IRAN - "Victim Card Strategy" Inawaumiza Kichwa Wazungu na Wazayuni wa Israel

Hapo umejibu ulichoulizwa au umeweka ramani nione?Bwana mkubwa acha vituko.Miaka 40 haujafikisha ila unapenda uitwe kizee.
 
Jadili hoja kijana. Achana na mipasho. Haina tija yoyote. Hoja yangu ni:

IRAN - "Victim Card Strategy" Inawaumiza Kichwa Wazungu na Wazayuni wa Israel​

Huo mkakati wewe ndiye unawaza kwamba Wazungu na Waisraeli wanaumiza vichwa.Nani alikudanganya Wazungu au Waisraeli wana hurumia Waarabu/Wapalestina?
 
Naunga mkono hoja,ni ngumu kuidunda Iran Kwa Sasa ukizingatia strait of Hormuz ambapo IPO kibarazani mwa Iran hupitisha 70% ya nishati duniani.Akiitumia vizuri hiyo kete Dunia itaingia matatizoni na ukizingatia nishati ya Urusi walishajiwekea vikwazo.
 
Uchambuzi mzuri.
Labda sijasoma Vizuri andishi, lakini nani anacheza hii victim card?

Israel ndiyo namba 1 kwenye hili, wanakalia ardhi za Wapalestina, wame-blockade Kila aina ya huduma ya kijamii, wamefurasha watu kuwa wakimbizi na hawataki warudi YET yeye anataka aonewe huruma na kupewa blank check afanye anachotaka kisa mauji ya Jews yaliyifanywa na manazi!

Two wrongs doesn't make one right!

Nije kwenye mtizamo wangu kuhus Iran -Israel war!
Israel ni favourite in every sense akisaidiwa kwa Kila jambo na US.
Yes wanaweza kupiga nuclear reactors za Iran, miundo mbinu ya mafuta nk.
But hawataweza kuyadhuvuti makombora yote ya Iran! Hapa Kuna issue, Israel ni NCHI ndogo Kila kitu kiko-concentrated kwenye maeneo madogo!
Hivyo shambulizi la kutapatapa la Iran linaweza kuwa na irreversible consequences kwa Israel!

Hii ina kumbusha scenario ya North na South Korea!
 
Israeli ni taifa la kijinga sana hawajui mabillion wanayopewa yanatokana na uwekezaji kwenye mafuta na ges inayozalishwa hapo mashariki ya kati ..tuone kama hapo pakifungwa atapewa hata sent tano ...unakata mkono unaokulisha ww mwenyewe
 
Nimesoma
Nitarudi kuweka hoja. Ngoja nikapekue shajara kwanza
 
Umenena vyema. Katika angle hiyo. But mimi nimeeleza katika angle kubwa zaidi. Angle ambayo ninaiongelea ni USA kuweza kuitawala mashariki ya Kati kupitia Israel Victim Card. Kitu hicho kinagonga mwamba kwa sababu Iran naye anatumia hiyohiyo Card kuweza ku Control Expansion ya USA hapo Mashariki ya kati.

Sadam Hussein aliweza kupigwa kwa sababu hakuwa na hiyo Card. Eneo la Israel kujitawala limeweza kudhibitiwa na Iran kutokana na yeye kuwa anamilki karata hii.

Malengo ya Uingereza na USA yanagonga mwamba kila siku maana Iran yupo na Upper Hand.

Israel Kushambulia direct ndani ya Iran ni risk kubwa sana. Maana Iran lengo lake kuu wala siyo hako ka nchi ka Israel. Lengo lake ni kuweza Ku-Control mashariki ya kati. Kushambulia Iran kunaweza kuzalisha mutiple impact:-
1. Economic Impact
2. Political Impact
3. Religion Impact (Iran ameapa kuwa yeye ni Mtetezi wa waislam wote) but in other hand yeye ni Shia ambaye ni against na Suni ambayo inanguvu kubwa hapo Saudia.


It is very complex kuvamia Iran
 
Subiria matusi toka kwa wajaa laana wa kiyaudi wa matombo na samvulachore
 

Strait of Hormuz




Iran inatumia mchanganyiko wa mbinu za kijeshi, kisiasa, kiuchumi, na za kijasusi kudhibiti na kuwa na ushawishi kwenye Strait of Hormuz. Mbinu hizi zinajumuisha uwepo wa vikosi vya wanamaji, uwezo wa makombora, migodi ya baharini, vitisho vya kufunga mlango huo, na vita vya asymmetrical. Kwa kuwa Mlango wa Hormuz ni njia muhimu kwa biashara ya mafuta duniani, uwezo wa Iran kuathiri shughuli katika mlango huu inatoa kadi muhimu katika diplomasia na ulinzi wake dhidi ya shinikizo la kimataifa, hususan kutoka kwa Marekani na washirika wake.
 
Houthis in Yemen



Harakati ya Houthi na msaada wa Iran ni sehemu ya mkakati mpana wa Iran wa kuimarisha ushawishi wake katika Mashariki ya Kati kwa kutumia vita vya "kwa niaba" (proxy wars). Iran inatumia Houthi kudhoofisha Saudi Arabia, kuimarisha nafasi yake ya kijiografia na kisiasa katika eneo hilo, na kudhibiti njia muhimu za kibiashara, hasa Bahari ya Shamu na Ghuba ya Uajemi.
 
Swali kidogo mkuu,hapana unyayo wa Mrusi hapa tukioni.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…