Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
KUNA HISTORIA KUBWA YA MWALIMU NYERERE NDANI YA SOKO LA KARIAKOO
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amelifungua Soko la Kariakoo jana Jumapili tarehe 8 February 2026.
Nimepata siku za nyuma kuandika makala kuhusu Soko la Kariakoo nikasema kuwa lazima liwekwe bango litakaloonyesha kuwa hapo sokoni kulikuwa na sehemu ilipojengwa ofisi ya Market Master ambayo sasa ofisi hiyo hapo lakini hapo ndipo ilipokuwa ofisi ya Brian Hodges, Market Master Muingereza.
Baada ya Brian Hodges kuacha kazi ile nafasi yake ikashikwa na Abdulwahid Sykes.
Hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 1950 na harakati za siasa za chini kwa chini dhidi ya ukoloni wa Muingereza zilikuwa zinaanza kupamba moto.
Mwalimu Nyerere alikuwa kachaguliwa Rais wa TAA April 1953 Makamu wa Rais akiwa Abdul Sykes.
Uchaguzi huu ulifanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 April 1953.
Ikawa Nyerere akitoka Pugu kuja Dar es Salaam mjini alikuwa moja kwa moja anakwenda ofisini kwa Abdul Sykes Soko la Kariakoo.
TANU ilipoundwa mwaka wa 1954 ofisi hii ya Market Master ikawa moja ya ngome kuu za harakati dhidi ya serikali.
Ofisi hii ikawa moja ya vituo vilivyokuwa vinasambaza kadi za TANU kwanza kwa wafanya biashara ndani ya soko lile na mwananchi yeyote aliyetaka kujiunga na chama.
Chini ya Abdul Sykes kulikuwa na watu wawili waajiriwa wa soko - Shariff Abdallah Omari Attas na Mshume Kiyate.
Shariff Attas alikuwa mkusanyaji wa ushuru wa nafaka na Mshume Kiyate alikuwa dalali wa samaki.
Hawa walikuwa watu maarufu sana Dar es Salaam na ndiyo walikuwa watu wa mwanzo kujuana na Mwalimu Nyerere alipofika Ofisi ya Market Master mwaka wa 1952.
Kupitia watu hawa watatu Mwalimu Nyerere akafahamika na watu wengi pale sokoni.
Haiba ya Ofisi ya Market Master ikaongezeka kutoka kuwa ofisi ya biashara kuwa ngome ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Harakati zilizokuwa za siri zikawa si siri tena Soko la Kariakoo likawa ngome kubwa iliyobeba wanachama wengi wa TANU na sehemu iliyotegemewa katika kuchangia fedha TANU.
Hapana shaka mchango wa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO ulianza hapo.
Soko la Kariakoo halikuishia hapo.
Soko la Kariakoo ndilo likawa linatoa chakula kila siku asubuhi kupeleka nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Magomeni Maduka Sita.
Mnunuzi wa chakula hiki alikuwa Mshume Kiyate na dereva wa TANU Said Kamtawa ndiye aliyekuwa akija sokoni Kariakoo kila siku kuchukua mahitaji ya kila siku ya nyumbani kwa Mwalimu.
Makachero wa Special Branch wakawa hawapungui Soko la Kariakoo na ndipo ilipoamuliwa Ofisi ya Market Master, Abdul Sykes ivamiwe ipekuliwe.
Hili lilifanyika na kadi za TANU zilikutwa ndani ya Ofisi ya Market Master Abdulwahid Sykes.
Hii ndiyo kwa muhtasari historia ya Soko la Kariakoo katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa miaka ya nyuma kulia hilo jengo dogo ndiyo ilikuwa ofisi ya Market Master.
View: https://youtu.be/5g_DMWsh_uE