Ipo haja sheria za unywaji pombe bar zirekebishwe

Ipo haja sheria za unywaji pombe bar zirekebishwe

Wanakusaidia usiamkie pombe wewe unaona wanakupuja.
 
Sasa unywe pombe mchana halafu uingie kazini usiku kweli! Kama huwezi kujizuia basi tambua kwamba wewe ni dhaifu!
Pombe mchana huonjwa onjwa tu kama kisindikiza ugali....! Pombe hasa muda wake ni usiku mpaka saa 7 - 8,unapovukisha hapo unakuwa ni mlevi fulani.
 
Kuna bars ubungo, sinza, kinondoni hiyo sheria hatuitambui kabisa.
-Rushwa-
Adui wa haki na mpindisha sheria,ipo kada hapo inakuwa inakula kiubwete rushwa, wengi tunaomba iwe official, naona biashara hii kwa awamu ya sita imeanza kuamka kwa kasi ya ajabu.
 
Kwa pamoja wanywaji wote tunasema hivi we ni mtetezi wetu.....ongeza lager 3 mwambie waiter bill alete huku
 
Naunga mkono hoja sisi wengine wakulima
Serekali na viwanda vyetu waliwajali sana wakulima ikitambua wakulima kwa tanzania wanamizania ya 85%, 3%wafanyakazi, na 12% ndio Sisi wafanyabiashara kwa Ujumla wetu, lakini kwa upendo viwanda vyetu pendwa vikawapa tunu wakulima kwa "The kick, na Balimi" kama tuzo maalumu kwenu.
 
Mbona tunakunywa masaa yote.
nadhani ni baadhi ya bar.
 
Leseni zinasema bar ifunguliwe saa 10 jioni mpaka saa 5 usiku kwa siku za j3-ijumaa,na Jumamosi na jumapili saa 8 mchana mpaka saa 6 usiku.
Nashauri leseni ziruhusu kunywa pombe masaa yote Isipokuwa kwa staha maalumu, namaanisha kwa masaa kabla ya saa kumi pombe zinywewe ndani ya bar au mahala ambapo mnywaji hataonekana na kadamnasi au hatukuwa katika hadhara za kadamnasi, itakapotimu saa kumi ndio iwe ruhusa watu kujivinjari na vinywaji vyao huku wakionekana na kadamnasi au hadhara.
Reasons:-
Kila mtanzania anamasaa yake ya kwenda kuwajibika katika kujitafutia riziki, Tupo ambao ni walinzi ambao muda wetu wa kujivinjari ni mchana tu, wapo wenye shifts zao viwandani ambao huingia kazini usiku, wakulima wao hujipangia muda wao wenyewe alkadhalika wafanyabiashara ni kada zinazojipangia muda kutegemeana na jukumu lililopo.
Tbl awali kilikuwa ndicho kiwanda tegemewa kimapato kwa serekali.
"TBL & SERENGETI BREWERIES, NOURISH YOUR LIVES"
Boss Mchana huo Walinzi tunakuwa tumelala tunajiandaa na lindo Usiku na na Wanaofanya kazi Mchana wanakuwa bize Sana hivyo wakirekebisha Sheria wafanyakazi wa Mchana watakuwa Walevi sana
 
Watu wanatumia pesa zao tena wanapangiwa muda wa kuzitumia. Me nadhani sheria ziwekwe kwa wale wazembe ambao wakinywa wanarukwa akili na kufanya mambo ya ajabu.
 
Back
Top Bottom