Ipi sehemu nzuri kujenga na kuishi?

Ipi sehemu nzuri kujenga na kuishi?

Acha kupovuka, zipo sehemu zimepimwa na bado viwanja vipo na vina uzwa acha kukariri
Aliyekariri mimi au wewe?

Tuwekee hapa hizo sehemu zilizopimwa watu wakaishi lah hukuweza wewe ndiye umetoa povu!
 
Habari zenu wana JamiiForums!

Ningependa kupata maoni kwa wadau katika kuchagua eneo la kuishi. Kuna ndugu yangu anataka kujenga kabisa, viwanja anasema vipo poa kapata maeneo haya;

1. kigamboni (mjimwema, gezaulole, kisiwa)
2. kimara
3. Mbezi mwisho
4. Kitunda
5. Goba

Hivyo viwanja maeneo hayo yote anasema dalali kamwambia ni swala la yeye kuchagua eneo, kote vipo anapelekwa mda wowote.

Je, ni sehemu gani nzuri ya kuishi?
Hizo sehemu nzuri ila akipata Oysterbay, Regency estate, Sea View au Masaki hakika ata enjoy sana life ya muda mfupi kwenye hii Jamhuri ya Kazi iendelee
 
Tubadili fikra na tuone mbele. Swali ni zuri lakini hivyo viwanja ni ukubwa gani? Kama unaona mbali ni muda sasa wa kuachana na kununua viwanja badala yake nenda pembezoni, nunua ekari 2 na kuendelea. Hapa ndo unaweza kufanya uendelezaji kwa ajili ya kuishi hadi uzeeni. Unaambiwa miaka ya 60 Tabata, Tegeta, Kawe, Mbezi yalikuwa ni mapori na wanaosimulia bado wako hai, mtu anakwambia hapa mbezi shule niliitiwa shamba nikakataa ili niishi Mikocheni kwenye watu.
Anataka kujenga ndani kama ya miaka ijayo atakuwa amemaliza yuko mwanza amehamishwa huku kikazi.
 
Habari zenu wana JamiiForums!

Ningependa kupata maoni kwa wadau katika kuchagua eneo la kuishi. Kuna ndugu yangu anataka kujenga kabisa, viwanja anasema vipo poa kapata maeneo haya;

1. kigamboni (mjimwema, gezaulole, kisiwa)
2. kimara
3. Mbezi mwisho
4. Kitunda
5. Goba

Hivyo viwanja maeneo hayo yote anasema dalali kamwambia ni swala la yeye kuchagua eneo, kote vipo anapelekwa mda wowote.

Je, ni sehemu gani nzuri ya kuishi?

Along side morogoro road is the future

So kimara,mbezi,kibamba ni bora hasa kama una plan za muda mrefu.ni sehemu ambazo zinakua in 5 years to come zitaungana na kibaha.
 
Along side morogoro road is the future

So kimara,mbezi,kibamba ni bora hasa kama una plan za muda mrefu.ni sehemu ambazo zinakua in 5 years to come zitaungana na kibaha.
Ila yeye mishe zake anasema zitakuwa maeneo ya posta.
 
Miaka yote nloishi dar kgambon cjawah fika ila naonaga kama imekaa kushoto sana. Kmara na mbez jenga kwa akili mana bomoa bomoa haijawah kuisha
 
Una guarantee ya kuishi mpaka uzeeni?
Hapana, lakini Maandiko Matakatifu (BIBLIA) husema;

"Mwenye haki ataishi kwa imani" hivyo tunaamini kwa neema za Mungu tutatusua hadi uzeeni.

NAKAZIA:

YEREMIA 29:11.

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
 
It ain't......

Unatoa shit kwa watu kutaka kujiendeleza kimaisha huku upo kwenye store hapo Tabata kusipopimwa tena banda la uwani,wewe Dar ni wapi kwa %100 pana viwanja vilivyopimwa kama siyo huko nje ya mji alikosema mleta mada?
Mkuu inategemea unasema Tabata ipi, Sehemu zilizo nyingi za Tabata kumepimwa.
 
Ukubwa wa eneo ndio 'factor' ya kwanza, kama utataka kuweka makazi ya kudumu mpaka kifo; angalau liwe ekari 5
 
Back
Top Bottom