Ipi sababu ya Kenya kupendwa kuliko Tanzania licha ya kuwapita utajiri wa utamaduni?

Ipi sababu ya Kenya kupendwa kuliko Tanzania licha ya kuwapita utajiri wa utamaduni?

Lugha gani tena? Hapo umeambiwa nchi 54, au unataka kusema Kenya wanazungumza zaidi kiingereza kuliko Uganda, Zambia, Zimbabwe, ghana, nigeria?
Tutafute sababu halisi
Kuna sehemu nimeongelea masuala ya lugha aisee au umenichanganya na mtu mwingine 😳😳
 
Ndugu yangu siku hizi kuna kitu kinaitwa 'cultural tourism' have you ever heard about it? Hii ni muhimu sana na inaleta pesa nyingi sana kwa wamasai.

Pia Kuna sex tourism wenzetu hapo Lamu na Malindi imeshamiri sana beach boys wanakula wamama wa kizungu kwa malipo naona Zanzibar imeanza hii.

Kuna agricultural tourism etc yani Ile sabasaba day inatakiwa wageni wajae Tanzania kuja kuangalia what do we in the market!

Kuna vitu tumezubaa ndio maana wenzetu wanatupiga bao sehemu ndogo sana.

Sisi tuna vivutio vingi zaidi Ila hatujajiongeza kuvifanya viafahamike kwamba tunavyo ili tuexplore hizo fursa.

Wakisema wanazo fursa tunaanza kukasirika all we have to offer is Kilimanjaro and Serengeti huu no ujinga wakenya hata Kilimanjaro wameacha kuitaja siku hizi.

We have to be proactive.
Tanzania kuna potential kubwa sana kiutalii sema focus yetu imekua tu sehemu ndogo .......wakenya na vivutio vichache ila wameweza kuvitumia, bongo ukiacha kaskazini huku kwingine kumesahaulika sana
 
Hiyo ndiyo point kubwa sana ya ujamaa wa mwalimu ndiyo ulituangusha kwa asilimia takribani 80.
Ilikuwa ngumu sana kuingia Tanzania kuomba visa kama unaomba ajira wakati wenzetu visa ilikuwa anagongwa Air port kwa watalii.
Madini kuchimbwa ilikuwa marufuku huku Hotel kubwa zote pale Nairobi zikiwa zimezungukwa maduka ya madini na madini yote yalikuwa yatoka Tanzania.
Elimu ilikuwa ni ya msingi darasa la saba utakwendanayo wapi utaifanyia nini.
Makampuni yote yakawa mali ya uma mkurugenzi anaweza akafungiwa nje na wafanyakazi.
Hii ndiyo Tanzania.
BET Awards Red Carpet...
Pamoja na mambo mengine, usikute Diamond hapo alidhani alikuwa anaitangaza Tanzania lakini kwa wale ambao ilikuwa ndo mara yao ya kwanza kumuona/kumsikia basi, kwa hiyo dressing code, majority aliwaaminisha yeye ni Mkenya!!

Nini hiyo dressing code, hata Kiswahili huko mbele majority wanadhani Kenya ndo "wenyewe"!!

Ingawaje kwa mbaaaaaaali hivi sasa kidogo inapungua lakini zamani kuitambulisha Tanzania ipo wapi ilikuwa ni kazi ngumu kweli kweli hususani kama HUTAKI kuitaja Kenya kwa sababu the only way kuitambulisha kirahisi ilikuwa uitaje Kenya manake hata ukitaja Mt Kilimanjaro, usishangae ukaambiwa "Oh! So, you mean it's Kenya"!

Bila shaka hapo utakuwa umepata jibu!!

In short, Ujamaa wa Mwalimu ulitufanya Watanzania kuwa mazombi and less aggressive! Na vile hatutaki hata kuwashtua CCM physically, ndo kabisa coz' in Africa, if you don't have something good to showcase, just showcase your unpleasant side!
 
Tanzania kuna potential kubwa sana kiutalii sema focus yetu imekua tu sehemu ndogo .......wakenya na vivutio vichache ila wameweza kuvitumia, bongo ukiacha kaskazini huku kwingine kumesahaulika sana
Ni kweli, unajua kwa mfano ziwa Tanganyika ndio ziwa lenye kina kirefu barani afrika na kuna utalii wa kutosha ziwani ikiwemo scuba diving, ziwa nyasa Kuna Mbuga Kama Mikumi, Katavi nk ambazo Zina wanyama na vivutio vingi zaidi.

Tuna mapori ya ziada makubwa sana ukanda wa magharibi ya Tanzania Ila ndio tupo busy na Serengeti tu.
 
