Iran - Nchi inayohofiwa zaidi ulimwenguni na Marekani kuliko Taifa lolote lile duniani

Iran - Nchi inayohofiwa zaidi ulimwenguni na Marekani kuliko Taifa lolote lile duniani

Ndio ninachokuambia hapo sasa Bluetooth ina patents 30,000 kila sehemu wame contribute.

Huo uliotaja ni patent moja Tu haimaanishi Gps yote imetengenezwa na patent moja kuna maelfu ya patents ya GPS, China pekee mwaka 2023 amefill patents nyingi za GPS/position system kuliko hata Us mwenyewe. Kampuni moja Tu kama Here Maps ina patent kama 5000 zinazohusiana na positioning system.
Mkuu asipokuelewa wewe basi hatumuelewa hata malaika gabriel akishuka toka mbinguni.
 
Israel ndio nchi ya hovyo kuwahi kutokea. Haina vikwazo, na inabebwa na nchi za magharibi ili waipe u-super power wa mchongo pale Middle East, lkn wapi, mpaka leo bado inategemea msaada wa ulinzi kutoka Marekani.

Nchi ipo Middle East, lkn bajeti ya ulinzi, madawa nk vinatoka Marekani. Sasa hiyo nchi inatofauti gani na nchi zetu za shithole ambazo hujiendesha kupitia misaada ya nchi za nje?

Umeshawahi kujiuliza kama Israel isingekuwa tegemezi kwa nchi zingine kama Marekani na washirika wake, leo hii Israel wangepata wapi silaha, na mifumo ya ulinzi?

Maana 90% ya bajeti ya ulinzi wa Israel, pamoja na silaha, mifumo ya ulinzi na madawa vinatoka Marekani? Je Marekani isingekuwepo, bajeti ya ulinzi na silaha za kisasa wangezipata wapi?

Umewahi kujiuliza kama Israel ambayo haina vikwazo inategemea ulinzi na silaha nyingi kutoka nje, je ingetokea kuwekewa vikwazo silaha za kupigana na Iran wangezitoa wapi wakati wanaonekana ni tegemezi kwa nchi zingine zenye nguvu?

Tukija kwa Iran kila mtu anafahamu uzito wa vikwazo ilivyowekewa, lkn kamwe haijawahi kutegemea bajeti ya ulinzi kutoka kwa nchi nyingine.

Wanatengeneza silaha zao wao wenyewe, na mifumo yao ya kujilinda wao wenyewe. Na hapo isingekua vikwazo vikali vya kiuchumi, basi wangetengeneza hata ndege nzuri za kivita. Ila kutokana na vikwazo vya kiuchumi na gharama za utengenezaji ndomaana imekuwa ngumu kutengeneza ndege hizo.

Sasa jiulize kama Iran ingepata opportunity ile walio nayo Israel leo hii kwa aina ya vichwa na akili zao si wangekuwa mbali mno kijeshi, teknolojia, uchumi nk.

Israel inabebwa zaidi na historia ya dini, kwamba ni taifa teule. Hivyo hata kama inaendeshwa hovyo, bado watu wataendelea kuisifu tu huku wakishuhudia kwa macho yao kwamba inabebwa tu na nchi za Magharibi bila kuwa na uwezo wowote wa kupigana vita hata ya miezi 2 bila msaada kutoka nje.
Israel ni jimbo la marekani Sasa ulitaka apate silaha kutoka wapi bana?

Iran zaidi ya drone na makombora silaha gani anayotengeneza mwenyewe?
 
Ndio ninachokuambia hapo sasa Bluetooth ina patents 30,000 kila sehemu wame contribute.

Huo uliotaja ni patent moja Tu haimaanishi Gps yote imetengenezwa na patent moja kuna maelfu ya patents ya GPS, China pekee mwaka 2023 amefill patents nyingi za GPS/position system kuliko hata Us mwenyewe. Kampuni moja Tu kama Here Maps ina patent kama 5000 zinazohusiana na positioning system.
Sasa hiyo patent si ndio technology ama?
 
Niaje waungwana.

Kama kawaida, leo nimekuja kutoa somo kamili kwa wale wayahudi uchwara wa Tandale kwa Mtogole, wasiojua nguvu halisi ya Iran katika miaka iliyopita, iliyopo na ijayo.

Bila kuongelea kuhusu dola la Iran (Persia Empire) ambayo ilitawala eneo zima la Mashariki ya kati kabla hata ya kuzaliwa Uyahudi, Israel, Firauni, Ibrahim, Yesu nk.

