Ngoja nikupe darasa shehe
Mgogoro wa Israel na Arabs ni wa kidini 100%. Kama mgogoro huo ungekua ni ardhi basi ungeshaisha muda sana. Hiyo asilimia unayosema ameichukua Israel ni kasehem kadogo sana hapo mashariki ya kati Yani ukikaangalia ni Hadi umulike na tochi.
Iko hivo hapo mashariki ya kati zimezaliwa dini tatu.. Judaism, Christianity na Islam
Judaism ilikuja na Nabii Musa kupitia torati, Christianity kupitia Yesu ikaja Injili ( Huu wote ni uzao wa ahadi wa Ibrahimu) then ikaja Islam kupitia Nabii Muhammad (uzao wa Ibrahimu lakini nje ya ahadi)
Alivokuja Yesu akasema mimi ndo njia ya uzima na kweli na mimi nimetumwa na Baba kwa hiyo hakuna haja ya torati ya Musa Tena Yale mambo ya kuchinja yashapitwa na wakati sababu mimi ndie kafara yenyewe. Bada ya Yesu akaja Muhammad nae akaja na utume wake na akasema Musa na Yesu (Issa bin Mariam) wale ni manabii tu ila mimi ndo Nabii wa mwisho na WA ukweli na hapatakua Tena na Nabii zaidi yangu mimi.
Hii inamaanisha nini:
Muhammad alikua anamaanisha kwamba Uislam ndio dini inayotakiwa itawale juu ya ukristo na uyahudi. Na ndio maana Al Aqsa ikajengwa lilipojengwa hekalu la suleimaani Ili kuonesha uhalali huo. Sasa ikitokea ikaonekana ukristo na uyahudi unatawala juu ya Uislam basi hapo kwa maana ingine Muhammad kadanganya. Hili ni tatizo kubwa kwa waarabu.
Sasa nakujibu hoja zako:
Ni kweli kwamba wayahudi wameishi na waislamu mashariki ya kati miaka mingi sana Tena wakiwa wamejenga na masinagogi yao. Lakini hawakua na nguvu yeyote.. Islam ilienezwa kwa upanga ikasambaa kote mashariki ya kati na hivo ndo ikawa yenye nguvu. wayahudi mashariki ya kati walitawanywa sehem mbalimbali duniani hapo mashariki ya kati wakabaki kama theluthi Moja tu ya population yao. Hivo kwa hapo waarabu hawakua na ugomvi wowote na wayahudi sababu walikuwa ni jamii ya minority isiyo na nguvu yeyote.
Wayahudi baada ya kuzunguruka Dunia nzima na kupata mateso huko ugenini wakaja kujua kumbe wana kwao ardhi ya mababu zao, wakaanzisha movement ya kurudi kwao. TATIZO LIKAANZIA HAPA.
Yule aliekua anajiona mtawala wa wenzake Sasa akaanza kutawaliwa. Je unafikiri hata kama ni wewe ungekubali? Islam ilivoona Jews imepata taifa rasmi mwaka 1948 ikaanzisha vita na uhasama dhidi ya taifa Hilo sababu iliona Uislamu hautatawala Tena Mashariki ya kati Bali ni Uyahudi utachukua hatamu uliokua nayo mwanzo. Uyahudi unataka kubomoa msikiti wa al Aqsa Ili ujenge hekalu lao like la zamani.
hapo lazima ni kwa njia ya vita. Mwenye nguvu ndo anabeba mali.
Hii ni ishara mbaya kwa Islam maana Uyahudi ukiwa juu ya Uislam ni kwamba Muhammad ataonekana sio Nabii wa Mungu
So Acha kupotosha