Ipi sababu ya Kenya kupendwa kuliko Tanzania licha ya kuwapita utajiri wa utamaduni?

Lugha gani tena? Hapo umeambiwa nchi 54, au unataka kusema Kenya wanazungumza zaidi kiingereza kuliko Uganda, Zambia, Zimbabwe, ghana, nigeria?
Tutafute sababu halisi
Kuna sehemu nimeongelea masuala ya lugha aisee au umenichanganya na mtu mwingine 😳😳
 
Tanzania kuna potential kubwa sana kiutalii sema focus yetu imekua tu sehemu ndogo .......wakenya na vivutio vichache ila wameweza kuvitumia, bongo ukiacha kaskazini huku kwingine kumesahaulika sana
 
Hiyo ndiyo point kubwa sana ya ujamaa wa mwalimu ndiyo ulituangusha kwa asilimia takribani 80.
Ilikuwa ngumu sana kuingia Tanzania kuomba visa kama unaomba ajira wakati wenzetu visa ilikuwa anagongwa Air port kwa watalii.
Madini kuchimbwa ilikuwa marufuku huku Hotel kubwa zote pale Nairobi zikiwa zimezungukwa maduka ya madini na madini yote yalikuwa yatoka Tanzania.
Elimu ilikuwa ni ya msingi darasa la saba utakwendanayo wapi utaifanyia nini.
Makampuni yote yakawa mali ya uma mkurugenzi anaweza akafungiwa nje na wafanyakazi.
Hii ndiyo Tanzania.
 
Tanzania kuna potential kubwa sana kiutalii sema focus yetu imekua tu sehemu ndogo .......wakenya na vivutio vichache ila wameweza kuvitumia, bongo ukiacha kaskazini huku kwingine kumesahaulika sana
Ni kweli, unajua kwa mfano ziwa Tanganyika ndio ziwa lenye kina kirefu barani afrika na kuna utalii wa kutosha ziwani ikiwemo scuba diving, ziwa nyasa Kuna Mbuga Kama Mikumi, Katavi nk ambazo Zina wanyama na vivutio vingi zaidi.

Tuna mapori ya ziada makubwa sana ukanda wa magharibi ya Tanzania Ila ndio tupo busy na Serengeti tu.
 

Ila swala la lugha ni utumwa tu, mataifa mengi yanaongea lugha zao mbona wameendelea. Hata Ethiopia hapo hawatumii kiingereza wala kifaransa, lugha yao inaongewa na wao wenyewe tu tena hata kitaifa ni jimbo moja la Addis Ababa. Mbona wazungu wanaitetemekea. Na waethiopia wengi hawajui Kiingereza. Ni lugha zao za kienyeji.
Nchi zote za Ulaya wanatumia lugha zao. Urusi, China, Indonesia, Malyasia, nenda arabuni, wanatumia lugha yao, na nchi nyingi nyinginezo. Ebu nitajie hiyo Kenya imeendelea nini zaid? Nitajie nchi iliyoendelea duniani kwa kutumia lugha isiyo yao!
Tuache mawazo ya kitumwa.
 
Aisee, hivi Kenya huwa tuna deni lenu, ambalo tumekataa kuwalipa au ndio huwa kunaendaje? Maanake inashangaza sana kwamba kati ya nchi zote hizo 54, nyie mmeiona tu Kenya. Mbona sisi mambo yetu tunayafanya bila kuitizama wala kujilinganisha na nchi yeyote ile nyingine? Mtapungukiwa nini mkifata utaratibu kama huo?
 
Kama ukikutana na Guide wa utalii anavyoiponda nchi yake na wazungu wanavyofurahi lengo ni kuitengeneza mazingira ya tip (mboneka) wapanda mlima wanaiita hutakumbuka tena Royal Tour
 
KENYA ILIJITANGAZA KWA MDA MREFU SANA DUNIANI TOFAUTI NA TANZANIA,TUNASHUKURU MAMA #SSH AMELIONA HILI NA ANAKWENDA NALO SAMBAMBA MUNGU AMBARIKI SANA MAMA HUYU,JAPO NI GHALI KUFANYA HILI LAKINI HAKUNA NAMNA,HATA KAGAME YUPO BIZE KWENYE HILI,RWANDA NAYO INAWEZA KUWA NEXT TO KENYA,LAKINI KWA BIDII HIZI ZA MAMA "AT NO LONGER WE SHALL BE NUMBER ONE"
 
Kingine kenya ni salama kwa wawekezaji hata mifumo ya utoaji haki ipo wazi na inatabirika huwezi kuta mahakama moja tena ya juu kabisa inatoa hukumu mbili kwa suala moja linalohusisha wadaawa walewale
 
Hivi mzungu anajifunza nini shuleni? Hata aulize swali la kijuha kama "is Tanzania the South afrika, Nigeria or Kenya? mbona sisi tunajua nchi zao na miji yao mikuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…