Leo napenda kuongelea Iran ya leo ambayo imeweza kushinda vita vya maneno na vitendo, dhidi ya maadui zake wakubwa duniani, ambao ni Marekani, Israel na kwa mbali nchi za Ulaya Magharibi.

Baada ya Marekani, Israel na washirika wao kushindwa kuidhibiti Iran kwa njia ya vita baridi, waliamua kuwatumia waarab njaa kama vile Saudi Arabia, Jordan, Iraq nk kuitenga nchi hiyo kupitia mgongo wa utofauti wa kiimani kama vile ushia na usunni. Vita hii ilileta mgawanyiko mkubwa, haswa ukizingatia waarab wengi hawana elimu yoyote ya kuweza kutambua kile kinachopandikizwa juu yao na jirani yao.

Baada ya kufanikiwa kupandikiza chuki hizo, wakaangalia nchi 1 wapo ambayo wakiipa silaha za kutosha itaweza kuingia vitani na Iran, kupambana na Iran, kuishinda Iran, kuuangusha utawala wa Iran na hatimae kuweka kibaraka wao ambae atakuwa tayari kufata yale yanayotakiwa na nchi hizo zilizotoa msaada wa kivita.

Basi bwana baada ya kukaa chini kutafakari, wakaona Iraq ndio nchi pekee itakayoweza kukamilisha mission kutokana na Jiografia, aina ya kiongozi (Sadam) plus propaganda za ki ushia na ki usunni. Bila kuchelewesha muda, Sadam akawezeshwa akaingia mzigoni kwa kushtukiza huku Iran Lisa haijajipanga, haina backup, Plus vikwazo vikali vya kiuchumi na silaha. Vita ile ilienda miaka 8, from 1980 hadi 1988, huku Iraq ikipewa kila aina ya silaha na Marekani ili iweze kushinda vita hiyo. Pamoja na Iran kukosa backup na vikwazo juu lkn iliweza kulinda mipaka yake na uongozi wake hadi kupelekea Sadam mwenyewe na maboss zake kunyoosha mikono ya kuomba poo ili vita iishe.

Baada ya vita kuisha bila Marekani na washirika wake kupata walichokitaka, walichukia na kuanza kuonesha chuki za wazi kwa Sadam baada ya kuwaingiza hasara ya silaha Kwa muda wa miaka 8, bila ushindi wowote. Chuki hii dhidi ya Sadam iliendelea, huku Sadam nae akipanga kuzitumia silaha zilizobaki kuishambulia Israel ambayo nayo ilikuwa kwenye mission ya kuitumia Iraq kama daraja la kuuangusha utawala wa Ayatollah na serikali yake.

Baada ya mbinu zile za ushia, sunni na vita kupitia Iraq kukwama, wakaja na mbinu za kutengeneza makundi ya mujahidina ili wayatumie kuyumbisha usalama wa eneo zima linaloizunguka Iran, Na baadae wayatumie kuingia Iran kufanya ugaidi na hatimae waanzishe vita dhidi ya serikali ya Iran. Iran ililiona hilo na kuamua kutengeneza na yenyewe makundi ya wapiganaji katika eneo linaloizunguka Israel na washirika wao wa Middle East. Ili wao wakimwaga ugali na yeye amwage mboga.

Lakini kama hiyo haitoshi Iran ikaendelea kujiimarisha Kwa teknolojia yake mwenyewe, silaha zao wenyewe nk.

Baada ya mbinu zote kukwama topeni, Marekani akaamua kumtumia mshirika wake alie karibu na eneo hilo (Israel) kufanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya viongozi wa jeshi, serikali na miundombinu ya ulinzi, kwa lengo la kuuangusha utawala walioushindwa kuuangusha miaka mingi iliyopita, huku Marekani ikiahidi kutoa support yoyote pale itapohitajika kufanya hivyo.

Intelejensia yao (US na Israel) zilijua kwamba baada ya ambush kufanyika, hakutakuwa na mwanajeshi hata 1 atakae kuwa na uwezo wa kushika hata kisu kuilinda nchi yake. Waliamini mbinu iliyotumika kuuangusha utawala wa Sadam na Ghadafi ingeweza tena kutumika kuuangusha utawala wa Jemedari Ayatollah. Wakasahau kwamba wale kina Sadam na Ghadafi walikuwa ni Waarab ambao nchi zao hazina historia sawa hata kidogo na Iran ambao ni waajemi, watu wenye akili na uwezo wa kuweza kupigana vita yoyote ile, tangu miaka na miaka.

