Iran kuishambulia Marekani

Iran kuishambulia Marekani

Iran imesema kwamba unaweza kuishambulia Marekani iwapo tu Marekani itaendelea kuisaidia Israel kulipa kisasi.

Iran bila uoga imetamka wazi wazi tutaipiga Marekani vibaya mno na linaweza kuwa shambulio la kihistoria endapo watazidi kuwasaidia Israel kutupiga sisi.

Vyombo mbalimbali vya kijasusi vimesema kuwa iran inapewa kiburi na washirika wake wakuu waliopo pembeni ambao ni Urusi, China na North Korea.

Washirika wa Iran wapo tayari muda wote kuisaidia Iran pindi tu vita vitakapoanza baina ya Marekani, Israel dhidi ya Iran.

Huu unaweza kuwa mgogoro mkubwa utakaoleta ww3
Mkuu nakurekebisha kidogo maeneo ambayo Iran wamesema ni Base za USA zilizopo Mashariki ya kati kama kule Iraq na Saudia Arabia ambapo Iran wamedai ni rahisi zaid kwa wao kuzichakaza kuliko hata kulenga Israel iwapo US itaisaidia Israel katika mashambulizi ya kulipa kisasi
 
Ni kweli amesema haya baada ya raisi wa Iran kutembelea qataria
Pia naye Ayatola ameyasema hayo katika khotuba yake wakati wa swala ya leo Ijumaa kwamba Iran itashambulia maeneo yenye maslahi ya Marekani huko mashariki ya kati endapo marekani itaingilia kumsaidia Myahudi.
Inaonekana kama vile Ayatola amechoka kuishi hapo Iran au kwingineko hapa duniani ana usongo na anatamani sana mabikra 72 na mito ya pombe.
Ngoja tuone itakavyokuwa.
 
Wewe jamaa ni kichekesho sana!

Uzi wako wa kwanza uliandika uongo wako na ukafeli! Umeulizwa maswali kule kwa ulichokiandika hujajibu mpaka sasa!

Umerukia kwenye Uzi mwengine ambao unaandika tu ilimradi unaandika.

Una matatizo gani?
 
kobaz acha kujifariji. huyo iran unayemsifia, juzi alipiga simu kwa marekani kuomba pooo simu haikupokelewa, akakimbia mbio hadi Qatar kuwaomba waongee na Marekani manake yeye simu hazipokelewi. hawajaishia hapo, wametuma ujume India, kwamba kwasababi India ni rafisi wa Israel (wa india ni rafiki kwa mbali wa Iran kwasababu ya uadui wa india na pakistan) kwamba india iongee na israel ili wasiwapige. wameishia tu vitisho kwamba wakipigwa watapiga pakubwa. ila wanajilaumu kwa nini walirusha zile. why? kwa sababu Israel anachofanya ni kupanga zana za ulinzi kudaka mabom yaani amepewa muda wa kuweka mambo yake sawa alafu anapiga.

atapiga wapi? mpango wa kwanza ni kupiga kituo cha nuclear enrichment ambacho kwa miaka mingi mno Iran wamekuwa wakikijenga, kupiga kisiwa cha uzalishaji mafuta ambacho leo hii Iran wameonekana wakiondoa baadhi ya mitambo, na kupiga kituo cha kuzalisha umeme. maeneo hayo yakipigwa, iran imerudishwa nyuma miaka rundo kiuchumi na itashindwa kuendesha nchi. tangu juzi wananchi wa iran wamejaa ATM kuchukua pesa na kuzibadilisha kuwa dola ya kimarekani in anticipation ya kukimbia nchi iwe rahisi wakiwa wakimbizi, ATM hazina pesa huko iran. shughuli za kiuchumi haziendi kwa amani na uchumi unashuka, ndio maana kamaumesikiliza hotuba ya ayatolah leo amesema "adui anapigana nasi vita ya kiuchumi, kisaikolojia na kimwili". trauma wanayoishi nayo huko haina mfano na hasa kwasababu marekani ameiruhusu Israel kupiga jambo ambalo miezi ya nyuma hakufanya.

Marekani ina vituo vya kijeshi kuzunguka iran yote, saudia na nchi za kiarabu zinategemeana na Marekani sana, watampa anga. huwa wanadanganya kwamba hawatampa anga ili iran ajisahau halafu wanampa, kwasababu ni maadui wa iran washia. vita ikianza, jua UK, ufaransa, Ujerumani na nchi zingine zitaingia pia. UK kwa sasa wana zana za kutungua rocket za mionzi (razor) ambazo wanampango au inawezekana washazipeleka Israel.

kwa kifupi, tuombe Mungu Israel asipige vibaya, au hata akipiga iran ichuchumae kimyaa ili vita isiendelee kwasababu watakaoumia ni waafrica, maisha yatapanda sana. na kama haujui, kuna uwezekano mkubwa hata jordan na waarabu waliambiwa waziache tu hizo rocket karusha juzi zidondoke israel kwasababu marekani na israel walikuwa na bado wanatamani sana iran aingie kwenye vita kubwa ili waisambaratishe kabisa kabisa.

hifadhi huu uzi, kuna siku utaurudia kujikumbusha wakati iran itakuwa iraq ya sasa.
We kenge wala sikusoma ulicho andika nilishia ilipo sema Iran kawabembeleza US na india nikafahamu wazi mtoto anaropoka sio mtu ana akili zake timamu.

US anaomba poa na Iran miaka na dalili mpaa leo wanamazungumzo ya siri kule Oman. Uliza wenye akili watakuambia.

