Ipi ni akili nzuri: Kutumia trilioni 7 kusambaza maji safi kila nyumba nchi yote au kuweka treni ya mwendokasi Dar mpaka Mwanza?

Ipi ni akili nzuri: Kutumia trilioni 7 kusambaza maji safi kila nyumba nchi yote au kuweka treni ya mwendokasi Dar mpaka Mwanza?

Mapato ya reli yatawahi kuleta maji kwa wananchi. Yaani return ya treni Ni haraka kuliko maji. Ni sawa ununue gari la biashara ama ujenge nyumba. Gari inaweza ikajenga nyumba ndani ya one to two years Ila nyumba mapato take hayawezi nunua gari kwa muda huo
Unayosema ni sawa kama reli itaendeshwa kwa ufanisi na mapato kusimamiwa vizuri. Kinyume cha hapo, ni kama pesa itakuwa imetupwa tu..!
 
Habari!

Siijui bajeti ya SGR kiundani ila najua tu kuwa ni zaidi ya trilioni 7 zitatumika kama itaanzia Dar mpaka Mwanza ikipitia Morogoro na Dodoma.

Shilingi trilioni 7 ukiziweka kwenye miundombinu ya maji zinaweza kufanya kila kaya nchi yote kupata maji safi na salama na chenji inarudi.

Je, tulipaswa kuanza na treni ambayo inapita mikoa michache tu au kusambaza maji safi kila kaya nchi mzima?.
Hayo ma Sgr ni upuuzi mtupu.Til.7 ni sawa na km 70,000 za lami Nchi nzima
 
Miaka yote ambapo hapakuwa na treni ya mwendokasi mbona hapakuwa na maji? Ukishasambaza hayo maji then what? Ila ukirahisisha usafirishaji na kuokoa pesa kwa kupunguza gharama, hiyo pesa unaweza kutumia kusambaza maji
 
Topic zongine huwa ni Rubbish [emoji1005]

Huwezi pinga miundombinu ambayo inakuja kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa taifa zima,huku ikiomgeza soko kwa Bandari yetu kuu ya Dar es Salaam.

Kama nchi lazima tuwe na vipaumnele ambavyo ni positive in long future economic!

Hiyo hela itakayozalishwa huko ndio itakuja kuanzisha na kusambaza miradi ya maji kwa wakati mwingine kama kipaumbele cha wakati huo.

Naona kama unamtafita Magufuli kiaina!
Maana nyingi bila Magufuli hakuna mnaloweza waza nje ya Box!
Inasikitisha sana kuona kuna vijana hata akili hawana!
 
Kwa hapa tulipofikia, tununue smelter tuanze kuzalisha chuma. Chuma kila siku tunatumia na tunauhitaji nacho sana.

Tunatumia madola mengi sana kuagiza bidhaa za Chuma kutoka nje. Sasa ifike wakati tuzalishe chuma kwa ajili ya matumizi yetu wenyewe na soko la nje pia
Hawatakubali hawa watu, walishanunuliwa kitambo ndiyo maana chuma inatoka kila kukicha kwenda kwa mabwana wakubwa wao
 
Habari!

Siijui bajeti ya SGR kiundani ila najua tu kuwa ni zaidi ya trilioni 7 zitatumika kama itaanzia Dar mpaka Mwanza ikipitia Morogoro na Dodoma.

Shilingi trilioni 7 ukiziweka kwenye miundombinu ya maji zinaweza kufanya kila kaya nchi yote kupata maji safi na salama na chenji inarudi.

Je, tulipaswa kuanza na treni ambayo inapita mikoa michache tu au kusambaza maji safi kila kaya nchi mzima?.
Unajua uchumi wa nchi unajengwa kwa namna ya ajabu ambayo ukifirikia kwa haraka haraka unaweza dhani viongozi wanazingua. Huo mradi ni catalyst (kichochezi) ni mradi utakachochea maendeleo mengine katika sekta zengine.

Kukiwa na usafiri wa uhakika kutoka dar mpaka mwanza kupitia morogoro sekta ya utalii itakuwa, mbuga zilizopo morogoro, vivutio vyote vilivyopo mkoa hii reli imepita vitakuwa na moja ya sababu ni uwepo wa huu mradi.

Mradi wa SGR utapelekea sekta ya uwekezaji nchini ikue. Pia mradi utatoa ajira kwa watanzania. Watu hawaelewi? Au hawawazi? Kazi yao kuponda tu. Mimi sio CCM lakini jamani kabla ya kuongea em shirisha ubongo wako kwanza.

Narudi
 
Back
Top Bottom