Baada ya maandalizi ya kutosha Israel imapiga ambush. Lakini kilichotokea masaa kadhaa tu baadae kiliiwacha mdomo wazi Dunia. Kwani Pamoja na maadui kutangaza kufunga anga, na kuweka maelfu ya mifumo ya kuzuia na kulinda anga kuanzia Saudi Arabia, Jordan na Israel kwenyewe, lkn bado mifumo hiyo iliendelea kufanywa chujio la nazi baada ya makombora hatari ya Iran kupenya mifumo hiyo bila kikwazo chochote, saa yoyote na eneo lolote.

Baada ya vita vya siku 12 huku Israel ikipokea kila aina ya silaha kutoka Marekani, UK, Ujerumani, Ufaransa, Italy, Belgium, Uholanzi nk. Netanyahu mwenyewe aliamua kuomba poo, baada ya maelfu ya waisrael wakiwemo mkewe na ndugu zake kukimbilia Poland katika nchi ya asili ya Benjamin Netanyahu.

Sasa vita iliisha huku waliovizia wakiwa hoi. Leo hii wanajipanga tena kwenda kupima upepo ambao bila shaka utageuka kimbunga chenye kusomba miti, nyumba, ndege, meli na magari.

Wakati Venezuela walienda kumchukua mtu bila kutumia risasi hata 1. Huku wanakwenda kushuhudia jinsi meli zao za kijeshi zinavyokwenda kuzamishwa majini kama karatasi bila huku mifumo yao ya kuzuia makombora ikiishia kuzuia nzi na vipepeo tu kama ilivyokuwa Israel siku ile.

Ogopa nchi ambayo pamoja na vikwazo vya miaka zaidi ya 50, lkn bado ni tishio kubwa kwa nchi zote zenye nguvu duniani kama vile Marekani, Israel, UK, Ufaransa nk.

Nchi ambayo, raisi wa Marekani (taifa lenye nguvu) fedha, teknolojia na intelejensia kubwa duniani (Trump) anaogopa itamuua.

Trump hakuwahi kuihofia Venezuela na nchi yoyote yenye uadui nao. Lakini kwa Iran ameonesha wasi wasi mkubwa juu ya maisha yake dhidi ya nchi hiyo.

So bila shaka Trump anasubiri ramadhani ndio aanze kuishambulia Iran, lkn nawahakikishia kuwa baada ya majibu ya Iran kuleta uharibifu mkubwa kwa jeshi, na vifaa vya Marekani. Trump ndo atakuwa mtu kwanza kuomba Iran ije mezani kufanya mazungumzo ya kusitisha vita kwa story ya kwamba Iran imekubaliana na baadhi ya masharti yake ili iondolewe vikwazo.


Mlale usingizi mnono.View attachment 3534933View attachment 3534935
Tuonyeshe na madhara yalioyokea iran
 
kiufunuo maono aliyoyafunua BWANA YESU kwa mtumishi wake
1)NCHI YA IRAN ndiyo inayomiliki silaha ya bomu la nyuklia hatari zaidi duniani kuliko nchi yeyote duniani,na endapo wakizitumia zitaleta madhara kwa sehemu kubwa zaidi ya dunia

2)YESU hataruhusu hizo silaha hatari zaidi na zenye uwezo wa kuharibu sehemu kubwa ya dunia
YESU HATARUHUSU IRANI izitumie silaha hizo KABLA HAJAWANYAKUA watakatifu wake waliopo DUNIANI.

kwenye maono ulimwengu wa ROHO mtumishi wa MUNGU alipelekwa mpaka nchi ya irani akaonyeshwa silaha hizo zilipofichwa kwa siri ambapo hakuna mtu anayejua zilipo ,ila YESU alimuonyesha mtumishi wake ..

ANGALIA mabomu haya ..usiyaone hivi ..haya mabomu ya nyuklia ni hatari zaidi kuliko mabomu yote duniani..na hakuna nchi nyingine yeyote duniani inamiliki na yamefuchwa sehemu ya siri hakuna mtu mwingine anajua ...kwa siri sana ..sehemu ya siri sana.

YESU hataruhusu irani iyatumie kabla hajawaondoa watu wake..yatasababisha madhara makubwa duniani sehemu kubwa zaidi.
(UJUMBE WA YESU...UNYAKUO WA WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI UMEKARIBIA SANA)
mtakatifu na azidi kutakaswa ,mwenye dhambi azidi kutenda

yafue mavazi yako yawe meupe...uwe tayari...
 
