Iran Yabadilisha Msimamo, Yasema Haijasimamisha Uhusiano na IAEA.

Iran Yabadilisha Msimamo, Yasema Haijasimamisha Uhusiano na IAEA.

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Baada ya vituo vyake vya kurutubisha nuclear energy kupigwa, mamia ya askari, wanasayansi na wananchi wake kuuawa, Bunge la Iran lilipitisha azimio la kuvunja uhusiano na IAEA, taasisi ya umoja wa mataifa inayofuatilia masuala ya nuclear energy. Ilitangazwa kuwa Rais wa nchi hiyo. aliridhia na kusaini uamuzi huo.

Lakini sasa waziri wa mambo ya nje wa Iran ametangaza kuwa Iran haijajitoa bali itaendeleza uhusiano na IAEA kwa namna tofauti na ile ya mwanzo.

Pia Iran imesema kuwa ipo tayari kuanzisha mazungumzo na Marekani kuhusiana na programu zake za nuclear.

Bila shaka Iran imegundua haina uwezo wa kushindana na mataifa makubwa, na hivyo kuamua kurudi nyuma, tofauti na msimamo wake wa awali.

Chanzo: Aljazeera.

Iranian Foreign Minister Abbas Araghchi said on Saturday that Tehran was reviewing the details of a possible resumption of nuclear talks with the US.

Separately, Araghchi said any talks with major powers would focus only on Iran’s nuclear activities, not its military capability.

Last month, Israel unleashed large-scale strikes on Tehran’s nuclear sites, its military leaders, nuclear scientists and residential areas, killing hundreds.

Israel claimed its assault on June 13 was undertaken to “roll back the Iranian threat to Israel’s very survival”, according to Israeli Prime Minister Benjamin.

But Iran said the war was an unprovoked aggression in violation of the UN Charter.

In the frenetic days that followed, Iran retaliated, and the two countries exchanged daily barrages.

Araghchi said on Saturday that cooperation with the nuclear agency “will take on a new form” after President Masoud Pezeshkian last week signed a law suspending Iran’s collaboration with the IAEA.
“Our cooperation with the agency has not stopped, but will take on a new form,” said Araghchi.
The new law outlines that any future inspection of Iran’s nuclear sites by the IAEA needs approval by the Supreme National Council
 
Attachments

  • 1752383282728.gif
    1752383282728.gif
    43 bytes · Views: 32
Sasa hujui huyo ni mwanadiplomasi mkuu wa Iran?. Lazima aongee msimamo mgumu kidiplomasia.
Ukishaona neno "BUT" pindi mwanadiplomasia anapoongea, jikite kuelewa sentensi inayofuata baada ya neno hilo na si lile la kabla yake.

Pia kama mwanadiplomasia nguli, lazima atume mixed signals ili kama upande wa pili wa mgogoro uko interested na kutafuta suluhu basi utapickup signal muhimu.
 
Hizo siasa mkuu za kuuma na kupuliza kumbuka azimio lilishspitishwa na bunge na waangalizi wa IAEE wote wameshatimuliwa,huyo ni mwanadiplomasia lazima aongee kauli za kuchanganya ili kupunguza mivutano ya siasa za kimataifa,lakini msimamo huo hauwezi kulegezwa kame!!
 
Bila shaka Iran imegundua haina uwezo wa kushindana na mataifa makubwa, na hivyo kuamua kurudi nyuma, tofauti na msimamo wake wa awali.
Yani mara umesahau kua bunge lisha pitisha sheria na Rais kaidhinisha na sasa Hao ma argent washatimuliwa Iran kamera zao zimetolewa .

Unakuja na maneno ya diplomasia kuyafanya ndio reference yako😁
 
Yani mara umesahau kua bunge lisha pitisha sheria na Rais kaidhinisha na sasa Hao ma argent washatimuliwa Iran kamera zao zimetolewa .

Unakuja na maneno ya diplomasia kuyafanya ndio reference yako😁
Kwa mawazo Yako unafikiri USA na Israel walikuwa wanawategemea hao IAEA wawape taarifa za mipango ya nuclear ya Iran? Unachotakiwa kujua ni kwamba Kila kitu wanachokifanya Iran ndani na nje ya nchi Yao Mossad na CIA wanajua vizuri tu acha waendelee na hiyo mipango muda utasema .
 
Mawazo ya nani ulicho kiandika kinaendana na nilicho comment ila nikuache tu pole
Na kwa taarifa tu kua bado msimamo wao uko pale pale
 
Back
Top Bottom