IRAN: Kuna hali ya misuguano ya kimamlaka kati ya Abbas Araghchi na viongozi wa IRGC kuhusu udhibiti wa Mlango wa Hormuz

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,475
Reaction score
12,281
Siku ya Ijumaa, Aprili 17, 2026, Waziri wa Mambo ya Nje, Abbas Araghchi, alitangaza kupitia mtandao wa X kuwa Mlango wa Hormuz uko "wazi kabisa" kwa meli zote za kibiashara. Alidai uamuzi huo umefikiwa kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano huko Lebanon.

Ndani ya saa 24, viongozi wa IRGC walitoa tamko kali la kupinga hatua hiyo. Jeshi hilo lilikosoa vikali kauli ya Araghchi na kusisitiza kuwa mlango huo utabaki chini ya udhibiti wao wa kijeshi na hautafunguliwa mpaka Marekani iondoe kizuizi chake cha majini (naval blockade) dhidi ya bandari za Iran.

IRGC wamechukua hatua za kivitendo kuzuia meli na wametangaza rasmi kuwa Mlango wa Hormuz umefungwa tena kuanzia Jumamosi jioni, Aprili 18. Hatua hii imeonekana kama mapinduzi ya ndani ya IRGC dhidi ya sera za kidiplomasia za Araghchi ili kuonyesha nani mwenye mamlaka halisi juu ya njia hiyo muhimu ya mafuta duniani.

NI NINI HASWA KINAENDELEA HAPA?

• Kuna mpasuko kati ya "reformists/diplomats" (Araghchi) wanaotaka kupunguza vikwazo kupitia majadiliano, na "hardliners" (IRGC) wanaotaka kutumia nguvu ya kijeshi kama karata ya shinikizo.

• Ripoti zinaonyesha kuwa IRGC wanahisi Araghchi alitoa ahadi za kimataifa bila ridhaa yao, jambo ambalo wanajihami nalo ili kulinda hadhi yao ya usalama.

• IRGC wanataka kudhibiti sera nzima ya majadiliano na Marekani na washirika wake, huku wakiona hatua ya Araghchi kama kudhoofisha msimamo wa Iran.
20260419_145454.jpg
 
Trump aamue moja, kutumia nguvu za kijeshi kuleta ufumbuzi wa huo mgogoro au kufungasha virago na kuondoka mashariki ya kati kwa sababu sasa hamna kinachoendelea ni kupoteza muda tu huku uchumi wa dunia ukiendelea kuporomoka.
 
Siku ya Ijumaa, Aprili 17, 2026, Waziri wa Mambo ya Nje, Abbas Araghchi, alitangaza kupitia mtandao wa X kuwa Mlango wa Hormuz uko "wazi kabisa" kwa meli zote za kibiashara. Alidai uamuzi huo umefikiwa kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano huko Lebanon.

Ndani ya saa 24, viongozi wa IRGC walitoa tamko kali la kupinga hatua hiyo. Jeshi hilo lilikosoa vikali kauli ya Araghchi na kusisitiza kuwa mlango huo utabaki chini ya udhibiti wao wa kijeshi na hautafunguliwa mpaka Marekani iondoe kizuizi chake cha majini (naval blockade) dhidi ya bandari za Iran.

IRGC wamechukua hatua za kivitendo kuzuia meli na wametangaza rasmi kuwa Mlango wa Hormuz umefungwa tena kuanzia Jumamosi jioni, Aprili 18. Hatua hii imeonekana kama mapinduzi ya ndani ya IRGC dhidi ya sera za kidiplomasia za Araghchi ili kuonyesha nani mwenye mamlaka halisi juu ya njia hiyo muhimu ya mafuta duniani.

NI NINI HASWA KINAENDELEA HAPA?

• Kuna mpasuko kati ya "reformists/diplomats" (Araghchi) wanaotaka kupunguza vikwazo kupitia majadiliano, na "hardliners" (IRGC) wanaotaka kutumia nguvu ya kijeshi kama karata ya shinikizo.

• Ripoti zinaonyesha kuwa IRGC wanahisi Araghchi alitoa ahadi za kimataifa bila ridhaa yao, jambo ambalo wanajihami nalo ili kulinda hadhi yao ya usalama.

• IRGC wanataka kudhibiti sera nzima ya majadiliano na Marekani na washirika wake, huku wakiona hatua ya Araghchi kama kudhoofisha msimamo wa Iran.View attachment 3575424

Dogolas zitto junior
 
Trump aamue moja, kutumia nguvu za kijeshi kuleta ufumbuzi wa huo mgogoro au kufungasha virago na kuondoka mashariki ya kati kwa sababu sasa hamna kinachoendelea ni kupoteza muda tu huku uchumi wa dunia ukiendelea kuporomoka.
Unadhani ni nguvu gani za kijeshi ambazo mpaka sasa haijatumika zinazo weza kutatua hichi kinacho endelea?
 
