Iran yaanza uuzaji silaha kimataifa

Iran yaanza uuzaji silaha kimataifa

Kosugi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
16,166
Reaction score
25,197
Tokea mwaka jana mwishoni vikwazo vya silaha vilipoisha kwa Iran,Iran imeonesha drone mpya iitwayo Gaza Doha yenye uwezo wa kutembea maili 1200 sawa na kilometa 2000 na yenye uwezo wa kubeba mabomu mpaka 13.

Tutarajie mpinzani mwingine katika soko la uuzaji silaha.

Pia hii itakua fursa kwa mataifa ya kiarabu kupata silaha toka kwa Mmashariki wa kati mwenzao kwa bei nafuu na zenye ubora zaidi.

Screenshot_2024-03-25-09-35-00-36_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
Screenshot_2024-03-25-09-35-58-23_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Ulisema unaenda kujiridhisha ukaingia mitini
Niliipata Egypt ilianzisha utawala wa kijeshi Gaza 1949-1956,baada ya Suez canal Crisis kuisha Gaza ikakaliwa tena na Egypt kuanzia 1957-1967 ambapo ndipo ilitokea six days war ambayo Egypt aliporwa Sinai na hiyo Gaza kuangukia chini ya Israel administration.
Ila kukaliwa kwa Gaza na Egypt Gaza haikukaliwa kinguvu ama kikoloni yani haikuwa annexed ama occupied kama Israel anavyofanya kwa Ramallah huko West bank.
Kukaliwa ama kuongozwa kwa Gaza chini ya Egypt kunajulikana sababu zake na Yasser Arafat ambaye alikua mkuu wa PLO pamoja na Arab league yote.
Gaza strip ilikua kimbilio la wakimbizi wengi waliokimbia occupation ya jewish settlers huko Haifa na maeneo mengine.
Na hao wakimbizi walikua wakilelewa chini ya gavani ya kijeshi ya Egypt.
Labda sijaelewa ulikua unalenga nini kwa Egypt kuikalia Gaza?
 
yenye uwezo wa kutembea maili 1200 sawa na kilometa 3000+
Umetoa wapi kilomita 3000 plus ?? Maili 1200 hazifiki hata kilomita 2000
Hivi unadhani audience ya JF ni watu wa aina gani yani, na wako wapi wanafanya nini, tunapika komoni kijijini Minjingu?
 
Umetoa wapi kilomita 3000 plus ?? Maili 1200 hazifiki hata kilomita 2000
Hivi unadhani audience ya JF ni watu wa aina gani yani, na wako wapi wanafanya nini, tunapika komoni kijijini Minjingu?
Ungeleta marekebisho kuliko kuleta taarabu.
Ungepungukiwa nini kama ungerekebisha kuwa ni kilomita 2000?
1mile=1.6 kilometres.
1,200miles=?
.
Uki cross multipliii utapata jibu 2000.
Nilikosea katika uandishi.
Ila kilometa 2000 zinafika.
 
Nisaidie ni hiki
Kwanini Egypt iliamua kujenga ukuta mpaka wake na Gaza?
Sijui mkuu.
Unaweza ukatuambia wewe unahisi kwanini Egypt imeongeza ukuta mpaka wa Rafah.
Jibu masahihisho Rafah ukuta ulijengwa toka muda Egypt imeimarisha kuta sio kujenga kwa mara kwanza.
 
Ni swali ambalo unatakiwa kujiuliza wewe na wenzako ambao mnaamini wayahudi ndo wamewafungia Gaza kwenye Gereza wakati mnajisahaulisha kwamba hata Egypt naye amejenga ukuta tena imara zaidi kuliko wa wayahudi.
Unajua kwanini tunasema Israel ameifunga Gaza katika gereza la wazi???
 
Dead wrong!

Maili ni KUBWA KULIKO kilomita

Kwa hiyo maili moja haiwezi kuwa 0.6km

Jiondolee stress kama hisabati zinakutatiza, waulize google!

View attachment 2944491
Nikajua utaleta kitu cha maana still umekuja na blunder kuliko mimi.
Embu soma hii article huwenda ikakuelekeza vizuri.
1Mile = 1.6 kilometres
Nilikosea nilitakiwa niweke 1.6 sio 0.6.
1mile haiwezi ikawa sawa na 1000 kilometres umeingia chaka.
Screenshot_2024-03-25-19-26-50-90_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg
 
Umetoa wapi kilomita 3000 plus ?? Maili 1200 hazifiki hata kilomita 2000
Hivi unadhani audience ya JF ni watu wa aina gani yani, na wako wapi wanafanya nini, tunapika komoni kijijini Minjingu?
Anatuona hatujui kumbe yeye ndo hajui
 
Sikusoma vizuri niwie radhi.
okay, haina shida, mapungufu ya kibinadamu, happens to the best of us. Sasa tunaweza kurudi kwenye mada.

la kwanza, Iran sio Muarabu na hayumo kwenye Umoja wa Waarabu, na haongei Kiarabu, kwa hiyo Waarabu hawatakuwa na nafuu kwenye soko la silaha kwa sababu tu eti Iran kaingia

pili, umesema mwaka jana mwishoni vikwazo dhidi ya Iran viliisha na sasa anaweza kuuza silaha. Nili miss hiyo habari, naomba source nijiridhishe kabla sijakurupuka kuanza kukuchana! You've been warned!
 
Nimesema waarabu watapata nafuu kwa silaha kwasababu Iran ni nchi inayotafuta influence middle east.
-Ungerejelea mfano wa Iran kuifadhili silaha na pesa houthi ambayo ni ya Yemeni na Yemeni ni ya waarabu.
-Pia rejelea Lebanon hizbollah ilivyofadhiliwa pesa na silaha na Iran ilhali Lebnon ni nchi ya kiarabu.
-Pia rejelea mfano wa Syria ambapo Assad alisaidiwa silaha na fedha na wanajeshi na Iran ili asalie madarakani na Syria ni nchi ya kiarabu.
Iran inatafuta influence middle east.
Labda hilo hukulifuatilia.
Haiangaliwi asili bali inatizamwa influence bro.
Iran inatafuta influence middle east.

Usidhani kukosea hesabu ya mile to kilometer basi ni mchache kwenye middle east geopolitics,nop bro.

Turudi kuhusu ushahidi wa Iran kuisha vikwazo vyake vya silaha,nakuletea sasa hivi.
 
okay, haina shida, mapungufu ya kibinadamu, happens to the best of us. Sasa tunaweza kurudi kwenye mada.

la kwanza, Iran sio Muarabu na hayumo kwenye Umoja wa Waarabu, na haongei Kiarabu, kwa hiyo Waarabu hawatakuwa na nafuu kwenye soko la silaha kwa sababu tu eti Iran kaingia

pili, umesema mwaka jana mwishoni vikwazo dhidi ya Iran viliisha na sasa anaweza kuuza silaha. Nili miss hiyo habari, naomba source nijiridhishe kabla sijakurupuka kuanza kukuchana! You've been warned!
Ushahidi huu hapa.
Screenshot_2024-03-25-22-45-20-26_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg
Screenshot_2024-03-25-22-45-26-38_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg
 
Back
Top Bottom