Ipi ni simu yako ya kwanza kumiliki?

Ipi ni simu yako ya kwanza kumiliki?

Nokia Jeneza mwaka 2008 ndio kwa mara ya kwanza nikaitumia kama kama mwaka nikaja nikanunua Nokia Express Music hii simu niliipenda sana baada ya hapo nikaja kununua Huawei zile za promotion ya Tigo Mlimani City yan zinasoma Tigo peke ake. The rest is history
 
Hii ndio ilikua simu yangu ya kwanza kipindi hicho nilikua naipenda sana hasa jins Keyboard yake ilivyokaa. Enzi hizo Nilikua nakesha Waptrick kupakua nyimbo za akina Wizkid,Burnaboy,K.O, Casper nyovest, Baky W, n.k wakati huo hao wasanii hawajulikani nadhani mtaani kwetu tu ndio tulikua tunawajua ajili ya kuwepo kwa channels ya HipTv, Soundcity na Chenel O.
View attachment 2239430
Hii ndio Smartphone yangu ya kwanza 2014 mzee wangu aliniletea toka Qatar nilikua naeatambia washkaji maana walikua wananivimbia na Tecno P5,Y6 zao. Kiukweli Sijawahi penda simu kama nilivyopemda hii. Kuanzia wallpapers zake na UI. Hapo kwenye Lige Companion nilikua nafuta naweka jina langu. Iliibiwa tarehe 5/6/2017 Zenji pamoja na Toshiba PC niliyopewa pamoja na hii simu (Sitasahau siku hiyo maana nilikesha ajili ya maumivu)
View attachment 2239443
2014 ulikuwa bado unapewa vitu na mshua wako?
 
Vodafone, mwaka 2008
20220624_001157.jpg
 
Huu Uzi umenikumbusha marehemu Baba yeye ndie alikuwa mtu wa kwanza kuninunulia simu enzi hizo alinunulia Sony Erickson ya kufunika na kufunua.
 
Chuma hiko hapo early 2002!

IMG_20220624_222941.jpg

Ilikuwaga kubwa mkononi hainienei hii nilipewa na mimi nioshee sura nikanunua line yangu ya Airtel kipindi hiko ikiitwa Celtel piga usipigiwe unakatwa salio nakumbuka kuna siku ilizima nikaweka battery za National zile ndogo mbili ikawaka.kinachonifurahisha mpaka sasa namba ninayotumia ni hii niliyonunua kwa ajili ya simu hiyo.
 
Chuma hiko hapo early 2002!

View attachment 2270973

Nina rafiki yangu anayo hiyo Simu na huwa anaifunga kwenye suluari,yaani anafanya kama comedy,ikiita kama call box
 
Chuma hiko hapo early 2002!

View attachment 2270973
Ilikuwaga kubwa mkononi hainienei hii nilipewa na mimi nioshee sura nikanunua line yangu ya Airtel kipindi hiko ikiitwa Celtel piga usipigiwe unakatwa salio nakumbuka kuna siku ilizima nikaweka battery za National zile ndogo mbili ikawaka.kinachonifurahisha mpaka sasa namba ninayotumia ni hii niliyonunua kwa ajili ya simu hiyo.
Betri za national? 😂🙌
 
Back
Top Bottom