Iran inasema iko tayari kwa makubaliano ya nyuklia ikiwa Marekani itaacha vitisho vya kijeshi

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
17,999
Reaction score
21,560
Iran inasema iko tayari kwa makubaliano ya nyuklia ikiwa Marekani itaacha vitisho vya kijeshi.

Iran iko tayari kushirikiana na Marekani katika mazungumzo siku ya Jumamosi kuhusu mpango wake wa nyuklia "kwa lengo la kusaini makubaliano", Waziri wake wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi amesema.

Lakini Rais wa Marekani Donald Trump lazima kwanza akubali kwamba hakuwezi kuwa na "chaguo la kijeshi", Araghchi alisema, na kuongeza kuwa Iran "kamwe haitakubali kulazimishwa".

Pia alisisitiza kuwa mazungumzo ya Oman hayatakuwa ya moja kwa moja, yakipingana na tangazo la mshangao la Trump siku ya Jumatatu kwamba yatakuwa "mazungumzo ya moja kwa moja".

Trump, ambaye aliiondoa Marekani katika mkataba wa nyuklia wa 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani katika muhula wake wa kwanza, alionya kuwa Iran itakuwa katika "hatari kubwa" ikiwa mazungumzo hayatafanikiwa.

Umelewa kilichoandikwa humo ndani lakin
 
Trump keshadindisha so iran anashika shika majani na kung'ata kucha tu.. Ayatollah alishesema sitaki kisha nataka now eti asitishiwe kupigwa kwani atatoa tu hata nyuma..

Me nilishawaelewa yaani wao upashkuna ndio unawasumbua.. wao kuchonganisha vibaraka wao wapigane huku wakitizama tu sasa washajua kichapo hakikwepeki wameanza kuachia machozi wanahama tu kila siku... walishasema wanaenda Oman sasa nini kipya wanaongea?

Trump kuwaongezea kuwa Israel ndio atapiga hahahaha.. maana majuzi kwenye website zao walifurahi kuwa Netanyahu ameenda Marekani na kurudi mikono mitupu kuwa kukosa uungwaji mkono wa kuipiga Iran wamefurahi haswa
 
Utaundaje Great Israel wakati Kuna Iran ambaye ndo kikwazo?, lazima itafutwe namna ya kumkanyaga Iran kisawasawa, lengo la Israel ni kuzidi kutanua mipaka yake. Israel wana malengo ya muda mrefu, bahati mbaya Hilo litatokea tukiwa wengi humu tushakufa, Kila kipande cha ardhi kitakacho faa kumegwa basi kitamegwa na Israel, waarabu ni watu wapumbavu lakini sisi tumewazidi.
 
Mbona kama unawasuta Sasa...

Back
Top Bottom