima hatimae mtaji ukaisha
5. Nasisitiza tena wizi wa pesa mtandaoni unafanywa na wahudumu wa M-PESA/Tigo pesa etc...hapa ndio panawavunja sana moyo agent wengi....yaani unaweza ukafanya miamala mingi sana kwa mwezi lakini ikija kwenye malipo ya commission utashangaa...uwe muelewa sana wa biashara hii ya pesa nakusihi sana!