kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Utafiti mdogo niliofanya kuhusu ukosefu was nguvu za kiume miongoni mwa vijana unaonyesha kuwa vijana wanaofanyakazi ya bodaboda wanakabiliwa na upungufu was nguvu za kiume kwenye umri mdogo.
Na tatizo ni kubwa kwa wale wanaobeba mishikaki (abiria zaidi ya mmoja) na mizigo mikubwa, kwakuwa inawafanya wasogee mbele na kukalia tank LA mafuta ambalo linabana na kuziminya kwa muda mrefu korodani na mishipa damu na fahamu kwenye sehemu zake za siri.
Pili, vijana wanaoendesha bodaboda hupenda kutumia kinywaji cha energy kama nyia ya kuwaondolea uchovu na usingizi. Lakini kinywaji hiki kina kiasi kikubwa cha caffeine ambayo sio rafiki kwa nguvu za kiume pia.
Tatu, Uchovu mwingi unaotokana na kiendesha bodaboda mchana kutwa juani, kwenye upepo na mvua vinawasababishia uchovu mwingi na magonjwa ya kwenye mfumo wa hewa ambayo yanapunguza ufanisi wa mfumo wao wa uzazi.
NNE, madeni ya pikipiki (hesabu) na polisi barabarani yanawasababishia msongo mkubwa wa mawazo ambao unakwenda kuathiri nguvu za kiume wakati wa tendo.
Serikali ichukue hatua kulilinda kundi hili kubwa na wananchi wake mapema kabla kuzalisha mahanithi wengi. Vijana watafutiwe ajira badala ya kudhani kazi ya bodaboda ni ajira kwa vijana.
Iko Siku (sio Leo) ambayo vijana watakuja kugundua kuwa bodaboda zinawaumiza na kudai kupewa Kazi nyingine salama. Hapo ndipo wanasiasa watatafutana.