Absolutely, Yes, because WHAT GOES AROUND, COMES AROUND...
Huyu jamaa [Tundu Lissu] ni muumini wa UTAWALA WA SHERIA na UHURU WA WATU kuendesha maisha yao kwa mujibu wa sheria. Ni njia ndefu na ya hatari anapitia kulifikia kusudi la kuletwa duniani. LAZIMA AWE KIONGOZI WA NCHI HII WHETHER WANATAKA ama HAWATAKI....
Historia yake ya uongozi na kupambania haki iko very clear...
Mfano, katika kipindi chake cha miaka 10 ya ubunge wake, ktk jimbo la Singida Mashariki alileta mwamko na mabadiliko sana ktk masuala ya kisheria na haki za watu kiasi ambacho ukifika kule, hata sasa, hata mtoto wa darasa la NNE kule Singida Mashariki huwezi kumwambia kitu kwenye masuala ya haki zake..
Nadhani kila mtu anapenda potential na talent ya mtu huyu ktk masuala ya sheria, siasa, uchumi, diplomasia na uongozi kwa ujumla kuleta mabadiliko ktk nchi hii yote....
Alihujumiwa sana na serikali ya CCM kwa kuhakikisha jimbo lake halipati fedha za miradi ya maendeleo ya kijamii ili tu wananchi wamuone kama kiongozi asiye na manufaa kwao...
Walifanya hivyo awamu ya kwanza 2005 - 2010, haikusaidia kwani wananchi walimchagua tena kwa awamu nyingine ya 2010 - 2015 na kurudia tena awamu ya tatu 2015 - 2020...
CCM wakaona huyu mtu hawezi kutoka kwa mbinu zozote kupitia sanduku la kura. Wakaamua kumaliza mambo kwa njia ya BUNDUKI na RISASI. Nayo ilishindwa kwa kiwango cha kutisha japo waliambulia kumtia ulemavu...
Nakubaliana na wewe mleta mada kuwa, WHAT GOES AROUND COMES AROUND. Tundu Lissu atakuwa kiongozi mkubwa sana nchi...!!