Ipi ni njia nzuri ya kutunza carrots na hoho nyumbani ili zisiharibike

Nina health issue inayonihitaji kula carrot, hoho, vitunguu na spinach on daily basis kama dawa, aidha vibichi, kwenye juisi au vipikiwe ila visiive sana. Lakini napata challenge kutunza hoho na carrot. Spinach hazina shida sababu niliweka kabisa bustani ila hoho na karrot ulimaji wake kinyumbani ni mgumu ndio maana nanunua in bulk kisha kutunza kwenye friji.

Changamoto ninayopata ni zinaharibika sana, yaan hamna tofauti kuziweka kwenye friji au kuziacha nje sababu kote kote tu zinaharibika kwa kutepeta tepeta hivi. Kununua chache ni usumbufu sana ukizingatia ratiba ya kuzitumia.

Wataalam wa jf naombeni somo hapa, nifanyeje niweze kuzitunza zisiharibike, kiasi ninachonunua ni aidha sado 1 hadi 2 kwa carrot na hoho ni karibia sado moja
Njia nzuri uzipike zote usiziwazie tena.
 
Bila shaka hizi ziplock plastic bags zitakuwa na msaada kwako. Ukihifadhi humo na ukafunga vizuri zikiwa kavu kabisa na kuziweka kwenye friji zitakaa muda mrefu. Hata kuhifadhia nyama, samaki n.k. kwenye freezer zinafaa sana. Ukienda supermarket hauwezi kuzikosa.
 
Attachments

  • 20241210_163841.jpg
    20241210_163841.jpg
    517.6 KB · Views: 10
Bila shaka hizi ziplock plastic bags zitakuwa na msaada kwako. Ukihifadhi humo na ukafunga vizuri zikiwa kavu kabisa na kuziweka kwenye friji zitakaa muda mrefu. Hata kuhifadhia nyama, samaki n.k. kwenye freezer zinafaa sana. Ukienda supermarket hauwezi kuzikosa.
Shukran mkuu
 
Kwenye fridge unaweka kwenye ile drawer haziharibiki wala kulegea hata mwezi. Kama hazitoshi hapo nunua airtight container zifunge na zile kitchen paper towel ziko kama tissue ila kubwa kisha unaweka ndani ya hizo airtight container. Unagonga mwezi bila kuharibika. Containers zipo maduka ya vyombo hakikisha tu ni airtight sio mfuniko unafunguka funguka kirahisi
Bila kuzifunga na hizo paper towels ukiziweka tu kwenye airtight containers na kuhifadhi kwenye friji zitaharibika?
 
Kazi ya hizo paper towels ni ku absorb water zinazuwia moisture,kutokana na ubaridi wa friji,inawezekana kutengeneza moisture ndani ya container japo ni kwa kiasi kidogo,

So,kutumia hizo towel paper ni safe zaidi.
 
A simple way and cheap chukua gazet au bahasha za kaki,fungia karoti zako then weka kwenye mfuko wa magufuli,weka kwenye friji,hata mwezi zinakaa mpaka utakuta zinataka kuota haziozi ,ila hoho ni changamoto kidogo nazo fanya hivyo hivyo
 
Nina health issue inayonihitaji kula carrot, hoho, vitunguu na spinach on daily basis kama dawa, aidha vibichi, kwenye juisi au vipikiwe ila visiive sana. Lakini napata challenge kutunza hoho na carrot. Spinach hazina shida sababu niliweka kabisa bustani ila hoho na karrot ulimaji wake kinyumbani ni mgumu ndio maana nanunua in bulk kisha kutunza kwenye friji.

Changamoto ninayopata ni zinaharibika sana, yaan hamna tofauti kuziweka kwenye friji au kuziacha nje sababu kote kote tu zinaharibika kwa kutepeta tepeta hivi. Kununua chache ni usumbufu sana ukizingatia ratiba ya kuzitumia.

Wataalam wa jf naombeni somo hapa, nifanyeje niweze kuzitunza zisiharibike, kiasi ninachonunua ni aidha sado 1 hadi 2 kwa carrot na hoho ni karibia sado moja.
Usininunuwe carrot zile za kuzowazowa zinapangwa chini hazina ubora.

Nunuwa carrot og ziweke kwenye ile mifuko laini ya nylon funga weka kwenye friji, ukihitaji unafunguwa unatowa unafunga tena unaweka kwenye friji carrot haziharibiki hata siku moja.
 
nmefanya kama hivi lakini zinapata barafu na kuganda. Ukitoa ukaweka kwenye maji zikilainika tu zinatepeta moja kwa moja
 
Ziweke kwenye mfuko wa plastic zikiwa kavu bila unyevu wowote. Funga vizuri mzuko weka kwenye fridge hata mwezi zinakaa.
Na Mimi huwa nafanya hivyo.Carrot hata kama huna fridge ikiwa kavu funga kwenye MFUKO WA nylon inakata hata week.
 
nmefanya kama hivi lakini zinapata barafu na kuganda. Ukitoa ukaweka kwenye maji zikilainika tu zinatepeta moja kwa moja
Utakuwa uliweka kwenye freezer. Ukiweka huko lazima zigande. Weka kwenye eneo la fridge lenye ubaridi wa kawaida.
 
Nina health issue inayonihitaji kula carrot, hoho, vitunguu na spinach on daily basis kama dawa, aidha vibichi, kwenye juisi au vipikiwe ila visiive sana. Lakini napata challenge kutunza hoho na carrot. Spinach hazina shida sababu niliweka kabisa bustani ila hoho na karrot ulimaji wake kinyumbani ni mgumu ndio maana nanunua in bulk kisha kutunza kwenye friji.

Changamoto ninayopata ni zinaharibika sana, yaan hamna tofauti kuziweka kwenye friji au kuziacha nje sababu kote kote tu zinaharibika kwa kutepeta tepeta hivi. Kununua chache ni usumbufu sana ukizingatia ratiba ya kuzitumia.

Wataalam wa jf naombeni somo hapa, nifanyeje niweze kuzitunza zisiharibike, kiasi ninachonunua ni aidha sado 1 hadi 2 kwa carrot na hoho ni karibia sado moja.
Mimi Huwa nakaa na Karoti na hoho kwenye fridge zaidi ya wiki tatu, Huwa nachukua mifuko ya lailoni ambayo haiingizi hewa weka humo.

Ukitaka ya kupikia chukua Moja then funga Mfuko vizuri.

Tikitimaji linaweza likaka hata kwenye fridge wiki nzima na lisirojeke ukitumia njia hiyo.
 
Back
Top Bottom