Ipo siku Tundu Lissu atakuja kuwa Rais wa Tanzania, ni suala la muda tu

Labda raisi wa mashoga lakini sio tz hii.
 
Juzi nilimsikiliza kupitia space ya Maria Sarungi nikakiri kimoyo moyo Tundu Lissu ni kichwa.
Anajua kujieleza, kupanga hoja, kutoa ufafanuzi kwa mifano halisi mpaka huchoki kumsikiliza. He is next level.
Ukishaona mtu moja yeye pekee ndiye anaamini ndiyo mwenye kauli ya mwisho kwa kila kitu na mwenye vipaji vyote tayari ujue hiyo ego yake ni hatari kwa ustawi wa jamii, nachelea kusema huyu mwenzetu ndivyo alivyo...Ni mzuri kwenye kutia pressure na siyo leasership...Bahati mbaya sana anaowategemea wana akili za kutumia watu kama yeye kufikia malengo yao lakini kamwe hawawezi kumwacha akashika rungu...Ni akili yangu tu ndogo inaniambia hata sasa ameshagundua yeye binafsi ametumiwa na hayo matumaini yanapotea kila iitwapo leo kwake ....Asipokuwa makini kete inaweza kugeuka akageuzwa mhalifu na hao hao anaowatumainia...Ushirika wa wachawi/waovu haudumu!
 
Licha ya akili alizonazo, but he also has spiritual power within !!
 
Kazi ya kuondoa CCM ni lazimai ianzie kwenye katiba, na ndiyo maana ukiwatajia neno katiba ni sawa na kumminya mtu sehemu sizo.
 

Hana sifa. Acha utoto.
 

Watu walio vizuri Ni wengi sana kuliko huyu kilaza. Hana break. Hana busara. Atakuwa Rais wa Nini.
 
Watu walio vizuri Ni wengi sana kuliko huyu kilaza. Hana break. Hana busara. Atakuwa Rais wa Nini.
Utakuwa umejaa chuki za vyama.
Mimi sipo kwenye vyama hivyo namwangalia lissu kwa mtazamo tofauti na wewe.
 
Umeandika kama vile Lissu ni immortal. Yaani wewe ndiyo hujui hiyo miaka mingi ijayo kama utakuwa mzima au la ila kwa Lissu yeye ni lazima atakuwa mzima na lazima atakuja kuwa Rais!!!!!!!! Mawazo ya kushangaza sana. Wewe na Salary Slip mna mahaba na Lissu kiasi cha kututia mashaka, hasa kwetu sisi wanaume rijali. Unasema anatumikia kafiri apate mradi wake. Unajua aina ya ukafiri anaoutumikia na kitu wanachomfanya kila siku katika kupata huo mradi wake?. Kwa sisi wanaume wa kweli tunamuonea huruma sana Lissu kwa anayofanyiwa na mabeberu. Usiombe uvae viatu vyake. Moto wake anaujua yeye.
 
Lissu ni Magufuli mwenye exposure. Siku akiwa Rais zitatengenezwa sheria nyingi kama Mwenzake alivyotengeneza mabarabara mengi. Only Time Will Tell.

Sent from my SM-N975F using JamiiForums mobile app
 
Jimbo aliloliongoza tundu lisu miaka 10 hajaliletea maendeleo yeyote hakuna hata maji je nchi anaweza kuileteaje maendeleo?
Wewe bure kabisa hujui hata majukumu ya mbunge na majukumu ya mkurugenzi ni nini.
Nani aliye kudanganya kazi ya mbunge ni kuleta maendeleo jimboni kwake?
 
Hangaya ni mbovu lakini ni mara elfu mia ikulu ibaki tupu kuliko lisu kuongoza taifa letu.
πŸ˜‚
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ , khaa, kwamba ni kweli nanii ni wa hovyo ila nanii ni wa hovyo zaidi.
 
Absolutely, Yes, because WHAT GOES AROUND, COMES AROUND...

Huyu jamaa [Tundu Lissu] ni muumini wa UTAWALA WA SHERIA na UHURU WA WATU kuendesha maisha yao kwa mujibu wa sheria. Ni njia ndefu na ya hatari anapitia kulifikia kusudi la kuletwa duniani. LAZIMA AWE KIONGOZI WA NCHI HII WHETHER WANATAKA ama HAWATAKI....

Historia yake ya uongozi na kupambania haki iko very clear...

Mfano, katika kipindi chake cha miaka 10 ya ubunge wake, ktk jimbo la Singida Mashariki alileta mwamko na mabadiliko sana ktk masuala ya kisheria na haki za watu kiasi ambacho ukifika kule, hata sasa, hata mtoto wa darasa la NNE kule Singida Mashariki huwezi kumwambia kitu kwenye masuala ya haki zake..

Nadhani kila mtu anapenda potential na talent ya mtu huyu ktk masuala ya sheria, siasa, uchumi, diplomasia na uongozi kwa ujumla kuleta mabadiliko ktk nchi hii yote....

Alihujumiwa sana na serikali ya CCM kwa kuhakikisha jimbo lake halipati fedha za miradi ya maendeleo ya kijamii ili tu wananchi wamuone kama kiongozi asiye na manufaa kwao...

Walifanya hivyo awamu ya kwanza 2005 - 2010, haikusaidia kwani wananchi walimchagua tena kwa awamu nyingine ya 2010 - 2015 na kurudia tena awamu ya tatu 2015 - 2020...

CCM wakaona huyu mtu hawezi kutoka kwa mbinu zozote kupitia sanduku la kura. Wakaamua kumaliza mambo kwa njia ya BUNDUKI na RISASI. Nayo ilishindwa kwa kiwango cha kutisha japo waliambulia kumtia ulemavu...

Nakubaliana na wewe mleta mada kuwa, WHAT GOES AROUND COMES AROUND. Tundu Lissu atakuwa kiongozi mkubwa sana nchi...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…