Iran wanaposimama imara, lakini si Watanzania

Iran wanaposimama imara, lakini si Watanzania

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Wa Iran wanawake kwa wanaume wamesimama imara kupigania haki zao.

Hijab haziwahusu wanaume ila haki za wanawake ni jukumu la wote. Kwetu haki zina macho. Ubinafsi umetamalaki.

"Kwetu polisi na wauwe watakavyo alimradi watasema wameuwa panya road hiyo ni sawa."

Mbaya zaidi ubinafsi huo umeota mizizi hata kwa ndugu na jamaa tuliodhani tukipigania nao katiba mpya.

IMG_20220916_233133_436.jpg

Ninakazia: Sisi tatizo letu ni ujinga ambao ukikomaa sawa sawa huitwa upumbavu.
 
Kwamba unataka kusema "wanawake wa Iran ni bora kuliko wanaume wa Tanzakiza"

Siku zote waoga hubaki duniani kuonesha makaburi ya mashujaa

Wanaume kwa wanawake huko wamesimama imara. Ingekuwa kwetu la wanawake liwahusu vipi wenye mikuyenge yao? Ubinafsi mtupu!
 
Haya mambo kuna wakati huwa nahisi yapo kwenye DNA za watu, ambapo huko nje wanazo, ila sisi hatuna, huu ukondoo wetu ni wa ajabu sana.

Nadhani inahitajika step ya kwanza, hata huko wanakoandamana kila siku, naamini nao walikuwa na mwanzo wao, sijui mwanzo wetu utakuja lini.
 
Hili tatizo la uoga limetengenezwa na huyo huyo anaye sema upumbavu ni kipaji.

Wakisema "mbaazi ikikosa maua husingizia jua."

Wanauawa watu na polisi - wapumbavu wanapongeza. Alaumiwe Nyerere?

Kwa hakika tunayo safari ndefu bado.
 
Wakisema "mbaazi ikikosa maua husingizia jua."

Wanauawa watu na polisi - wapumbavu wanapongeza. Alaumiwe Nyerere?

Kwa hakika tunayo safari ndefu bado.
Mwalimu ana makosa yake makubwa sana juu ya huu uoga wa WATANZANIA hata yeye wakati wa uhai wake alikiri kufanya haya makosa, kitu ambacho kwa sasa matokeo yake yame kuwa makubwa yaliyo hasi mwalimu hapaswi kukwepa lawama juu ya hili kama ambavyo tuna msifia kwa mazuri yake pia kwa mabaya aliyo tenda kama hili la uoga lawama zita kuwa juu yake.

Lakini mwisho wa siku tunapaswa kusonga mbele ila kuuondoa huu uoga ni kazi iliyo ngumu sana na siku zote hakuna mabadiliko palipo jaa uoga.
 
Haya mambo kuna wakati huwa nahisi yapo kwenye DNA za watu, ambapo huko nje wanazo, ila sisi hatuna, huu ukondoo wetu ni wa ajabu sana.

Nadhani inahitajika step ya kwanza, hata huko wanakoandamana kila siku, naamini nao walikuwa na mwanzo wao, sijui mwanzo wetu utakuja lini.

Kumbuka vita vya maji maji, mkwawa na wajerumani nk.

Kumbuka Nyerere na Uhuru.

Mtanzania kapigania sana haki. Tatizo ni uwepo wa walio waoga leo. Wenye kutaka wao kuishi, ila kama vipi; wengine:

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi
 
Kama ni DNA ndani ya watu basi aliye zipachika hizo DNA ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere , Mwinyi akafuata akaziongeza, Mkappa akajaza nyingine za kutosha , Kikwete akaongeza, Magufuli akashindilia, Samia akaongeza zake na akazimwagia maji zizidi kunawiri ndani ya WATANZANIA.

: NI upumbavu kwa viongozi kuwa fungia watu mabandani Kama mbuzi wanao subiri kuchinjwa, Amani hailindwi kwa watu kuwa mazezeta na mandondocha hili ni bomu la machafuko na vita viongozi wanao litengeneza wao wenyewe kuna mmoja wao litakuja kumlipukia. tutakuwa kama Congo, Nigeria, Somalia , Rwanda, Sudan n k.
 
Mwalimu ana makosa yake makubwa sana juu ya huu uoga wa WATANZANIA hata yeye wakati wa uhai wake alikiri kufanya haya makosa, kitu ambacho kwa sasa matokeo yake yame kuwa makubwa yaliyo hasi mwalimu hapaswi kukwepa lawama juu ya hili kama ambavyo tuna msifia kwa mazuri yake pia kwa mabaya aliyo tenda kama hili la uoga lawama zita kuwa juu yake.

Lakini mwisho wa siku tunapaswa kusonga mbele ila kuuondoa huu uoga ni kazi iliyo ngumu sana na siku zote hakuna mabadiliko palipo jaa uoga.

Mkuu Nyerere hayupo. Jukumu la kuiweka nchi hii katika misingi inayokubalika kwa maslahi yetu, wanetu na hata ya watoto wa wanetu ni letu sisi leo.

Kwa hakika hii ya kwako ya kumlaumu mtu aliyefariki miaka 20 iliyopita, kwa kushindwa kwetu kufanikisha kupatikana katiba mpya ni mwendelezo ule ule wa kutotaka kuwajibika

Kwa hakika hatuna wa kumlaumu isipokuwa sisi wenyewe:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu
 
Kumbuka vita vya maji maji, mkwawa na wajerumani nk.

Kumbuka Nyerere na Uhuru.

Mtanzania kapigania sana haki. Tatizo ni uwepo wa walio waoga leo. Wenye kutaka wao kuishi, ila kama vipi; wengine:

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi
Kumbe basi kwa kadri hili taifa linavyozidi kuzalisha wasomi, ndivyo ambavyo linazidi kuzalisha tatizo jipya la ubinafsi, hii sijui maana yake nini, ni bora tungebaki wajinga labda tungekuwa na mabadiliko zaidi ya haya, lakini elimu tunazozipata hazitusaidii chochote, ndio zinazidi kuturudisha nyuma.
 
Back
Top Bottom