Ipi ni akili nzuri: Kutumia trilioni 7 kusambaza maji safi kila nyumba nchi yote au kuweka treni ya mwendokasi Dar mpaka Mwanza?

Unayosema ni sawa kama reli itaendeshwa kwa ufanisi na mapato kusimamiwa vizuri. Kinyume cha hapo, ni kama pesa itakuwa imetupwa tu..!
 
Hayo ma Sgr ni upuuzi mtupu.Til.7 ni sawa na km 70,000 za lami Nchi nzima
 
Miaka yote ambapo hapakuwa na treni ya mwendokasi mbona hapakuwa na maji? Ukishasambaza hayo maji then what? Ila ukirahisisha usafirishaji na kuokoa pesa kwa kupunguza gharama, hiyo pesa unaweza kutumia kusambaza maji
 
Inasikitisha sana kuona kuna vijana hata akili hawana!
 
Hawatakubali hawa watu, walishanunuliwa kitambo ndiyo maana chuma inatoka kila kukicha kwenda kwa mabwana wakubwa wao
 
Unajua uchumi wa nchi unajengwa kwa namna ya ajabu ambayo ukifirikia kwa haraka haraka unaweza dhani viongozi wanazingua. Huo mradi ni catalyst (kichochezi) ni mradi utakachochea maendeleo mengine katika sekta zengine.

Kukiwa na usafiri wa uhakika kutoka dar mpaka mwanza kupitia morogoro sekta ya utalii itakuwa, mbuga zilizopo morogoro, vivutio vyote vilivyopo mkoa hii reli imepita vitakuwa na moja ya sababu ni uwepo wa huu mradi.

Mradi wa SGR utapelekea sekta ya uwekezaji nchini ikue. Pia mradi utatoa ajira kwa watanzania. Watu hawaelewi? Au hawawazi? Kazi yao kuponda tu. Mimi sio CCM lakini jamani kabla ya kuongea em shirisha ubongo wako kwanza.

Narudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…