Ipi ni simu yako ya kwanza kumiliki?

Nokia Jeneza mwaka 2008 ndio kwa mara ya kwanza nikaitumia kama kama mwaka nikaja nikanunua Nokia Express Music hii simu niliipenda sana baada ya hapo nikaja kununua Huawei zile za promotion ya Tigo Mlimani City yan zinasoma Tigo peke ake. The rest is history
 
2014 ulikuwa bado unapewa vitu na mshua wako?
 
Huu Uzi umenikumbusha marehemu Baba yeye ndie alikuwa mtu wa kwanza kuninunulia simu enzi hizo alinunulia Sony Erickson ya kufunika na kufunua.
 
Chuma hiko hapo early 2002!


Ilikuwaga kubwa mkononi hainienei hii nilipewa na mimi nioshee sura nikanunua line yangu ya Airtel kipindi hiko ikiitwa Celtel piga usipigiwe unakatwa salio nakumbuka kuna siku ilizima nikaweka battery za National zile ndogo mbili ikawaka.kinachonifurahisha mpaka sasa namba ninayotumia ni hii niliyonunua kwa ajili ya simu hiyo.
 
Nina rafiki yangu anayo hiyo Simu na huwa anaifunga kwenye suluari,yaani anafanya kama comedy,ikiita kama call box
 
Betri za national? 😂🙌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…