Ipi lugha sahihi ya kujifunzia

Ipi lugha sahihi ya kujifunzia

TIASSA

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2014
Posts
2,926
Reaction score
3,530
Wasalaam wandugu.

Kumekuwa na mjadala siku nyingi kuhusu lugha gani hasa Hapa Tanzania itumike kujifunzia mashuleni hadi vyuoni, hapo kuna aina mbili za mawazo.

Walewanao sema kiswahili kitumike wanasema hivi..

1. Wanafunzi mashuleni wamekuwa wakifeli kutokana na kutoelewa lugha ya Kiingereza vizuri. Na kwamba mtu anapofundiswa kwa lugha mama ni rahisi zaidi kuelewa.

2. Kiswahili ni lugha ya taifa, NCHI mbali mbali kwa mfano china urusi wamekuwa wakitumia lugha zao wenyewe kujifuzia kwahiyo ni vyema Tz nayo ikatumia lugha yake ya kiswahili.

(3) kutumika kwa kiswahili kama lugha ya kujifunzia, kutakiendeleza kiswahili na kukifanya kuwa lugha bora zaidi. Mfano kutaongezeka misamiati na pia watumiaji wa lugha wataongeza. Kwakuwa wale wageni watakao kujakusoma nchini watajifunza kwa kiswahili.

Wale wanaosema Kiingerezaa wanasema hivi.

(1) Kiswahili bado hakina misamiati mingi ya kisayansi.

(2) Kiingereza kinatumika zaidi dunia asilimia 99% YA biashara zote duniani hufanywa kwa Kiingerezaa.

(3) Kiingereza kinawatumiaji wengi zaidi duniani karibu 70% ya watu wote duniani wanatumia Kiingereza

(4) Kiingereza kikitumika kufundishi haita kipoteza kiswahili bali kiswahili kikitumika kitakipoteza Kiingerezaa.

(5) kutafsiri material yote ya Kiingereza kwenda kiswahili ni gharama kubwa

nini mawazo yako kuhusu ipi lugha sahihi ya kufundishia kati ya kiswahili na Kiingereza.?
 
Vitumike vyote viwili, pale penye maana pana kwa lugha ya kiingereza basi kitumike kiingereza,pale penye uhitaji mkubwa wa kiswahili patumike kiswahili, Alternative way ipo!!!

Serikali ianze mkakati wa muda mrefu wa kukirasimisha kiingereza(kama ilivyo south africa)na wakati huo huo itengeneze mfumo elimu utakaoweza kutumia lugha zote mbili kwa wakati mmoja!hii itasaidia zaidi kwa kuwa mwanafunzi ataweza kuchukua sentensi anayoielewa vyema kutoka kwenye kiingereza,akainyumbulisha kwa kiswahili,kisha akatoa jibu kwa kiingereza anachokijua!!!

Tukiweka mikakati makini tutaweza ndani ya miaka miwili tu!! SA ina lugha rasmi zaidi ya tano!! Na mambo yanaenda vyema sana tu! Why not us?
 
Dunia ya utandawazi hii pampja na kuendelea kukipa kipaumbele Kiswahili lakini wakati huo huo kiingereza kinabidi nacho kipewe kipaumbele kinachostahili.

Na kwa mani yangu kufanya hivyo hakutafanya Kiswahili kidharaulike. Wanafunzi wa baadhi ya nchi za Western Europe wanaongea lugha 3 hadi tano (Kiingereza, Kifaransa, kidachi,

Kijerumani na labda lugha moja wapo kutoka Scandinavian countries) kwa ufasaha mkubwa sioni kwanini Wanafunzi wa Kitanzania washindwe kuzitumia lugha hizi mbili kwa ufasaha mkubwa.

Kuacha kufundisha Kiingereza mashuleni ni kosa kubwa sana ambalo litazidi kuwaacha wanafunzi wa Kitanzania nyuma zaidi ulinganisha na wale wa nchi za jirani.

Seikali hii kama kawaida yake imekurupuka na kuja na sera ya elimu ambayo badala ya kuinua elimu nchini itazidi kuidumaza.
 
Imefika wakati inabid tuache siasa katika masuala ya msingi hivi kweli hadi kidato cha nne lugha iwe ni Kiswahili taifa linaenda wapi kama sio shimoni, wanafunzi hawa watajuaje lugha muhimu ya kiingereza.

Watoto wenyewe wa kitanzania inajulikani walivyo mbumbumbu sasa mkitoa hiyo mitihani na uhakika hakuna mwanafunzi atakae kuwa anasoma. Ebu nyie mnaotunga sera mfikirie sio kukurupuka.
 
alexis jr

Sioni tofauti yetu na nchi kama Malawi, siera Leone na zingine ambazo zinatumia Kiingereza tangu awali.

Kuwapa watu maarifa na kuwafanya wajue Kiingereza ni mambo mawili tofauti, tukizungumzia maarifa tunaumia pakubwa kwa kutumia lugha ambayo si yetu hatuimudu, tunaumiza watoto wetu ambao tunawabatiza ukilaza kwa kuwa tu wameshinda kusema kwa ufasaha lugha ya wakoloni.

Tuwape maarifa kwa lugha yao ili wayaelewe, kisha kama kujua Kiingereza ni muhimu, tunaweza kuwafunza!
 
Last edited by a moderator:
CCM oyeeee maana hamna neno umeambiwa lugha itakayotumika ni kiswahili we ukibisha utapigwa tu maana hamna namna nyingine ya ku implement hii sera
 
Mphamvu;

kwahiyo na ICT itakuwa inafundishwa kiswahili? kingeleza nacho kitafundishwa kwa kiswahili
 
Last edited by a moderator:
kwahiyo na ICT itakuwa inafundishwa kiswahili? kingeleza nacho kitafundishwa kwa kiswahili



Kiingereza kitafundishwa kama international language kama Ilivyo kwa nchi Zote za ulaya isipokuwa uingereza.