Lugha inawabeba wenzetu sana ni Wakati sasa wa kuanza kufundisha Lugha ya Dunia kuanzia Primary mpaka Chuo kikuu, Hili Swala la kukumbatia kiswahili tu. Kwa kweli linatukosesha Kuwa linked na Ulimwengu tembea hata Platform nyingi uone wakenya wanavyo ji brand ila sisi watz tunakwama kwa ajili ya Lugha pia

Ila swala la lugha ni utumwa tu, mataifa mengi yanaongea lugha zao mbona wameendelea. Hata Ethiopia hapo hawatumii kiingereza wala kifaransa, lugha yao inaongewa na wao wenyewe tu tena hata kitaifa ni jimbo moja la Addis Ababa. Mbona wazungu wanaitetemekea. Na waethiopia wengi hawajui Kiingereza. Ni lugha zao za kienyeji.
Nchi zote za Ulaya wanatumia lugha zao. Urusi, China, Indonesia, Malyasia, nenda arabuni, wanatumia lugha yao, na nchi nyingi nyinginezo. Ebu nitajie hiyo Kenya imeendelea nini zaid? Nitajie nchi iliyoendelea duniani kwa kutumia lugha isiyo yao!
Tuache mawazo ya kitumwa.
 
Aisee, hivi Kenya huwa tuna deni lenu, ambalo tumekataa kuwalipa au ndio huwa kunaendaje? Maanake inashangaza sana kwamba kati ya nchi zote hizo 54, nyie mmeiona tu Kenya. Mbona sisi mambo yetu tunayafanya bila kuitizama wala kujilinganisha na nchi yeyote ile nyingine? Mtapungukiwa nini mkifata utaratibu kama huo?
 
Kama ukikutana na Guide wa utalii anavyoiponda nchi yake na wazungu wanavyofurahi lengo ni kuitengeneza mazingira ya tip (mboneka) wapanda mlima wanaiita hutakumbuka tena Royal Tour
 
Nilikuwa naangalia video flani YouTube inahusu capital city za nchi 54 za Africa. Sasa nikaenda sehemu ya comments kusoma nikajionea watu wengi kutoka mataifa mbalimbali dunia wakiisifia Kenya kuwa ndo favourite country yao lakini kiuhalisia ni dhahiri tumewazidi vivutio (Sina haja ya kuvitaja vinajulikana) pamoja na utamaduni tuna makabila mengi ambayo wazungu labda wangetamani kuja kwetu kujifunza Mila za makabila pia tuna amani hatuna historia mbaya ya kumwagana damu kugombana kubwa zaidi tuna eneo kubwa la ardhi mapori yasiyofanyiwa chochote yameachwa tu hivyo ni rahisi kuwekeza tofauti na Kenya ambapo ardhi inashikiliwa na wachache.

Sielewi kwanini wazungu waipende kenya tukisema kwamba sababu ni ina maendeleo sio kweli maana hata kwao ulaya huko wako vizuri tu hawawezi kuja kushangaa magorofa ya Nairobi hapo na hata hivyo kama kutupita kiuchumi hawajatupita sana ni gap fulani la kawaida.

Ingawa pia nilianza kuhisi labda comments hizo zaweza kuwa ni za Wakenya wenyewe wameamua tu kujimwambafy; si mnajua walivyo makanjanja kwenye kujipaisha.

Video yenyewe iko hapo chini search YouTube nenda upande wa comments.

View attachment 2104557
KENYA ILIJITANGAZA KWA MDA MREFU SANA DUNIANI TOFAUTI NA TANZANIA,TUNASHUKURU MAMA #SSH AMELIONA HILI NA ANAKWENDA NALO SAMBAMBA MUNGU AMBARIKI SANA MAMA HUYU,JAPO NI GHALI KUFANYA HILI LAKINI HAKUNA NAMNA,HATA KAGAME YUPO BIZE KWENYE HILI,RWANDA NAYO INAWEZA KUWA NEXT TO KENYA,LAKINI KWA BIDII HIZI ZA MAMA "AT NO LONGER WE SHALL BE NUMBER ONE"
 
Kingine kenya ni salama kwa wawekezaji hata mifumo ya utoaji haki ipo wazi na inatabirika huwezi kuta mahakama moja tena ya juu kabisa inatoa hukumu mbili kwa suala moja linalohusisha wadaawa walewale
 
Hivi mzungu anajifunza nini shuleni? Hata aulize swali la kijuha kama "is Tanzania the South afrika, Nigeria or Kenya? mbona sisi tunajua nchi zao na miji yao mikuu.
 
Back
Top Bottom