Sasa hiyo patent si ndio technology ama?
Ukifanya research na kugundua kitu hata kiwe kidogo vipi unakuwa awarded patent, kutengeneza product yoyote ya kisasa unatumia maelfu ya Patents, hakuna technology ya kisasa iliotengenezwa na MTU mmoja, ndio maana sio Jambo la ajabu kukuta Technology critical za Mmarekani kuna Mchina ama Muiran and vice versa.
 
Israel ni jimbo la marekani Sasa ulitaka apate silaha kutoka wapi bana?
Kumbe mwaka jana Iran ilikuwa inapambana na Marekani hadi Marekani ikaomba poo!!

Basi nimekuelewa.
Iran zaidi ya drone na makombora silaha gani anayotengeneza mwenyewe?
Kama inatengeneza drone na makombora pekee kwanini iwekewe vikwazo vya silaha?

Waitolee vikwazo vya silaha na uchumi, halaf baada ya miaka mi5 uje uone silaha atakazounda.
 
Sijasoma ila nahisi tu hamna la maana. Ukiona mtu anaandika sanaa kushawishi hoja yake, ujue hoja haina mashiko. Yaani ni HOJA YA NGUVU NA SI NGUVU YA HOJA.
 
Ukifanya research na kugundua kitu hata kiwe kidogo vipi unakuwa awarded patent, kutengeneza product yoyote ya kisasa unatumia maelfu ya Patents, hakuna technology ya kisasa iliotengenezwa na MTU mmoja, ndio maana sio Jambo la ajabu kukuta Technology critical za Mmarekani kuna Mchina ama Muiran and vice versa.
Sasa si ndo kugundua kwenyewe? Gunduzi zote za technology kuanzia sayansi inaanza ni muendelezo wa lililogunduliwa nyuma. Na ugunduzi husika kwa muda husika ndo unafanya product husika iwe Kama ilivo kwa muda huo husika ilipogunduliwa hiyo technology
 
Kumbe mwaka jana Iran ilikuwa inapambana na Marekani hadi Marekani ikaomba poo!!

Basi nimekuelewa.

Kama inatengeneza drone na makombora pekee kwanini iwekewe vikwazo vya silaha?

Waitolee vikwazo vya silaha na uchumi, halaf baada ya miaka mi5 uje uone silaha atakazounda.
Sijawah ona Iran imepambana na marekani.

Inawekewa vikwazo vya silaha sababu inataka kuiangamiza israel
 
Sasa si ndo kugundua kwenyewe? Gunduzi zote za technology kuanzia sayansi inaanza ni muendelezo wa lililogunduliwa nyuma. Na ugunduzi husika kwa muda husika ndo unafanya product husika iwe Kama ilivo kwa muda huo husika ilipogunduliwa hiyo technology
Yani umenipinga wee, mpaka mwisho umechukua point yangu kama point yako. Hichi si ndio ulikua unakipinga huko nyuma nikikuelekeza namna wanasayansi wa Marekani na Iran wanavyoshirikiana na bomu moja linahusisha maelfu ya wanasayansi?
 
Yani umenipinga wee, mpaka mwisho umechukua point yangu kama point yako. Hichi si ndio ulikua unakipinga huko nyuma nikikuelekeza namna wanasayansi wa Marekani na Iran wanavyoshirikiana na bomu moja linahusisha maelfu ya wanasayansi?
Hakuna sehem niliyosema wanasayansi wa Iran wanashirikiana na WA US. Na hicho kitu hakipo kwa maslahi ya nchi husika hasa kwa zile field muhimu. Pia kuanzia mwanzo nimesema ugunduzi wowote wa kisayansi ni muendelezo wa gunduzi za nyuma.. pia wewe ulisema bomu la nuclear halijagunduliwa..Sasa Kama halijagunduliwa mbona mwanzo halikuwepo? na Kama unasema ilikua ni just kuungamisha zile technology na kuunda kitu kimoja je iweje nchi zingine zilishindwa akaweza marekani kwani hao wanasayansi wa nchi zingine walikua hawawezi kuungamisha hizo technology na formula za hesabu na fizikia na wao kutengeneza bomu?

Iweje urusi akaenda kuiba technology hiyo kutoka marekani hadi na yeye akatengeneza la kwake? Iweje Iran anatengenezewa nuclear na urusi kwani si ana wanasayansi wake kwa Nini wasichukue hizo technology wanazoshirikiana na marekani na wao wakatengeneza la kwao au we unafikiri kutengeneza nuclear bomb si simpo tuu Kama kucheza kikoba?
 
Back
Top Bottom