Iran yafungua lango la Hormuz kupisha mazungumzo ya Israel na Lebanon

iran kabanwa imebidi aachie tu tena bure kabisa hakuna tena mambo ya kulipisha dola milioni 2 πŸ˜‚

View attachment 3574390
We mjinga kweli Iran amewachia as long as kuna ceasefire wakijidai kugusa Lebanon Hormuz inafungwa kwa hio Iran ndio anaye amua iwe bure au walipe hakuna ambaye anaweza kugusa Hormuz huyo kibabu wenu mikono yake ipo kwenye tweeter tu.

Kwa tarifa yako Trump anataka kuwahonga Iran mabillions ili wampe Uranium hahaha we baki na ujinga wako eti Iran kafanyiwa pressure 🀣
 
Waache uongo Trump Kawabata mpaka wameachia wenyewe!! Walijifanya wanajua kumbe Trump kujua zaidi yao hawana namna Bali kufungwa tu Hormuz!!

Wachambuzi Uchwara wameachia wenyewe waarabu-koko wa Bonyokwa wanajifanya kumpamba Iran Eti kufungua Hormuz kutisha usitishwaji wa mapigano huko Lebanon wakati si Kweli kabisa.

Iran kafungua mwenyewe baada ya mbinyo wa Marekani wala sivinginevyo!!
 
Najua inauma ila kubali tu,ile block ya marekani haikuwa mchezoo
Usiongee mambo kishabiki tangu usitishaji wa vita mlango ulifunguliwa kama moja wapo ya makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki 2 ,ila Iran aliufunga tena baada ya Israel kukiuka makubaliano kwa kuendelea kushambulia Lebanon.
Sasa jana Israel imekubali kusitisha mashambulizi dhidi ya Lebanon ndo maana Iran na yenyewe imerudi kwenye makubaliano ya kuuweka wazi huo mlango na ndio maana wamesema umefunguliwa kipindi cha sitisho la mapigano tu inamaana muda ukiisha kama kutakuwa hakuna makubaliano mapya mlango utafungwa tena.

Alafu huo uzio wa Trump una siku 4 tu sasa unategemea hizo siku nne zinatosha kushinikiza Iran kubadili msimamo?
Tatizo nyinyi mlikuwa mnaamini kuwa Marekani ni zaidi ya mungu huwa hawashindwi kitu ndo maana mpaka sasa hamtaki kuamini kuwa hii vita imeiendea kombo marekani tofauti na malengo yake..
Na nina uhakika hata Trump huko aliko atakuwa anajutia pakubwa sana kuanzisha vita hivi maana vimekuja kufichua kuwa kumbe nguvu ya marekani ina mipaka tofauti na propaganda zao walizo kuwa wakitumezesha miaka mingi.
 
US ni giant sana, China pamoja na ukaribu wote na Iran na agreements kibao wame Saini ila amekuwa akichungulia tu mwenzake akidudwa

Strait of Hormuz is completely opened for commercial vessels
Lakini pia trump still anadai kuwa blockade itaendelea until makubaliano yapite
 
Na pia umefunguliwa kwa Masharti, Meli zote lazima zipite njia ambayo Jeshi la Iran imepanga, na sio Meli zote zitaruhusiwa kupita, Civilian wanaopita hapo pia wanatakiwa wakaguliwe.
zinapita njia ambayo irani imepanga kwa sababu eneo jingine la ule upande wa oman,jeshi la irani limetega mabomu chini ya maji.
 
Israel alichomfanyia Iran kupitia kwa mshirika wake Hezbola ndicho hichohicho Iran alikuwa akikifanya kwa washirika wa marekani (waarabu). Yaani ukitandikwa, wewe unamtandika mshirika wa anayekupiga. Mwenyewe atakubali mzungumze tu!.
 
Iran kafungua huo Mlango je kule Malawi kusini mafuta yatashuka Bei ?
 
Hakuna kizuwizi chochote pale mana mnunuwaji mkubwa wamafuta ya iran ni China,China ambayo inanunua mafuta zaidi ya %85 ya mafuta ya iran,unakumbuka juzi Trump ametangaza kwamba Meli za mafuta ya China hazitazuwiliwa inamana biashara kati ya Iran na china inaendelea kama kawaida sasa USA anazuwia meli za nchi gani?
 
zinapita njia ambayo irani imepanga kwa sababu eneo jingine la ule upande wa oman,jeshi la irani limetega mabomu chini ya maji.
Sasa marekani si wana control hilo eneo si wategue hayo mabomu ili meli zipite
Au khadija Turampet alikua anatupiga za chembe???
 
Nilisema Trump alicheza kete vizuri,kitendo Cha kupiga block Kwa Meli za Iran ilikuwa kilio Cha kusaga meno Kwa Iran
Embu ficha ujinga wako basi. Iran imeufungua huo mlango KWAAJILI YA LEBANON VITA ISIMAME.
Iran haathiriki maana ana bahari ambayo anachangia na nchi nne ikiwemo Urusi ambayo ni Caspian. Huko anafanya biashara zake zote na kupitisha mahitaji yako yote muhimu. Aya Jumapili ameufunga tena huo mlango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…