Rais wa Iran mpya alipo ingia alisema Iran na US ni kama ndugu hio ni politics sio kwamba kawaomba poa na US.

Huyo huyo Rais alisema hawana haja ya kuwa support Hezbullah leo kasema hatawacha kuwasupport.

Usiwe kila ukisikia mwenye siasa anacho ongea ukakiamini.

Nipe dalili unacho ongea mpaa pale uliposema Iran anambembeleza India ili Israel asimpige sababu sikutaka kusoma utumbo wako nimeona wote ni uwongo mtupu.
 
Pia naye Ayatola ameyasema hayo katika khotuba yake wakati wa swala ya leo Ijumaa kwamba Iran itashambulia maeneo yenye maslahi ya Marekani huko mashariki ya kati endapo marekani itaingilia kumsaidia Myahudi.
Inaonekana kama vile Ayatola amechoka kuishi hapo Iran au kwingineko hapa duniani ana usongo na anatamani sana mabikra 72 na mito ya pombe.
Ngoja tuone itakavyokuwa.
Heri.kuwahi mabikira 72,kuliko kwenda kupakatwa na kidume Ibrahim,kama Lazaro alivyopakatwa na huyo kidume Ibrahim.
 
Heri.kuwahi mabikira 72,kuliko kwenda kupakatwa na kidume Ibrahim,kama Lazaro alivyopakatwa na huyo kidume Ibrahim.
Lakini mbona imeandikwa: ".........alimwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake..... ?(Luk.16:19-31) au mtu kuwa kifuani ndo kupakatwa?
 
Kwenye vita Kila kitu kinaweza tokea,it took 20 yrs for U.S to fight Taliban and last handling military devices to its enemy🤣😀😀😀
Usa hawakua na shida na Taleban, let us be clear on this, shida yao ilikua Osama Bin Laden ambaye alikua anashirikiana na Taleban pale Afghanistan, Osama wameisha muua, Taleban wa kazi gani tena?
 
We kenge wala sikusoma ulicho andika nilishia ilipo sema Iran kawabembeleza US na india nikafahamu wazi mtoto anaropoka sio mtu ana akili zake timamu.

US anaomba poa na Iran miaka na dalili mpaa leo wanamazungumzo ya siri kule Oman. Uliza wenye akili watakuambia.

Rais wa Iran mpya alipo ingia alisema Iran na US ni kama ndugu hio ni politics sio kwamba kawaomba poa na US.

Huyo huyo Rais alisema hawana haja ya kuwa support Hezbullah leo kasema hatawacha kuwasupport.

Usiwe kila ukisikia mwenye siasa anacho ongea ukakiamini.

Nipe dalili unacho ongea mpaa pale uliposema Iran anambembeleza India ili Israel asimpige sababu sikutaka kusoma utumbo wako nimeona wote ni uwongo mtupu.
huwezi kusoma kwasababu huwa mnakimbia kisomo kama kawaida yako. hata ungesoma usingeelewa, bora haujasoma kabisa.
 
Yaani Iran ni typical mswahili anaongea maneno mengi yasiyo na maana yoyote, sasa akikaa kimya halafu afanye hayo anayo jigamba kuyafanya atakuwa amepoteza nini.

Iran bure kabisa.
 
Umasikini unapotaka kumfika mtu, unanguvu za ajabu, na unapokuja, humwelekeza jambo la kufanya na kumhakikishia kuwa hatapata hasara,

Hii ni hasa mtu anapoacha ku focus mambo yake ambayo kwayo yanampa faida

Eti Iran apige USA

Hii ndiyo tofauti ya mzungu na mifano ya wazungu
Nadhani hujamwelewa vizuri! kasema Iran inatiwa kiburi nawashilika wake, sawa na Izirael inavyopewa sapoti nawashilika wake.
 
Usa hawakua na shida na Taleban, let us be clear on this, shida yao ilikua Osama Bin Laden ambaye alikua anashirikiana na Taleban pale Afghanistan, Osama wameisha muua, Taleban wa kazi gani tena?
Kwanini hawakuondoka tu baada ya kumuua Osama ambae walikua ndio shida nae
 
Ndio matatizo ya maendeleo , mkishapata maendeleo mnaanza kutafuta mtu wa kupigana nae.
Uko sahihi mkuu. Maana sijamuona mwenye njaa anakunja ngumu kupigana, ila aliyeshiba hata kiporo tu anavitisho na mkwara kuliko dubu na simba.
 
Irani alishamwanbia USA kuwa kuanzisha vita na Irani nitapiga kwako USA Moja Kwa Moja Mimi tofauti na hao wengine ukipigana nao wanapiga katika base zako

Na USA hakuna kitu anachoogopa kama nchi yake kuwa uwanja wa vita na ndio maana Huwa anapigana na watu Kwa kuchagua nchi za wajinga wajinga ndio ziwe uwanja wa vita kama Ukraine na Israel
 
Israel tu kamgeuza shamba la bibi, kashavuna viongozi wa juu wa Iran na wanasayansi wake kibao.

Iran kaishia kurusha mabomu bila kusababisha madhara makubwa kwa wahusika, sasa atamuweza USA mfupa uliomshinda fisi kuutafuna?.

Aache maigizo ya futuhi asubiri Yahood kuendeleza alipoishia
Wewe ndiyo unajua hakuna madhara kwa sababu imeamuliwa ujue hivyo
 
Back
Top Bottom