Kwani anayetoa maelekezo ni waziri wa mambo ya nje au Ayatollah? Mnajua hamjitambui. Kazi ya mwanadiplomasia ni kutafuta suluhu mezani ndio ambacho Arragarchi anafanya toka vita inaanza wala hajaanza ijumaa.

Kutofautiana ingekua pale Ayatollah atoe maelekezo alafu IRGC ipinge ila chochote chini ya hapo ni maoni tu na hayana madhara maana Arragarchi anaweza ondolewa uwaziri akawekwa mwingine so ni non consequential kabisa.
 
We Khayatolla mara ya mwisho umemwona akitoa maelekezo ni lini? 😀
 
Trump aamue moja, kutumia nguvu za kijeshi kuleta ufumbuzi wa huo mgogoro au kufungasha virago na kuondoka mashariki ya kati kwa sababu sasa hamna kinachoendelea ni kupoteza muda tu huku uchumi wa dunia ukiendelea kuporomoka.

Japo leo nakuunga mkono mzozo huu ulipo kutatuliwa kwa mazungumzo haiwezekani !!

sababu tayali Trump kaitupa iyo fursa pale alipochagua Vita badala ya mazungumzo!!!

Kwasasa Trump nikama anatafuta mzozo mkubwa KiDunia tawala nyingi Duniani zishaanza kumchukia mana anadhiweka rohoo juu Kiusalama
kwasababu ya Mafuta.!!!

Kwasasa hakuna chaguo lengine njia ni moja tu !!
Marekani kupigana Vita tena ya Ardhini tu,,

au. Wasepe na kukubali kushindwa na kuporomoka kukubwa Kimataifa

watakuwa wameporomoka
sekta 3 kubwa

1( kitechnology

2( kiuchumi pamoja na pesa yao.

3( kuwa Nijesh lenye nguvu
kimataifa ✍️
 
Mbona IRGC jana tu wametoa muongozo kuwa meli hazipiti sababu Ayatollah katoa maelekezo. So wana internal mechanisms za kuwasiliana au unadhani huwa wanawasiliana kupitia social media kama Trump?
Hao Wairan hata hiyo mitandao ya kijamii tu pamoja na kuzifunga ili kuficha uharibifu waliofanyiwa usijulikane nje lakini pia hawawezi kuzitumia kwa sababu za kiusalama.

Meli kama hazipiti hata na za kwao pia hazipiti vilevile. Iran lazima wafahamu vema kwamba ujeuri katu hautaweza kuwasaida.
 
Marekani wao ujeuri utawasaidia?!!
IRAN aendelee kupambana tuu kuilinda hadhi yake,Mafuta yapande bei hata yakiwa 7000 per lita mpaka watanganyika tunene kwa lugha
 
Trump aamue moja, kutumia nguvu za kijeshi kuleta ufumbuzi wa huo mgogoro au kufungasha virago na kuondoka mashariki ya kati kwa sababu sasa hamna kinachoendelea ni kupoteza muda tu huku uchumi wa dunia ukiendelea kuporomoka.
Kuna muda saa mbovu husema ukweli
Marekani hana chake tena hapo si kashikwa akili na pakanyau sasa anadhalilika
 
Hao Wairan hata hiyo mitandao ya kijamii tu pamoja na kuzifunga ili kuficha uharibifu waliofanyiwa usijulikane nje lakini pia hawawezi kuzitumia kwa sababu za kiusalama.

Meli kama hazipiti hata na za kwao pia hazipiti vilevile. Iran lazima wafahamu vema kwamba ujeuri katu hautaweza kuwasaida.
Mbona mnalalamika lalamika sana huku
Mlikua munapitishwa free pale hormuz mukaona munafaidi
Sasa ule chuma au upite angani no more
 
Hao Wairan hata hiyo mitandao ya kijamii tu pamoja na kuzifunga ili kuficha uharibifu waliofanyiwa usijulikane nje lakini pia hawawezi kuzitumia kwa sababu za kiusalama.
Israel ina mesia censorship kubwa zaidi ukikutwa umepost uharibifu unawekwa ndani. Na hao waandishi kutoka mataifa mbalimbali kuja israel na kihere here kuripoti so far wameuwawa zaidi ya 30.

Pia hawauwawi sababu ya teknolojia, mara nyingi tu israel inaweka dau kubwa kwa mtu atakayetaja alipo kiongozi wa Iran mfano Mojtaba imewekwa dau la zaidi ya USD 10 Million maana yake ukitonya tu unapewa TSH 22 billion. Mnapenda sana ku overrate technology ya israel wakati ilifeli kuwapata mateka kwenye kamji kadogo kama Gaza.
 
Back
Top Bottom