Nina health issue inayonihitaji kula carrot, hoho, vitunguu na spinach on daily basis kama dawa, aidha vibichi, kwenye juisi au vipikiwe ila visiive sana. Lakini napata challenge kutunza hoho na carrot. Spinach hazina shida sababu niliweka kabisa bustani ila hoho na karrot ulimaji wake kinyumbani ni mgumu ndio maana nanunua in bulk kisha kutunza kwenye friji.
Changamoto ninayopata ni zinaharibika sana, yaan hamna tofauti kuziweka kwenye friji au kuziacha nje sababu kote kote tu zinaharibika kwa kutepeta tepeta hivi. Kununua chache ni usumbufu sana ukizingatia ratiba ya kuzitumia.
Wataalam wa jf naombeni somo hapa, nifanyeje niweze kuzitunza zisiharibike, kiasi ninachonunua ni aidha sado 1 hadi 2 kwa carrot na hoho ni karibia sado moja.