Pia huwezi kuendelea kwa lugha ya kukopa. Fikiri juu ya upeo wako...utafakari japani, china na nchi zote za ulaya ambazo zimeendelea kwa kutumia lugha zao.

Hata south africa makaburu hawakuijenga kwa kutumia kiingereza bali lugha yao-africaana. Usisahau urusi. Na nchi zingine hata zinazotengene,a atomic bomb kama Iran,korea na hata israel wanatumia lugha zao si lugha za kukopa
 
Utingo

Una mawazo ya kimapinduzi ingawa wengine ni vigumu kukuelewa.
 
Last edited by a moderator:
alexis jr;

Kiingereza kitafundishwa bana kama lugha. Mbona waTz wagumu kukubali vyenuuu.
 
Last edited by a moderator:
Utingo

Una mawazo ya kimapinduzi ingawa wengine ni vigumu kukuelewa.

mkuu si uanamapinduzi...tatizo na shida yangu kubwa ni kuipenda nchi yangu kupita kiasi....mtu anayepinga hili ninamshangaa...ninasema hivi kwa sababu watu wengi leo wanasoma google kwa kiswahili...nami ni mmoja wa watu waliotafsiri terminology za google kwa kiswahili na sasa inaeleweka mtandaoni.

Shida ninayoiona kwa mfumo huu ni kwamba serikali inatakiwa isisitize sana lugha ya kiingereza kama lugha ya kimataifa ili lisiwapo "gap" kati ya watakaosoma academy schoo na watakaosoma shule za serikali ili watakapofika form five wote wawe na uelewa sawa wa lugha. Uwepo msisitizo kama wa masomo ya sayanzi na hisabati.
 
Nimeamua kubadilisha msimamo wangu na kuungana na wanaosema kua kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia.
Nakumbuka nilipokua form flani, nilipokua nakariri sentensi bila kujua maana yake na kwenda kujibu mtihani na kufaulu. Baada ya muda mfupi tu, vitu vyote vinapotea. Nilipata shida sana. Niseme ukweli tu, kuna vitu vingine nilikuja kuvifahamu zaidi baada ya kwenda 'levo' za juu.
Nakumbuka pia nilipomaliza form 6, nlienda kufundisha kwa muda katika shule fulani. Nilikua natumi kiingereza kwa muda mrefu. Kitu nilichokiona ni kwamba, unaweza kuona wanafumzi wakodoa macho wakionyesha kutoelewa. Mara utapofafanua kwa kiswahili, utawaona wakinong'ona 'aaaaaa, kumbe ndio inyo'. Hii ina maana kwamba wanafunzi walikua wanaelewa zaidi pale nilipokua natumia kiswahili kufafanua jambo fulani.
Kuhusu kutotoeka kwa kiingereza, ni vyema mamlaka husika ilifanya somo la kiingereza kuwa SOMO MUHIMU kama hisabati ilivyo sasa.
Ifahamike kua asilimia kubwa ya wahitimu wetu sasa wanafeli zaidi. Baahati mbaya pia, asilimia kadhaa ya waliofaulu, nao wamekarii na sio kuelewa.
Tujiridhishe kwa kuangalia matokeo ya kiswahili na masomo mengine. Bila shaka matokeo y kiwahili niazuri kuliko masomo mengine.
Pamoja na kua wapo wanaofeli hata kiswahili, ila hii inasababiswa na KUKATA TAMAA kunakosababisha na kufeli zaidi katika masomo mengine, na sio ugumu wa kiswahili chenyewe.
Tanzania yangu, kiswahili changu!
 
hyo sera kutumia kiswahili kamA lugha ya kufundixhiA waLa siungI mkono kwanI hao tunaojfananishA nao kama japan,china,urus,iran walishapga hatua ktk teknolija wanauwezo wa kutengeneza chochote kile sasa kwetu ni blaa blaa tu mainjia wapo weng lakn hawawezi kuunda chochote zaid ya kufanya repair vtu vilivyoundwa na wenzetu.
 
hyo sera kutumia kiswahili kamA lugha ya kufundixhiA waLa siungI mkono kwanI hao tunaojfananishA nao kama japan,china,urus,iran walishapga hatua ktk teknolija wanauwezo wa kutengeneza chochote kile sasa kwetu ni blaa blaa tu mainjia wapo weng lakn hawawezi kuunda chochote zaid ya kufanya repair vtu vilivyoundwa na wenzetu.

Hao wahandisi unaowataja eti hawana lolote ndio hao waliojifunza kwa kiingereza na kukariri mambo badala ya kuyaelewa. Sasa ili waweze kuunda kitu, wanatakiwa waelewe mambo kwa undani zaidi na sio na sio kukariri. Kama kiingereza kimeshindwa kusababisha mtu kuelwa vizuri vitu kwa undabi ili aweze kuunda vitu, basi kikae pembeni na kiache kiswahili kifanye kazi hiyo.
Kuhusu kuongea 'this is a pencil' tutajifunza taratibu, wakati huo huo tukiwa tunaelewa kwa undani ujuzi tunaoupata kwenye masomo mbalimbali, ili utusaidie kuunda vitu mbali mbali!
 
Coni mantiki ya kushabikia kiingereza wakati wengi wetu tuliobahatika fika mpk univ tulifaulu kwa kukariri tu. Ukimchukua mtu kuzungumza hapo ni tatizo kubwa. Sasa ni bora kikaingia kiswahili ili naona itasaidia kuelewe badala ya kukariri.
 
Back
Top Bottom